Tundu Lissu: CCM walivunja kanuni uchaguzi EALA

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,903
4,051
Anaandika mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh Tundu Lissu!

Wakubwa habari za asubuhi.

I'm still licking my wounds, kama wasemavyo Waingereza.

Pamoja na kwamba vumbi la uchaguzi wa jana bado limetanda, naomba niseme yafuatayo juu ya uzoefu wa hizi siku chache zilizopita.

1) Kuna wanaodai tulikosea kutokuangalia gender balance ndio maana tumeshindwa.

Hapana.

Kosa letu sio kutokuzingatia jinsia. Kosa letu kubwa na lisilosameheka ni kuwa chama kikuu cha upinzani dhidi ya MaCCM. Na tumelifanya kosa hilo tangu mwaka 2010.

Wenzetu wa CUF nao walishawahi kufanya kosa hili kubwa miaka ya nyuma na mnakumbuka yaliyowapata. Na NCCR Mageuzi kabla ya CUF.

2) Kosa letu la pili ni kuwa chama kikuu cha upinzani lakini bila kuwa na nguvu ya kutosha bungeni kuzuia njama za MaCCM ndani na nje ya Bunge.

Ni hivi. Sisi wa UKAWA tupo 116, MaCCM yako 252 na bado wanajiongeza i.e. Salma Kikwete na wengineo watokao Magogoni. Wao wana 70%, sisi tuna 30% ukihesabu kila mtu aliyeko bungeni.

Kwa balance hii hata tukifanyaje tutaonewa tu. Na chochote tutakachopata itakuwa ni kwa fadhila yao.

Kwa sababu ya balance hii, hawahitaji hata kuheshimu sheria na kanuni za Bunge.

Kati ya Jumamosi na jana wamebadilisha sheria na kanuni za uchaguzi kwa namna ambayo inatisha.

In fact, hawakufuata chochote kilichoandikwa kwenye Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge wa EALA. Badala yake, walibadilisha kanuni kadri mchezo ulivyokuwa unaendelea na kadri ya mahitaji ya maslahi yao.

Kanuni inavipa vyama vya siasa haki ya kuweka mgombea mmoja hadi watatu kwa kila nafasi inayogombaniwa. Ndivyo tulivyofanya. Machoni pao tulikosea sana.

Kwa practice ya Bunge letu, wagombea wasiokuwa na mpinzani hupita bila kupingwa. Na hii ndio sheria yetu ya uchaguzi hata nje ya Bunge. Jana imebadilishwa.

Wagombea wa CUF walikuwa wanne kwenye nafasi moja wakati kanuni zinasema maximum ni wagombea watatu kwa nafasi moja.

Watatu kati ya hao hawakuwa na fomu za uteuzi zilizosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF kama ilivyotakiwa na kanuni. Bali, kwa kauli ya Katibu wa Bunge na Msimamizi wa Uchaguzi, majina yao yalitokea NEC.

NEC inahusikaje na uteuzi wa majina ndani ya vyama, mimi sijaelewa bado.

Kura zilipigwa kwa utaratibu usiokuwepo kwenye kanuni kabisa. Hakuna upigaji wa kura ya ndio au hapana kwenye uchaguzi wa EALA. Lakini wamepigia wagombea wetu au hapana.

Hakuna utaratibu wa wengine wanapigiwa kura ya ndiyo tu lakini wengine wanapigiwa ndio au hapana kwenye karatasi hiyo hiyo moja ya kura. Jana wagombea saba wamepigiwa kura za ndio tu, wawili wamepigiwa ndio au hapana.

Kanuni inasema usipochagua wagombea tisa basi kura yako imeharibika. Jana wamepigia kura wagombea saba tu na hakuna kura yoyote iliyoharibika.

Kanuni inaelekeza kura kuwa ya siri lakini jana usiku hakukuwa na kura yoyote ya siri.

Na mengine mengi.

Yote haya yanatokana na dominance ya MaCCM bungeni. Na juu ya yote haya, ongezea la Msimamizi wa Uchaguzi ambaye anajifanya ni refa wa mchezo huu lakini kiuhalisia ni kocha wa timu ya MaCCM.

Katika mazingira haya, je, watu hawa wataitisha uchaguzi mwingine ili kujaza nafasi mbili za CHADEMA zilizobaki???

Hili ni kwa wale wanaofikiria tukiongeza jina moja au mawili basi shida itakwisha na MaCCM yatatupatia nafasi zetu. Mimi sina jibu lake lakini hisia zangu zinaniambia hii imetoka.

Nitaendelea wakati mwingine.
 
Ongezeni majina kura itapigwa ila hao wa hapana itaendelea kuwa hapana. Kupunguza nafasi za uwakilishi EALA ni pigo kwa CCM kwa sababu kura za Tanzania zitapungua na ushawishi wetu kupungua vilevile.
 
Mimi nilishangaa sana,kwa kweli ushabiki wangu kwa chama changu CCM unanipotezea amani kwenye nyumba yangu na familia yangu!!Ushawishi wa mke wangu unewafanya watoto na ndugu wa karibu kuwa wafuasi wa chadema na UKAWA.

Mambo haya ya aibu yanapotokea,yanfanya sebule zetu kuwa chungu kukaa na kujadiliana na watoto juu ya mustakhabali wa nchi yetu.Katika hali hii,baba unakosa ujasiri wa kukitetea chama chako mbele ya watoto.

