Tundu Lissu hakujua kuwa wazungu kwa sasa hawaweki ''mayai yote'' katika kapu moja!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Siasa za kimataifa zimebadilika sana tokea kuibuka kwa taifa la China kiuchumi na kutishia uchumi wa muungano wa nchi za Ulaya na Marekani.

Kuibuka kiuchumi kwa nchi ya China kumesababisha mzani wa maamuzi kutoka nchi za Ulaya na Marekani kwa nchi zenye uchumi wa chini na kati kama Tanzania yafanyike kwa uangalifu mkubwa.

Kuibuka kwa China kumewafanya wazungu wa nchi za Ulaya na Marekani waanza kufanya siasa za ''kutofungamana na upande wowote'' ndani ya vyama vya siasa katika nchi hasa za Afrika huku wakitumia muktadha wa kibiashara unaosema, ''usiweke mayai yote kwenye kapu moja''. Hii ina maana kwamba usiwekeze katika eneo moja pekee. Unatakiwa kutawanya uwekezaji wako katika maeneo tofauti tofauti ili uwekezaji mmoja ukianguka mwingine utaendelea kukuzalishia.

Wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani kwa sasa wanajua dhana ya ''World Order'' haipo tena.

Wazungu walipomwambia Tundu Lissu wako nyuma yake na wakamsafirisha katika nchi mbali mbali za Ulaya na Marekani kutoa mihadhara inayohusu siasa za Tanzania ili apate uungwaji mkono, alidhani wazungu wameweka ''mayai yao yote'' kwenye kapu lake!

Tundu Lissu kwa kutojua siasa za sasa za nchi za Ulaya na Marekani, alianza kutamba huku akiiambia dunia, ''Western world is done with Magufuli regime''! Magufuli regime has been isolated not only in EA and SADC but in all democratic world!

Kwa kuamini wazungu wameweka ''mayai yao yote'' kwenye kapu lake, Tundu Lissu akaingia kwenye kampeni nchini akijua wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani watahakikisha utawala wa Rais Magufuli unaangamizwa kwa yeye kuwa Rais au kutokuwa Rais kwa sababu wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani wako nyuma yake.

Siku ya uapisho wa Rais Magufuli ilikuwa ni siku iliyotuma ujumbe kwa Lissu kuwa ''Western World is not done with Magufuli regime''. Mabalozi wote wa nchi za Ulaya na Marekani walihudhuria sherehe za uapisho wa Rais Magufuli kule Dodoma. Na kwa kutaka kuonyesha kuwa walihudhuria, walitoa official statement kuzieleza nchi zao.

Kwa sasa tunaona mabalozi wa nchi za Ulaya na Marekani wakianza kufanya kazi na serikali ya Rais Magufuli kwa niaba ya serikali za nchi zao. Juzi tulimuona balozi wa nchi za Ufaransa akitoa pongezi kwa Rais Magufuli na kuahidi ushirikiano wa karibu.

Mabalozi wengine wameanza kutoa pongezi kwa vyama vya siasa vinavyoungana na serikali ya Tanzania ili kuwa sehemu ya serikali katika kuwatumikia wananchi.

Kwa maana nyingine, Kushindwa kwa Tundu Lissu hata kuwashawishi wananchi kuandamana, wanasiasa wa nchi za Ulaya na Marekani walijua mayai waliyoweka kwenye kapu la Tundu Lissu yamevunjika yote na hapo hapo wakageukia biashara nyingine ya mayai waliyoweka kwenye kapu la Rais Magufuli.

Wazungu walichofanya ni kumrudisha Tundu Lissu kule ambako walimtoa (Ubelgiji) ili wasije wakapata lawama kama atapatwa na matatizo nchini yatakayowafanya wao kuhojiwa kwa nini walimleta Tanzania!

Kuna baadhi ya watu eti wameaminishwa na wanasubiri serikali ya Tanzania kuwekewa vikwazo na Rais Magufuli kufikiswa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)! Hawa wajinga watasubiri sana!

Yanayompata Tundu Lissu yalimpata pia Maalim Seif mwaka 2015 baada ya kuamini kuwa wazungu wameweka ''mayai yao yote'' katika kapu lake! Maalim Seif akagomea Uchaguzi wa marudio akitegemea wazungu watakuwa nyuma yake. Baadaye alizunguka duniani akiwaomba wazungu watimize ahadi zao lakini wao wakamwambia hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu Zanzibar kwa sasa kuna amani.

Maalim Seif ametumia uzoefu alioupata mwaka 2015 kutatua tatizo ambalo lilijitokeza tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Wakati akihojiwa na Clouds TV baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif amesema uzoefu waliopata mwaka 2015 umewafunza kuwa huwezi kususia kila kitu kwa sababu kususia huko kuliwaathiri sana kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Wakati akihojiwa na Radio ya Sauti ya Amerika (VOA), Tundu alisema kwa sasa wazungu wanamuambia Tanzania kuna amani lakini yeye anawaambia hakuna amani. Wazungu wanachomwambia kwa sasa Tundu Lissu ndicho kile kile walichokuwa wanamwambia Maalim Seif baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliposusia uchaguzi.

