Tundu Lissu: CCM walivunja kanuni uchaguzi EALA

Sina ubishi na kutumia wingi wenu kufanya mpendalo, lakini mantiki ya kile unachokifanya hapo ndio ulipo mgogoro. Kwa kuwa mko wengi hata mkitaka kutunga sheria ya kuchua wake wa wabunge wa upinzani kisheria ni sawa ndugu.

Ndo manake, au wewe ulifikiri ni kwa nini Vyama hupigania kuwa na absolute majority Bungeni? Kwanza ni mara chache sana kupata Chama kina absolute majority kama vile CCM, hivyo maana yake ni kwamba Upinzani ni dhaifu mno na haukubaliki bado na Watanzania vinginevyo CCM isingekuwa na absolute majority!
 
Inahitajika akili ya kawaida sana kujua kuwa haki inapindishwa. Kama vyama vya upinzani vimepewa kuteua wagombea wa kujaza nafasi walizopewa na kisha bunge linalotawaliwa kwa uwingi na mahasimu wao likayakataa majina hayo, utata huo unamalizwaje? Inawezekana wapinzani wakawachagua wanaokubalika na chama tawala kweli? Na kwa nini wafanye hivyo wakati hiyo ni nafasi yao kuwateua wanaowakubali kuwa watawakilisha matarajio yao? Na ikiwa majina yale yale yaliyokataliwa yataletwa tena bungeni nini kitatokea? Mimi naona wabadilishe kifungu cha wabunge wa upinzani kisomeke wabunge wa CCM ili majina yasiwe yanakataliwa ili tufikishe idadi ya wabunge tisa wanaohitajika. Ndugai kama kazidiwa aombwe Jecha mwenye uzoefu. Yapo mengi ya kujadili yenye maslahi ya taifa kuliko hili. Tungependa kujua kwa mfano waziri aliposema wenye vyeti feki hawatavumiliwa alimaanisha nini?
 
Ndo manake, au wewe ulifikiri ni kwa nini Vyama hupigania kuwa na absolute majority Bungeni? Kwanza ni mara chache sana kupata Chama kina absolute majority kama vile CCM, hivyo maana yake ni kwamba Upinzani ni dhaifu mno na haukubaliki bado na Watanzania vinginevyo CCM isingekuwa na absolute majority!

Kwa tume hii ya uchaguzi tena kwangu naona hata hiyo ccm hiyo unayoita absolutely majority bado wamepunjika. Ilitakiwa hivyo vyama vya upinzani viwe na mbunge mmoja mmoja kama ilivyo NCCR na ACT.
 
Ni aibu sana kwa the 'finest lawyer' kulalamika na kulia mitandaoni.
Wamevurunda wanakuja kuwalisha matango pori wafuasi wao wa mitandaoni ambao wana uwezo mdogo sana wa kufikiri.
Haiingii akilini kwa chama kinachojiita cha kidemokrasia kuleta watu wapite bila ya kupingwa

Mkuu, mwenzako amekuja na kanuni, na ameeleza zinasema A, B,C...

Nilitegemea na wewe utupe darasa ya kuwa si kweli bali kanuni zinasema C, A, B

Hebu, jaribu kusoma tena ulichoandika, je kama hivi ndio tunavyoenda kujenga hoja huko huko EAC?
 
Kwa tume hii ya uchaguzi tena kwangu naona hata hiyo ccm hiyo unayoita absolutely majority bado wamepunjika. Ilitakiwa hivyo vyama vya upinzani viwe na mbunge mmoja mmoja kama ilivyo NCCR na ACT.

Bla bla blah kila siku kutafuta visingizio, kwani nini Wasimamizi wa Kimataifa waliosimamia Uchaguzi wetu kuanzia wa AM, SADC, AU, EU mpaka USA na Uchina hakuna hata mmoja aliyesema Tume yetu ya uchaguzi haikutenda haki? Na hawa walikuwepo site kabla hata ya uchaguzi haujaanza, lkn wote ripoti zao za mwisho hakuna waliposema Tume yetu ya uchaguzi haikutenda haki, final report ilisema ,,the election was free and fair"!
 