Mambo mengine yapo wazi kabisa...Practice ya uchaguzi mara baada ya mfumo wa vyama vingi,kukiwa na mgombea mmoja au wawili katika uwiano wa nafasi zinazogombewa,basi mgombea/wagombea wanapita bila kupigwa.

Ndio maana JPM uchaguzi wa ubunge huko nyuma alipita bila kupingwa,na hakukuwa na kura za NDIYO na HAPANA.William Lukuvi 2010 alipita bila kupingwa kwao Isimani sbb hakuwa na mpinzani na yeye ni mmoja katika uwiano wa nafasi moja,kadhalika January Makamba na Hawa Ghasia.

Kwa "authority" hii ya bunge katika uchaguzi wa EALA,mwaka 2020 wabunge wa CCM watakaakosa washindani,itabidi wananchi tupige kura ya NDIYO AU HAPANA.

Classmate wangu Kashilila kaniangusha sana,hata tukikutana kugonga mvinyo tamwambia aitunze heshima yake hata kama anatumwa.Siasa zina leo na kesho
 
Ni aibu sana kwa the 'finest lawyer' kulalamika na kulia mitandaoni.
Wamevurunda wanakuja kuwalisha matango pori wafuasi wao wa mitandaoni ambao wana uwezo mdogo sana wa kufikiri.
Haiingii akilini kwa chama kinachojiita cha kidemokrasia kuleta watu wapite bila ya kupingwa
 
MaCCM yako tayari Tanzania iwe na wawakilishi wachache kwenye Bunge la Afrika ya Mashariki (wabunge 7) kuliko kuona wawakilishi toka CHADEMA wanaingia kwenye bunge na hivyo kuwa na idadi kubwa ya wabunge tisa.
 
Mimi nilishangaa sana,kwa kweli ushabiki wangu kwa chama changu CCM unanipotezea amani kwenye nyumba yangu na familia yangu!!Ushawishi wa mke wangu unewafanya watoto na ndugu wa karibu kuwa wafuasi wa chadema na UKAWA.

Mambo haya ya aibu yanapotokea,yanfanya sebule zetu kuwa chungu kukaa na kujadiliana na watoto juu ya mustakhabali wa nchi yetu.Katika hali hii,baba unakosa ujasiri wa kukitetea chama chako mbele ya watoto.

Mambo mengine yapo wazi kabisa...Practice ya uchaguzi mara baada ya mfumo wa vyama vingi,kukiwa na mgombea mmoja au wawili katika uwiano wa nafasi zinazogombewa,basi mgombea/wagombea wanapita bila kupigwa.

Ndio maana JPM uchaguzi wa ubunge huko nyuma alipita bila kupingwa,na hakukuwa na kura za NDIYO na HAPANA.William Lukuvi 2010 alipita bila kupingwa kwao Isimani sbb hakuwa na mpinzani na yeye ni mmoja katika uwiano wa nafasi moja,kadhalika January Makamba na Hawa Ghasia.

Kwa "authority" hii ya bunge katika uchaguzi wa EALA,mwaka 2020 wabunge wa CCM watakaakosa washindani,itabidi wananchi tupige kura ya NDIYO AU HAPANA.

Classmate wangu Kashilila kaniangusha sana,hata tukikutana kugonga mvinyo tamwambia aitunze heshima yake hata kama anatumwa.Siasa zina leo na kesho
Hivi huoni aibu kuendelea kujiita mwana-CCM?unataka wafanye nini ndio ujue kuwa hawa jamaa hawafai?! CCM imekuloga?Kama unaelewa yote haya na bado unakumbatia hiki chama,wa vijijini wafanyaje?

Kama Nyerere alikuwa tayari kuikacha CCM iwapo itaacha misingi ya kuanzishwa kwake,nyinyi mnasubiri nini?

Mkuu unanishangaza sana na nyie ndio chanzo cha yote haya kwa kukumbatia hiki chama.

Mimi hata diwani wa CCM kura yangu hawezi kupata.Hiki chama nakichukia sana kwasababu hawa ndio wameifikisha hii nchi hapa ilipo leo hii na hawana moral authority ya kujidai eti leo ndio wanajirekebisha badala ya kuwa jela.
 
Lisu analia lia tu, busara ndogo tu ingeepusha aibu mliyopata jana, mlishaambiwa muongeze wagombea, kuna ugumu kwa hilo. Hivi CDM nzima hauwezi kupata wagombea mahiri 4, wanaume 2 na wanawake 2. Haya ni matatizo ya kujitakia na bunge limewafundisha maana ya demokrasia, bunge si rubber stamp ya maamuzi yenu.
 
Ni aibu sana kwa the 'finest lawyer' kulalamika na kulia mitandaoni.
Wamevurunda wanakuja kuwalisha matango pori wafuasi wao wa mitandaoni ambao wana uwezo mdogo sana wa kufikiri.
Haiingii akilini kwa chama kinachojiita cha kidemokrasia kuleta watu wapite bila ya kupingwa
You're cursed moron son .. You know nothing than being an empty headed claiming to be genius
 
Mimi nashauri kama sheria inataka wabunge wa EALA watoke kila chama chenye sifa na kama hawawezi kuapisha wabunge 7 kutoka nchi moja mpaka watimie 9, basi nashauri CHADEMA wasipeleke majina na waachane na hii issue ili walau wabunge hao waliochaguliwa kwa mbwembwe waendelee kutazama vikao vya bunge hilo kupitia You tube.
 
Diyo siri tena kuwa adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu! ni chama cha Sisiem
 
Back
Top Bottom