Tundu Lissu hakujua kuwa wazungu kwa sasa hawaweki ''mayai yote'' katika kapu moja!

Hivi ukinunua ndege kwa wazungu, kwa 'cash', halafu wazungu waka'kutulija', ... hizo spea za ndege utazitoa wapi?
1607581786671.png
 
Ni dhana kwani wewe huoni? katiba na sheria zinavyofinyangwa wewe huoni? watu kukaa kimya haimaanishi wana amani!
Ukiona unapita mbele za watu wanaguna lakini hawaongei tambua kuwa kuna tatizo, miguno imezidi rudini nyuma muone ni wapi mnajikwaa mparekebishe,sio hizi cheap propaganda haziwasaidii kitu.
Na kama unajua kutizama mbele mwendelezo unazidi kuonyesha kuwa kadiri miaka inavyo songa mbele chaguzi kwa CCM zitazidi kuwa ngumu sana, mfano rahisi ni huu, Miaka mitano iliyopita mlipiga marufuku vyama vya upinzani visifanye siasa na ili wasisikike kabisa mlichukua hatua zaidi 1. mkaondoa bunge live 2. mkavikandamiza vyombo vya habari Radio/TV visiseme kuhusu wapinzani wenu na vitangaze mafanikio yenu hakika mlifanikiwa sana katika haya, ambayo nia yake kuu ilikuwa kuondoa kabisa ufahamu wa wananchi kuhusu upinzani, 3. CCM na serikali ilijipanga kuleta maendeleo na ambayo ni dhahili yanaonekana hakuna ubishi na yote haya ilikuwa ushindi wa uchaguzi 2020 upatikane bila jasho.
Kwa ghafra na mshituko kubwa mlijikuta mnapambana na upinzani mkubwa kuliko wa 2015.
Msipo kaa chini na kuyapatia majibu haya mwaka 2025 itawabidi CCM wawe chama cha kijeshi ili washinde uchaguzi, tafuteni mzizi wa tatizo ni nini? kwa nini hamkubariki richa ya mazuri mnayotenda,kuna mahali mnafeli. kama hayo mazuri yameshindwa kuwabadiri watu mna,dhani propaganda ndio zitawafaanya mkubalike?
Mkuu;
Umeandika maelezo marefu yenye hoja za kifikirika na kinzani ambazo hazina uhalisia!
 
Siasa za kimataifa zimebadilika sana tokea kuibuka kwa taifa la China kiuchumi na kutishia uchumi wa muungano wa nchi za Ulaya na Marekani.

Kuibuka kiuchumi kwa nchi ya China kumesababisha mzani wa maamuzi kutoka nchi za Ulaya na Marekani kwa nchi zenye uchumi wa chini na kati kama Tanzania yafanyike kwa uangalifu mkubwa.

Kuibuka kwa China kumewafanya wazungu wa nchi za Ulaya na Marekani waanza kufanya siasa za ''kutofungamana na upande wowote'' ndani ya vyama vya siasa katika nchi hasa za Afrika huku wakitumia muktadha wa kibiashara unaosema, ''usiweke mayai yote kwenye kapu moja''. Hii ina maana kwamba usiwekeze katika eneo moja pekee. Unatakiwa kutawanya uwekezaji wako katika maeneo tofauti tofauti ili uwekezaji mmoja ukianguka mwingine utaendelea kukuzalishia.

Wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani kwa sasa wanajua dhana ya ''World Order'' haipo tena.

Wazungu walipomwambia Tundu Lissu wako nyuma yake na wakamsafirisha katika nchi mbali mbali za Ulaya na Marekani kutoa mihadhara inayohusu siasa za Tanzania ili apate uungwaji mkono, alidhani wazungu wameweka ''mayai yao yote'' kwenye kapu lake!

Tundu Lissu kwa kutojua siasa za sasa za nchi za Ulaya na Marekani, alianza kutamba huku akiiambia dunia, ''Western world is done with Magufuli regime''! Magufuli regime has been isolated not only in EA and SADC but in all democratic world!