Haishangazi kuona Tundu Lissu anawashambulia sana wale alidhani wako naye ambao wanaungana na serikali ya Tanzania au Serikali ya Mapinduzi, Kwake wanaofanya hivyo wanakuwa wanaua hoja zake kwa wazungu kuwa Tanzania hakuna amani.

Tundu Lissu ajiandae kisaikologia, Ninajua sio muda mrefu CHADEMA wataanza kupokea ruzuku ya serikali itokanayo na kura za wabunge ambazo Tundu Lissu anadai hazitambui! Hata wabunge wa viti maalum waliopitishwa na ''kamati kuu'' wataenda bungeni!

Niliwahi kusema, kwa hulka za Wazungu, Tundu Lissu atakuwa kama mwanasiasa za Venezuela, Juan Guaido. Ukitaka kusoma mada ya Juan Guaido, Gonga link hii;

Kadri siku zinavyoenda, Tundu Lissu atazidi kugombana na wanasiasa wengi anaodhani wanamsaliti bila kujua tatizo ni yeye kudhani kuwa wazungu waliweka ''mayai yao yote'' katika kapu lake!
 
Utakuja kuzikana hizi mizaha unazoandika. Kimya kingi huwa kina mshindi mkuu. Na Mungu yupo na wenye subira kwani huvuta heri.
Uonevu unazidi tamalaki nawe unauona usizani utaendelea kuvumiliwa kusubiri wazungu.
Mkuu;
Yaani na wewe unajibu ''mizaha'' ninayoandika!

Mungu yupo kwa kila mtu sio kwa wenye subira pekee labda kama hujui kuwa Mungu aliumba binadamu wote!

Uonevu kutamalaki ni dhana tu kulingana na upeo wako!
 
Mkuu;
Nadhani hoja yako haina uhusiano na mada yangu!

Inawezekana umesoma mada nyingine ukawa na jibu lakini badala ya kuliweka kwenye mada hiyo ukakosea na kuweka kwenye mada yangu!
Ina uhusiano...kwa awamu hii mara ngapi tumeshuhudia hawa wahisani wakiitwa mabeberu kwa awamu hii je ni sawa na awamu zilizopita?

Cha kustaajabisha ni pale tu wanapowakodoa mfano uchafuzi mkuu ule ...
 
MsemajiUkweli umenena ukweli ila nguchiro wa JF watabisha tu! Hivi Mshana Jr alienda na Tototundu ubelijiji akamfulie chupi zake? Mbona hasikiki kutamba kama wakati wa kampeni
Mkuu;
Huyo Mshana Jr alijiapiza katika mada zake nyingi kuwa Tundu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania 2020 ije mvua, liwake jua! Baada ya Uchaguzi Mkuu akapotea mazima!
 
MsemajiUkweli Tundu alishafeli tangu pale alipoamini wazungu ndio kila kitu wenye dunia hii

Alifeli kwa kutowajua wa Tanzania aliokua anawaomba kura huku akiwaonyesha wazi kwamba nchi yao sio lolote bila wazungu, watanzania wenye imani hizo sio wapiga kura wala wazalendo na ni wachache sana yeye akiwa mmoja wapo

Alifeli kwa kutojua mabadiliko ya uchumi na siasa duniani akidhani wazungu wangeweza kututesa kwa sanctions na mengine kama hayo. Hakujua kwamba wazungu wanajua kuiwekea nchi hii sanctions ni hasara kwao maradufu

Tundu alijikuta mjuaji asiyejua na watanzania wakampuuza na sasa wazungu wameshampuuza
MsemajiUkweli
😁😁😁😁
 
Maalim yeye amekula shavu tayari,yeye acha aendelee kususa, angerudi Tz tuu angepewape hata Utendaji wa kata
Maalim Seif ametumia uzoefu wake wa mwaka 2015 baada ya kususa akitegemea serikali ya Mapinduzi haitaweza kufanya kazi zake!

Jana Maalim Seif alisema wamejifunza kuwa kususa kunawaumiza wao na sio serikali!
 
lissu hoja zake ni strong mno ila bahat mbaya sana watanzania hawamuelewi.

pia naamin lengo la lissu kutafuta support ya wazungu ni kuifanya TZ tuwe na mfumo huru wa tume ya uchagu ila ndio vile haitakaa itokee labda tuwe na uhuru wa pili mbali na ule wa JK wa kwanza
Hoja za ''Tume Huru ya Uchaguzi'' zinazungumzika nchini lakini njia aliyotumia ya kutegemea wazungu haiwezi kufanikisha adhma yake!
 
Back
Top Bottom