Tundu Lissu: CUF ni chama cha Zanzibar!

Tundu Lissu: CUF ni chama cha Zanzibar!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Mbunge wa Singida Mashariki mh Tundu Lissu,amesema kuwa CUF ni chama cha Zanzibar. Akizungumza kipitia Star tv ktk kipindi kiitwacho MEDANI ZA SIASA NA UCHUMI.

Akihojiwa na mtangazaji wa star tv amesema kuwa hakuna haja ya kutafuta ushahidi kuhusu hilo kwani tangia kuanzishwa kwa vyama vingi nchini Tanzania CUF haijawahi kupata wabunge zaidi ya 3 wa kuchaguliwa huku bara. Hii inaonyesha wazi kwamba CUF ngome yake ni Zanzibar.

Akiulizwa kuhusu CDM kuwa kutokuwa na Wabunge Zanzibar,alijibu kuwa ni kweli ila ukweli ni kuwa uweze kushinda uchaguzi Tanzania huitaji kushinda Zanzibar. Kwanza Zanzibar haina hata kura milioni moja zaidi sana ni kura laki tano,na Jimbo la Ubunge pekee lina zaidi ya kura laki nne.

Huyo ndie Tundu Lissu Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni. Je yawezekana ni kweli CUF ni chama cha Zanzibar?
 
Hivyo vyama vya kisiasa wala haihusu kuwa ni suala la muungano. na tumepeleka kwa nguvu hoja ya kuondolewa katika tume ya katiba, kupitia mabaraza ya katiba (kutoka huku zanzibar).

Siasa huendeshwa kwa kuzingatia sana utamaduni, hulka uchumi na mazingira ya pande husika. ukiangalia hilo tunavurugana sana kusema hili jambo liwe la muungano ukichukulia maanani tofauti kubwa ya misingi niliyoitaja hapo juu.
 
CDM is business entity and not political party.
CCM 😕:thumbup::thumbup:😕
Kwa kauli hyo je CDM ngome yk wapi sasa

"Liberal Member"
 
Huyu tundu kweli ugoro mtupu cuf ipo tanzania wakati yeye akiwa niki nda ktk siasa.hoja aliyeitoa haina mashiko kwani kuwa na wabunge wachache bara si kipimo,mbona cuf ina madiwani na wenyeviti wa mitaa kibao bara au kwakua chama chake hakikubaliki zanzibar ndo aneleta sababu mfu. Mbona nccr,tlp,tadea havizungumzii! bila shaka huyu tundu anawashwa. Namshauri akae kitako kudili na chama chake ka siasa zinamshinda akalime viazi ikungi.
 
Acha ugoro wako wewe mama..
Zanzibar ni nchi huru na ni majirani zetu na hakuna lingne zaidi ya hilo.
 
Cuf ni chama pekee chenye wabunge unguja pemba na tanganyika.ccm hawana mbunge pemba, chadema hawana mbunge pemba wala unguja.
 
Kama ni kwelu Leo mh. TUNDU nimekushusha thamani,
hivi kweli lengo letu ni kuondoa hawa mafisadi ccm.
Ama ndio ule wimbo kwamba chadema mnawachukia waislam na watu wenye asili ya uislam kama znz.
 
CUF chama cha Zanzibar, Chadema chama cha maeneo fulani Tanzania Bara.
orodha ya maeneo hayo ni kama ifuatavyo:
Arusha
Dar
Kilimanjaro
Kigoma
Singida
Manyara
Mbeya
Iringa
Mwanza
Shinyanga
Morogoro
...,...n.k
 
Kama ni kwelu Leo mh. TUNDU nimekushusha thamani,
hivi kweli lengo letu ni kuondoa hawa mafisadi ccm.
Ama ndio ule wimbo kwamba chadema mnawachukia waislam na watu wenye asili ya uislam kama znz.

huko kwenu ndio waanzilishi wa kuchoma makanisa,katika history ya Tanzania ni sehemu moja tu ambayo kasisi alipigwa risasi na kuukuliwa.

Tundu anazungumzia economics hapa kwamba hatuwezi kugharimia watu ambao hawafanyi kazi milele.

Humu jamvini kuna mtu ameanzisha suala la Shinyanga(poverty),linganisha Shy na Zanzibar na nani anapata per capita
mgao wa serikali
 
Nampenda Lissu kwa kusema ukweli bila kumumunya maneno. Cuf ni kweli ni chama cha Zanzibar ndio maana hata walio Zanzibar wana kauli tofauti na walio bara chini ya Lipumba(ambao kauli zao haziheshimiwi ndani ya chama)
 
Upo sahihi kabisa, hasa kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Pwani, Kanda ya Nyanda za juu na Kanda ya Kusini, maana katika kanda hizo zote CHADEMA au ina wabunge au ina madiwani, wenyeviti wa serikali za vijiji/mitaa au wote kwa pamoja. Kuwa na macho ni kuwa na uwezo wa kuona siyo kuwa tu na lile duara linaloitwa jicho.

CUF chama cha Zanzibar, Chadema chama cha maeneo fulani Tanzania Bara.
 
Huu ni ukweli mtupu,cuf ni ya nchi jarani pekee.
Kuna watu wanampinga Lissu kwa kuwa mkweli lakini ni vema ukweli ukasemwa wazi.
Lissu hawa wachache wasikutoe kwenye hoja, kwanza wale ni ccm tu.
 
Back
Top Bottom