Kwa kuamini wazungu wameweka ''mayai yao yote'' kwenye kapu lake, Tundu Lissu akaingia kwenye kampeni nchini akijua wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani watahakikisha utawala wa Rais Magufuli unaangamizwa kwa yeye kuwa Rais au kutokuwa Rais kwa sababu wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani wako nyuma yake.

Siku ya uapisho wa Rais Magufuli ilikuwa ni siku iliyotuma ujumbe kwa Lissu kuwa ''Western World is not done with Magufuli regime''. Mabalozi wote wa nchi za Ulaya na Marekani walihudhuria sherehe za uapisho wa Rais Magufuli kule Dodoma. Na kwa kutaka kuonyesha kuwa walihudhuria, walitoa official statement kuzieleza nchi zao.

Kwa sasa tunaona mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani wakianza kufanya kazi na serikali ya Rais Magufuli kwa niaba ya serikali za nchi zao. Juzi tulimuona balozi wa nchi za Ufaransa akitoa pongezi kwa Rais Magufuli na kuahidi ushirikiano wa karibu.

Mabalozi wengine wameanza kutoa pongezi kwa vyama vya siasa vinavyoungana na serikali ya Tanzania ili kuwa sehemu ya serikali katika kuwatumikia wananchi.

Kwa maana nyingine, Kushindwa kwa Tundu Lissu hata kuwashawishi wananchi kuandamana, wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani walijua mayai waliyoweka kwenye kapu la Tundu Lissu yamevunjika yote na hapo hapo wakageukia biashara nyingine ya mayai waliyoweka kwenye kapu la Rais Magufuli.

Wazungu walichofanya ni kumrudisha Tundu Lissu kule ambako walimtoa (Ubelgiji) ili wasije wakapata lawama kama atapatwa na matatizo nchini yatakayowafanya wao kuhojiwa kwa nini walimleta Tanzania!

Kuna baadhi ya watu eti wameaminishwa na wanasubiri serikali ya Tanzania kuwekewa vikwazo na Rais Magufuli kufikiswa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)! Hawa wajinga watasubiri sana!

Yanayompata Tundu Lissu yalimpata pia Maalim Seif mwaka 2015 baada ya kuamini kuwa wazungu wameweka ''mayai yao yote'' katika kapu lake! Maalim Seif akagomea Uchaguzi wa marudio akitegemea wazungu watakuwa nyuma yake. Baadaye alizunguka duniani akiwaomba wazungu watimize ahadi zao lakini wao wakamwambia hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu Zanzibar kwa sasa kuna amani.

Maalim Seif ametumia uzoefu alioupata mwaka 2015 kutatua tatizo ambalo lilijitokeza tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Wakati akihojiwa na Clouds TV baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif amesema uzoefu waliopata mwaka 2015 umewafunza kuwa huwezi kususia kila kitu kwa sababu kususia huko kuliwaathiri sana.

Wakati akihojiwa na Radio ya Sauti ya Amerika (VOA), Tundu alisema kwa sasa wazungu wanamuambia Tanzania kuna amani lakini yeye anawaambia hakuna amani. Wazungu wanachomwambia kwa sasa Tundu Lissu ndicho kile kile walichokuwa wanamwambia Maalim Seif baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliposusia uchaguzi.

Haishangazi kuona Tundu Lissu anawashambulia sana wale alidhani wako naye ambao wanaungana na serikali ya Tanzania au Serikali ya Mapinduzi, Kwake wanaofanya hivyo wanakuwa wanaua hoja zake kwa wazungu kuwa Tanzania hakuna amani.

Tundu Lissu ajiandae kisaikologia, Ninajua sio muda mrefu CHADEMA wataanza kupokea ruzuku ya serikali itokanayo na kura za wabunge ambazo Tundu Lissu anadai hazitambui! Hata wabunge wa viti maalum waliopitishwa na ''kamati kuu'' wataenda bungeni!