Wamevunja kanuni ipi? CHADEMA walileta majina mawili na kura zikapigwa, hawakushinda. sasa kanuni gani imevunjwa? Mkubali mmejifunga goli wenyewe na mjifunze.
Hahaha tatizo la watanzania wasiojielewa,kwan huko eala chadema inapata faida gani,au hujui faida ni ya nchi,bashite anza evening class
 
Mimi nilishangaa sana,kwa kweli ushabiki wangu kwa chama changu CCM unanipotezea amani kwenye nyumba yangu na familia yangu!!Ushawishi wa mke wangu unewafanya watoto na ndugu wa karibu kuwa wafuasi wa chadema na UKAWA.

Mambo haya ya aibu yanapotokea,yanfanya sebule zetu kuwa chungu kukaa na kujadiliana na watoto juu ya mustakhabali wa nchi yetu.Katika hali hii,baba unakosa ujasiri wa kukitetea chama chako mbele ya watoto.

Mambo mengine yapo wazi kabisa...Practice ya uchaguzi mara baada ya mfumo wa vyama vingi,kukiwa na mgombea mmoja au wawili katika uwiano wa nafasi zinazogombewa,basi mgombea/wagombea wanapita bila kupigwa.

Ndio maana JPM uchaguzi wa ubunge huko nyuma alipita bila kupingwa,na hakukuwa na kura za NDIYO na HAPANA.William Lukuvi 2010 alipita bila kupingwa kwao Isimani sbb hakuwa na mpinzani na yeye ni mmoja katika uwiano wa nafasi moja,kadhalika January Makamba na Hawa Ghasia.

Kwa "authority" hii ya bunge katika uchaguzi wa EALA,mwaka 2020 wabunge wa CCM watakaakosa washindani,itabidi wananchi tupige kura ya NDIYO AU HAPANA.

Classmate wangu Kashilila kaniangusha sana,hata tukikutana kugonga mvinyo tamwambia aitunze heshima yake hata kama anatumwa.Siasa zina leo na kesho
Mzee hongera umemwaga nondo by the way haya majina tunayotumia huku JF yanatufanya tunaonekana ni vijana wadogo kumbe ni watu na heshima na umri zetu!!! Hongera sana
 
Mimi nilishangaa sana,kwa kweli ushabiki wangu kwa chama changu CCM unanipotezea amani kwenye nyumba yangu na familia yangu!!Ushawishi wa mke wangu unewafanya watoto na ndugu wa karibu kuwa wafuasi wa chadema na UKAWA.

Mambo haya ya aibu yanapotokea,yanfanya sebule zetu kuwa chungu kukaa na kujadiliana na watoto juu ya mustakhabali wa nchi yetu.Katika hali hii,baba unakosa ujasiri wa kukitetea chama chako mbele ya watoto.

Mambo mengine yapo wazi kabisa...Practice ya uchaguzi mara baada ya mfumo wa vyama vingi,kukiwa na mgombea mmoja au wawili katika uwiano wa nafasi zinazogombewa,basi mgombea/wagombea wanapita bila kupigwa.

Ndio maana JPM uchaguzi wa ubunge huko nyuma alipita bila kupingwa,na hakukuwa na kura za NDIYO na HAPANA.William Lukuvi 2010 alipita bila kupingwa kwao Isimani sbb hakuwa na mpinzani na yeye ni mmoja katika uwiano wa nafasi moja,kadhalika January Makamba na Hawa Ghasia.

Kwa "authority" hii ya bunge katika uchaguzi wa EALA,mwaka 2020 wabunge wa CCM watakaakosa washindani,itabidi wananchi tupige kura ya NDIYO AU HAPANA.

