Tundu Lissu: CCM walivunja kanuni uchaguzi EALA

HILI JAMBO NI LA KUIAIBISHA TANZANIA NA WATANZANIA. TUNASHINDWA KUHESHIMIANA KWA SABABU YA UCHAMA NA HATUTAHESHIMIKA HATA HUKO EALA. KUNA UWEZEKANO HII NGOMA IKAINGIA EALA AU MAHAKAMA YA EAC KWA MAELEZO KWAMBA KATIKA HAO 7 WALIOCHAGULIWA, UKIONDOA WA CCM, WENGINE WOTEUCHAGUZI WAO NI BATILI. INAHITAJIKA KUWE NA WABUNGE WA UPINZANI EALA - KITU AMBACHO HAKIPO KWA TANZANIA. KWANZA CUF KUNA MGOGORO MKUBWA ULIKO MAHAKAMANI NA HAIJULIKANI NANI KIONGOZI NA NANI SIO. PILI, KATIKA NCHI ZA EAC, LOLOTE LENYE KASORO KWA TANZANIA NI NEEMA KWA WANACHAMA WALIO WENGI EAC. KWA HIYO KESI YOYOTE ITAKAYOPELEKWA PALE, TAZANIA ITASHINDWA NA HAO SABA WANAWEZA KUATHIRIKA AU TUSIWE NA UWAKILISHI KABISA. TANGU LINI CHAMA TAWALA KIKAWA NA SIFA YA KUWACHAGULIA WAPINZANI LILILO JEMA (VICE VERSA IS ALSO TRUE). HALAFU UCHAGUZI MMOJA LAKINI UNA KANUNI TOFAUTI TOFAUTI- HII NI KASORO KUBWA. WEKENI UVYAMA PEMBENI PALE KWENYE MASLAHI MAPANA KWA TANZANIA.
 
Ni aibu sana kwa the 'finest lawyer' kulalamika na kulia mitandaoni.
Wamevurunda wanakuja kuwalisha matango pori wafuasi wao wa mitandaoni ambao wana uwezo mdogo sana wa kufikiri.
Haiingii akilini kwa chama kinachojiita cha kidemokrasia kuleta watu wapite bila ya kupingwa
Hujaelewa kinachozungumziwa, umekuja na majibu yako
 
Tundu Lissu umeeleweka, umeandika matatizo lakini hujatoa ufumbuzi, mimi nadhani kwa andiko hili ni wakati sasa CHADEMA mkabadili mikakati yenu badala ya kulalamika kila siku muamue kuwekeza nguvu nyingi kwa wananchi ili 2020 hata kama hamtachukua nchi basi uwiano wenu bungeni uweze kuwapa nguvu ya kufanya maamuzi..
Vinginevyo mtaendelea kulalamika kila siku na mwisho wa siku na nyie yatawakuta ya CUF na NCCR..
Ombi langu kwenu, acheni kuingia kwenye mtego wa CCM ambao wameamua kutumia udhaifu wa mihemuko yenu kuwabambika kesi kila uchao ili msiweze kupata nafasi ya kukinadi chama kwa wananchi..
Kama upinzani mtaweza kujipanga vizuri, na kutumia vizuri turufu ya udhalimu wa CCM mnaweza kuwa na nguvu mno, na nguvu yenu kubwa itakuwa ni wananchi, mmeshakuwa na nguvu mijini.. Nendeni vijijini ambako bado CCM wanajivunia, mikoa kama ya Tabora, Pwani, Katavi, Rukwa, Iringa na mingine mingi huko vijijini sijaona Upinzani ukiweka mikakati madhubuti kuwafikia watu wake..
Kama kweli mnataka kuchukua nchi au kuwa wapinzani wenye nguvu ni wakati sasa mbadili mikakati yenu...
 
Hawa watu laana haitawaacha salama.

Kama inawezekana kubadili kanuni hata hizo nafasi 2 ziende kwao waachieni tu ijulikane moja.

Na la hilo la NEC hata mimi nilipigwa butwaa na kwakweli sikuelewa kabisa liliingiaje katika huo uchaguzi.
Kwani waliochaguliwa sio Chadema
 
Back
Top Bottom