Tundu Lissu hakujua kuwa wazungu kwa sasa hawaweki ''mayai yote'' katika kapu moja!

Ina uhusiano...kwa awamu hii mara ngapi tumeshuhudia hawa wahisani wakiitwa mabebetu kwa awamu hii je ni sawa na awamu zilizopita?

Cha kustaajabisha ni pale tu wanapowakodoa mfano uchafuzi mkuu ule ...
Kwani ni lini wahisani waliacha kuitwa mabeberu? Au hujui maana ya neno mabeberu kwa kiingereza?
 
Asante kwa uchambuzi mzuri, atasubiri sana. Uchaguzi umekwisha, sote tushirikiane kujenga Nchi yetu!
Nawe asante kwa kuchangia katika mada yangu!

Tundu Lissu anasumbuliwa na maneno ya hekima ya Wahenga waliosema, ''akili nyingi huondoa maarifa''

Tundu Lissu ana akili nyingi lakini zimeondoa maarifa!

Ni kweli tushirikiane kujenga nchi yetu.
 
Mkuu;
Yaani na wewe unajibu ''mizaha'' ninayoandika!

Mungu yupo kwa kila mtu sio kwa wenye subira pekee labda kama hujui kuwa Mungu aliumba binadamu wote!

Uonevu kutamalaki ni dhana tu kulingana na upeo wako!
Hata mzaha hujibiwa ili aliyeandika ajitambue kuwa amechokianfika ni mzaha na apate mrejesho kuwa watu wanamuona ni mtu wa mzaha.
 
Acha wamsahau kabisa!

Na Tundu ukifatilia maongezi yake ya juzi anaonekana mwenye jazba, eti mapolisi na maccm jamaa anahangaika sana huko aliko
Yaani kwa sasa kila anayeonekana kushirikiana na serikali anamtolea povu zito?

Sio muda mrefu hata CHADEMA watapeleka wabunge bungeni hata kama sio kina Halima Mdee na kundi lake!
 
Hoja za ''Tume Huru ya Uchaguzi'' zinazungumzika nchini lakini njia aliyotumia ya kutegemea wazungu haiwezi kufanikisha adhma yake!
hizo hoja ni ngumu mno kutekelezeka,maana hata huyo lissu si wa kwanza kulipigia kelele na kutafuta suluhu akiwa inchini.

tangu enzi za kina Dr.slaa walishajadili hayo na wakashindwa.

hvyo kwa lissu kwenda huko ugenn ni sahihi kwa sababu nyumban alishashindwa
 
Matamko yote waliyotoa wazungu kusisitiza utawala bora na kukemea uminywaji wa demokrasia nchini sio ya bahati mbaya, usijidanganye, wanawaonya kweli na msiposikia mtakiona cha mtema kuni.

Mpaka sasa kuna misaada mingi serikali imenyimwa au imepunguzwa toka kwa wazungu na Marekani, zaidi juzi tu Makonda kapigwa stop kwenda Marekani.

Wacha kujiaminisha uongo eti wazungu na marekani wanamuogopa mchina, unataka kusema tukigomewa na hao wawili tunaweza kufanya biashara na mchina na tukapata sawa na kile ambacho tungeweza kupata toka kwa wazungu na wamarekani? wacha kujidanganya.

Mchina peke yake hawezi kufanya biashara na mataifa yote duniani kwa kiwango sawa, lazima wapo watakaopata zaidi na watakaopata kidogo.

Zaidi hata huyo mchina mwenyewe mara nyingi anatupa mikopo ambayo mbeleni lazima tuilipe, sasa sijui unampendea nini.
 
Hata mzaha hujibiwa ili aliyeandika ajitambue kuwa amechokianfika ni mzaha na apate mrejesho kuwa watu wanamuona ni mtu wa mzaha.
Usiweke neno ''watu'' katika mwamvuli wa fikra zako!

Unayeona ni mzaha ni wewe na unajibu ni wewe. Hiyo dhana ya ''watu'' unaitoa wapi au unajaribu kuhalalisha hoja zako kwa kutumia mwamvuli wa ''watu''!

Wewe endelea kujibu ''mizaha'' yangu kama inakupendeza!
 
hizo hoja ni ngumu mno kutekelezeka,maana hata huyo lissu si wa kwanza kulipigia kelele na kutafuta suluhu akiwa inchini.

tangu enzi za kina Dr.slaa walishajadili hayo na wakashindwa.

hvyo kwa lissu kwenda huko ugenn ni sahihi kwa sababu nyumban alishashindwa
Nadhani hujui kuwa kwenye bunge la katiba kulikuwa na suala la ''Tune Huru ya Uchaguzi'' lakini upande mwingine ukatoka nje kwa sababu tu ya hoja ya serikali tatu!

Badala ya kulegea sharti la serikali tatu ili wapate ''Tume Huru ya Uchaguzi'' lakini wao wakaamua kutoka nje ya bunge!

Matokeo yake ndio haya ya kina Tundu Lissu kwenda kuomba ''Tume Huru ya Uchaguzi'' kupitia kwa wazungu!
 
Hao wazungu wakiwakosoa tena mnawaita mabeberu ila bakuli mnapokea!
Enda kwenye hoja achana na bakuli, kwani wewe ukipewa pesa hupokei?
Ila usinyanyaswe kwa ajili ya kupewa pesa kwa kudhalilisha utu wako.
Tunachotaka ujibu hoja kama una ona kasema uongo sehemu, hapa hajasemea mambo ya bakuli.
Muwe mnatumia akiri kidogo hizo mlizo baki nazo.
 
Nafuraia sana kuona kwamba wasomi ni mbumbu kuliko ambao hawakusoma.
Je,uchaguzi wetu unakidhi sifa za kuitwa Uchaguzi wenye kufuata taratibu za kidemokrasia?
Je,mleta mada unaweza kutueleza kwanini Uchaguzi wa Rais haupingwi mahakamani?
Mwisho, hivi wazungu wanaitegemea Tz kwa mambo yapi kua bila Tz wazungu wataishi maisha magumu?
 
Matamko yote waliyotoa wazungu kusisitiza utawala bora na kukemea uminywaji wa demokrasia nchini sio ya bahati mbaya, usijidanganye, wanawaonya kweli na msiposikia mtakiona cha mtema kuni.

Mpaka sasa kuna misaada mingi serikali imenyimwa au imepunguzwa toka kwa wazungu na Marekani, zaidi juzi tu Makonda kapigwa stop kwenda Marekani.

Wacha kujiaminisha uongo eti wazungu na marekani wanamuogopa mchina, unataka kusema tukigomewa na hao wawili tunaweza kufanya biashara na mchina na tukapata sawa na kile ambacho tungeweza kupata toka kwa wazungu na wamarekani? wacha kujidanganya.

Mchina peke yake hawezi kufanya biashara na mataifa yote duniani kwa kiwango sawa, lazima wapo watakaopata zaidi na watakaopata kidogo.

Zaidi hata huyo mchina mwenyewe mara nyingi anatupa mikopo ambayo mbeleni lazima tuilipe, sasa sijui unampendea nini.
Tunasubiri tuone Rais Magufuli akifikishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu(ICC)!

Misaada ni haki yao kutupatia au kutotupatia lakini kwa sasa hawana haki ya kutulazimisha eti Tundu Lissu awe Rais wa Tanzania na kama sivyo basi nchi itawekewa vikwazo vya kiuchumi!
 
Back
Top Bottom