Classmate wangu Kashilila kaniangusha sana,hata tukikutana kugonga mvinyo tamwambia aitunze heshima yake hata kama anatumwa.Siasa zina leo na kesho

Kweli inasikitisha sana, kama ndo hivyo Tanzania bado sana... na ni better Chadema wazipotezee tu hizo nafasi ili ushawishi wa Tz uwe mdogo... by the way wanafanya haya yote kwa faida ya nani?? Siamin kama JPM anaweza kushauri vitu kama hivi.... sasa wanamkomoa nani... CCM jifunzeni kufanya kama mioyo yenu inavyowataka kufanya. Msiwewa kuamua kwa kuongozwana mihemko... na msidhanie mmemkomoa Wenje wala Masha ila mmetukomoa wote na mnafifisha matumaini yetu. Mmetumwa kwenda kutuwakilisha wananch bali nyie sijui mwamuwakilisha nani huko. Very disappointing kwa kweli
 
Siku zote nimewaambia kuwa 'uchawi" ni wivu wa kutotaka kuona mwenzako anafanikiwa hata kama mafanikio yake ni kwa maslahi ya wengi ukiwemo wewe. Viongozi wa CCM ni sawa na 'Genge la Wachawi' na Wachawi hawana soni wanapotenda yasiyopasa!!!
 
Bla bla blah kila siku kutafuta visingizio, kwani nini Wasimamizi wa Kimataifa waliosimamia Uchaguzi wetu kuanzia wa AM, SADC, AU, EU mpaka USA na Uchina hakuna hata mmoja aliyesema Tume yetu ya uchaguzi haikutenda haki? Na hawa walikuwepo site kabla hata ya uchaguzi haujaanza, lkn wote ripoti zao za mwisho hakuna waliposema Tume yetu ya uchaguzi haikutenda haki, final report ilisema ,,the election was free and fair"!

Unajua unachokisema ama unaleta ubishi wa mshipa? Wasimamizi hao hao wakimataifa walikuwa ZnZ na inafahamika ni nini walisema kuhusu uchaguzi wa kule. Unaweza kunionyesha mahali ulipowaunga mkono? Kumbuka suala hilo ndio baadhi ya mambo mpaka leo yametuacha na uhusiano mbaya na wahisani. Kama unatafuta ushindi basi umeshinda lakini kama ni uhalisia ni bora ukakaa kimya tu.
 
aibu ya bunge letu sjui nani tu atakuja kujibu mbele ya vizazi 6 mbele,wenzetu abroad walifikiri sana kuhusu future ya vizazi vyao
 
Anaandika mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh Tundu Lissu!

Wakubwa habari za asubuhi.

I'm still licking my wounds, kama wasemavyo Waingereza.

Pamoja na kwamba vumbi la uchaguzi wa jana bado limetanda, naomba niseme yafuatayo juu ya uzoefu wa hizi siku chache zilizopita.

1) Kuna wanaodai tulikosea kutokuangalia gender balance ndio maana tumeshindwa.

Hapana.

Kosa letu sio kutokuzingatia jinsia. Kosa letu kubwa na lisilosameheka ni kuwa chama kikuu cha upinzani dhidi ya MaCCM. Na tumelifanya kosa hilo tangu mwaka 2010.

Wenzetu wa CUF nao walishawahi kufanya kosa hili kubwa miaka ya nyuma na mnakumbuka yaliyowapata. Na NCCR Mageuzi kabla ya CUF.

2) Kosa letu la pili ni kuwa chama kikuu cha upinzani lakini bila kuwa na nguvu ya kutosha bungeni kuzuia njama za MaCCM ndani na nje ya Bunge.

Ni hivi. Sisi wa UKAWA tupo 116, MaCCM yako 252 na bado wanajiongeza i.e. Salma Kikwete na wengineo watokao Magogoni. Wao wana 70%, sisi tuna 30% ukihesabu kila mtu aliyeko bungeni.

Kwa balance hii hata tukifanyaje tutaonewa tu. Na chochote tutakachopata itakuwa ni kwa fadhila yao.

Kwa sababu ya balance hii, hawahitaji hata kuheshimu sheria na kanuni za Bunge.

Kati ya Jumamosi na jana wamebadilisha sheria na kanuni za uchaguzi kwa namna ambayo inatisha.

In fact, hawakufuata chochote kilichoandikwa kwenye Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge wa EALA. Badala yake, walibadilisha kanuni kadri mchezo ulivyokuwa unaendelea na kadri ya mahitaji ya maslahi yao.

Kanuni inavipa vyama vya siasa haki ya kuweka mgombea mmoja hadi watatu kwa kila nafasi inayogombaniwa. Ndivyo tulivyofanya. Machoni pao tulikosea sana.

Kwa practice ya Bunge letu, wagombea wasiokuwa na mpinzani hupita bila kupingwa. Na hii ndio sheria yetu ya uchaguzi hata nje ya Bunge. Jana imebadilishwa.

Wagombea wa CUF walikuwa wanne kwenye nafasi moja wakati kanuni zinasema maximum ni wagombea watatu kwa nafasi moja.

Watatu kati ya hao hawakuwa na fomu za uteuzi zilizosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF kama ilivyotakiwa na kanuni. Bali, kwa kauli ya Katibu wa Bunge na Msimamizi wa Uchaguzi, majina yao yalitokea NEC.

NEC inahusikaje na uteuzi wa majina ndani ya vyama, mimi sijaelewa bado.

Kura zilipigwa kwa utaratibu usiokuwepo kwenye kanuni kabisa. Hakuna upigaji wa kura ya ndio au hapana kwenye uchaguzi wa EALA. Lakini wamepigia wagombea wetu au hapana.

Hakuna utaratibu wa wengine wanapigiwa kura ya ndiyo tu lakini wengine wanapigiwa ndio au hapana kwenye karatasi hiyo hiyo moja ya kura. Jana wagombea saba wamepigiwa kura za ndio tu, wawili wamepigiwa ndio au hapana.

Kanuni inasema usipochagua wagombea tisa basi kura yako imeharibika. Jana wamepigia kura wagombea saba tu na hakuna kura yoyote iliyoharibika.

Kanuni inaelekeza kura kuwa ya siri lakini jana usiku hakukuwa na kura yoyote ya siri.

Na mengine mengi.

Yote haya yanatokana na dominance ya MaCCM bungeni. Na juu ya yote haya, ongezea la Msimamizi wa Uchaguzi ambaye anajifanya ni refa wa mchezo huu lakini kiuhalisia ni kocha wa timu ya MaCCM.

Katika mazingira haya, je, watu hawa wataitisha uchaguzi mwingine ili kujaza nafasi mbili za CHADEMA zilizobaki???

Hili ni kwa wale wanaofikiria tukiongeza jina moja au mawili basi shida itakwisha na MaCCM yatatupatia nafasi zetu. Mimi sina jibu lake lakini hisia zangu zinaniambia hii imetoka.

Nitaendelea wakati mwingine.
Tundu usijioshe,hujakishauri chama chako vizuri,na ubishi unaozusha ni very unprofessional !
 
Wale maadui Watatu Nyerere aliowataja alisahau moja wanatakiwa kuwa wanne CCM ni adui namba nne
 
Unajua unachokisema ama unaleta ubishi wa mshipa? Wasimamizi hao hao wakimataifa walikuwa ZnZ na inafahamika ni nini walisema kuhusu uchaguzi wa kule. Unaweza kunionyesha mahali ulipowaunga mkono? Kumbuka suala hilo ndio baadhi ya mambo mpaka leo yametuacha na uhusiano mbaya na wahisani. Kama unatafuta ushindi basi umeshinda lakini kama ni uhalisia ni bora ukakaa kimya tu.

Zanzibar ni special case nimesahau kuiweka hiyo lkn lkn TZ Bara uchaguzi ulikuwa free and fair kwa mujibu wa Wasimamizi wa Kimataifa na walisema tu tu fix Zanzibar, lkn Bara hakuna dosari!
 
Ni wahuni wote hawa Mkuu wasiojali maslahi ya nchi yetu hata chembe.

Hawa watu laana haitawaacha salama.

Kama inawezekana kubadili kanuni hata hizo nafasi 2 ziende kwao waachieni tu ijulikane moja.

Na la hilo la NEC hata mimi nilipigwa butwaa na kwakweli sikuelewa kabisa liliingiaje katika huo uchaguzi.
 
Chadema hamna Demokrasi mna dikteta anayeteua majina atakayo!! Kwanini msipeleke majina zaidi yakapigiwa kura Kama wenzenu walivyofanya '!!"???
 
Back
Top Bottom