Niliwahi kusema, kwa hulka za Wazungu, Tundu Lissu atakuwa kama mwanasiasa za Venezuela, Juan Guaido. Ukitaka kusoma mada ya Juan Guaido, Gonga link hii;

Kadri siku zinavyoenda, Tundu Lissu atazidi kugombana na wanasiasa wengi anaodhani wanamsaliti bila kujua tatizo ni yeye kudhani kuwa wazungu waliweka ''mayai yao yote'' katika kapu lake!
Watu wana plan za muda mrefu ,muda wa kati na muda mfupi , wewe unawasemea wazungu unawajua au unawasikia ? Hujui plan zao , hujui plan za Lissu unawasemea umekuwa sheikh Yahya . Watu wana plan usifikiri hapo alipofikia Jiwe ndio kafaulu kila kitu , bado Kuna kazi nzito sana .
 
Ukweli mchungu kwa MACHADEMA wote.

Hakuna mtu atawekewa vikwazo
 
Usiweke neno ''watu'' katika mwamvuli wa fikra zako!

Unayeona ni mzaha ni wewe na unajibu ni wewe. Hiyo dhana ya ''watu'' unaitoa wapi au unajaribu kuhalalisha hoja zako kwa kutumia mwamvuli wa ''watu''!

Wewe endelea kujibu ''mizaha'' yangu kama inakupendeza!
Sidhani kama hizo ni fikra zako kama ni zako nawe usingesemea wazungu na kuingia kwenye fikra zao. Kwa sifa nilizonazo za kuweka kupelemba mawazo ya watu kwa maoni yao muonekano wao naweza kuwasemea watu.
Unaosubiriwa ni muda tu watu waanze kutoa ya moyoni. Upinzani wanasubiri wenzao kutoka CCM wanaonza kushughulikiwa kama wanafunzi wa chekechea na kubezwa kama mazuzu hadharani, waje waungane kugomea uonevu unaoendelea. Hapo ndipo utajua wananchi ndio wenye nchi.
Dhiki za wafanyakazi na machungu wanayopitia nayo ni mlipuko mwingine unwsubiri.
Karibu wabunge wote CCM wameiba kura pamoja na Rais wao. Ukimya wa wananchi ni wa kutafakari na kuisikilizia dunia inasema nini. Kama haitakemea watachukuwa hatua hilo lipo wazi. Huu utulivu ni butwaa tu iliyowakumba watu. Hivi ni kweli wizi unaweza kufanyia kijinga namna hii?
Sijui kama unakumbuka Arab spring ilivyoanzia Tunisia. Kwa kinachoendelea Uganda kinaweza kuja kwetu. Kumetulia sasa kwa sababu wanaamini kura zikipigwa dikteta nje ya ulingo. Hivyo kikitokea kama kilichotokea kwetu hali itakuwa mbaya. Na kwetu pia
 
Mkuu vipi unataka kujitoa mhanga?
Usijidanganye,,watanzania ni zaidi ya unavyowafikiria.
Muda haujafika tu tupo kama walivyo wengine. Uvumilivu huwa unamwisho. Ngomq ikilia sana hupasuka. CCM walihisi ni salama sasa hivi kila mtu anayomachungu yake watakuja kuungana na wananchi kudai haki
 
Kwanini walipe billioni kadhaa wakati walituibia trlions?
Huu sini uhujumu uchumi kama mwingine?
Tume ya maridhiano iliyoongozwa na Prf Kabudi wanaweza kua na majibu. Lakini msingi wa comment yangu ni kua makubaliano hayo yalikua ni afadhali ya serikali kwenye uchaguzi mkuu wa 2020. Kama wangekomaa na mapesa yote yale, huku wakiendelea kushikilia makinikia, basi TAL angekua na nguvu ya ajabu kwenye uchaguzi uliopita... Na mabeberu yasingekua na uvumilivu na nguvu ambayo dola ingetumia kuzima wapinzani, hapo ndipo CCM wangeisoma number wanayowasomesha wapinzani.

Nisisitize kwamba Madini,gesi, na mafuta hata kama rasilimali hizi zipo nchini kwako weka mazingira ya wakubwa kuja kuwekeza kwa interest zao... Ukishupaza shingo na kijitia kiburi yatakukuta ya Gadafi. Dunia hii kuna jinsi inavyoendeshwa na wenye nguvu

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom