Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani

Kwa ushahidi wote huu wa wazi, kwanini tusiamini kuwa rais sasa anaongoza nchi kikanda na kikabila huku akionesha chuki za wazi kwa baadhi ya kanda?
Kwa mujibu wa maelezo ya mhe.Tundu Lissu ni kuwa viongozi wakuu wote wa vitengo muhimu rais Magufuli ameteuwa watu wa kanda ya Ziwa kama ifuatavyo;

1. Mwanashweria Mkuu wa serikali (Kanda ya ziwa)
2. Mwendesha mashtaka wa serikali (Kanda ya ziwa)
3. Kaimu jaji mkuu (Kanda ya ziwa)
4. Mkuu wa majeshi (Kanda ya ziwa)
5. Mkuu wa Polisi (Kanda ya ziwa)
6. Mwanasheria wizara ya nishati na madini (Kanda ya ziwa/ndugu)
7. Katibu mkuu wizara ya fedha na mlipaji mkuu wa serikali (Kanda ya ziwa na mpwa wa rais).

Agenda hii inahitaji ukosefu wa akili kiwango cha kuwa "tabula rasa" ili kuipuuza.
Inaonekana kuwa na "essence" kubwa ndani yake.

Ni kwamba kanda zingine hakuna wasomi wa kushika nafasi za juu nchi hii??

#TOKOMEZA_UBAGUZI

Joseph Mohonia Politician
 
Lini na wapi?
Amejichotea yeye na mpwa wake mapesa kedekede kununua ndege na kujenga uwanja wa ndege Chato, bila idhini ya wananchi. Pia hakufuata procurement procedures za serikali. Sasa kwanini nisiamini anakula pesa za wananchi? Kaambiwa aweke mikataba ya ununuzi na huo ujenzi wazi, anarukaruka tu!
[HASHTAG]#magufuliisaphony[/HASHTAG]
 
Waafrika tulitawaliwa na wazungu kwa sababu ya ujinga wetu, sasa mumekuwa huru wa kufikiri na kutoa maoni yenye thamani, mnatoa za hovyo kabisa
Kwahiyo ulitaka nimsifu kwa nyimbo na kumwita shujaa huyuhuyu Lisu kwa kuropoka tususiwe harafu tukisha susiwa nitafaidika na nini iwapo yeye ataendelea kupokea posho zake kama kawaida!!!!?

Kama wewe unaona yuko sahihi endelea kumsifia huyo mwanaume mwenzio by the way kwanza namwona mnafiki mkubwa na kichaa flani si huyuhuyu pia aliwahi kushupaza misuri ya shingo miaka 8 kutuambia Lowasa fisadi!!!!? Leo vipi bado fisadi?
Siwezi kumwani tena Lisu abadani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye nae aanze kwa kususia Ruzuku na Posho za Ubunge zinazokusanywa na kugawiwa na Serikal ya Magufuli

Serikali ni ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ni ya watanzania wote sio mtu mmoja. Hayo mambo ya mtu mmoja yako chama chenu
 
K
Kama wewe unaona yuko sahihi endelea kumsifia huyo mwanaume mwenzio by the way kwanza namwona mnafiki mkubwa na kichaa flani si huyuhuyu pia aliwahi kushupaza misuri ya shingo miaka 8 kutuambia Lowasa fisadi!!!!? Leo vipi bado fisadi?

Siasa za Tanzania haziendi bila unafiki bibie! Magufuli huyuhuyu alizisifia safari za nje za Kikwete. Nakumbuka Magufuli alisimama Bungeni na kushupaza misuri kuzitetea safari hizo na kumwomba Kikwete asafiri zaidi ili ailetee nchi mapesa! Nafikiri sina haja ya kukuambia nini alisema baada ya kuwa Rais.

Pia CCM hawa hawa walishupaza misuri ya shingo kusema Lowassa siyo fisadi. Hadi Kikwete alikwenda kumfanyia kampeni ya Ubunge kule Monduli! Nape akaanzisha kampeni ya kuvua magamba, huku mwanzoni akisema Lowassa ni moja ya magamba hayo! Mwishowe wake unaufahamu.

Na mwisho, Magufuli anajipambanunua kama anapiga vita ufisadi! Sasa ni nini kinamzuia kumfungulia mashtaka fisadi Lowassa? Si hadi ilianzishwa Mahakama ya mafisadi? Mbona Mahakama inakosa wateja wakati kila kukicha Magufuli analalamika juu ya nchi hii kuliwa na kuchezewa sana (yeye mwenyewe alishiriki katika kuila na kuichezea); yaani analalamika kama mwananchi wa kawaida!!

Lowassa, Sumaye, Mkapa na Kikwete na viongozi waandamizi wengi waliopo na waliopita wa serikali ya CCM wanapaswa kuwa wamefikishwa Mahakama ya mafisadi!
 
Kama nchi haitaenda mbele kwa ajili ya majaji uchwara, basi wote wajiuzuru tuone.

Hapa hatishwi mtu.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Cheki hadi sasa serikali ili sema ajira elfu 52 zimeenda wapi zile au ndio kusema ilikuwa kiki si wasomi na Kayambo yetu tunatabikaa mtaani miaka ,2 Sasa huwezi ukaniambia huyu bwana anafaulu kafeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani huoni jinsi jamaa yako anavyoona ujiko kujiita rais wa TLS?

Kwa taarifa yako rais wa TLS ana maana kubwa kwani anachaguliwa na watu wanaojitambua na elimu zao. Wakati rais wa nchi hata akinunulia watu wali, wawe wanajua kusoma ama la kinaeleweka.
 
watanzania wapenda demokrasia wapo tayari kwa lolote ambalo litamfanya magufuli na mshauri wake mkuu yaani Maliyamungu Bashite waache Udikteta wao, kwani lengo la chadema ni kurejesha ubinadamu Tanzania ambao magufuli kaanza kuupoteza kwa Udikteta wake, ebu nyinyi CCM mkatazeni boss wenu aache ubabe, uonevu, kuwakomoa, kuwabambikia watu kesi kesi muone kama Wapinzani watahangaika na kumshitaki kwa wazungu.
Sio watanzania wote kwasababu kati ya wengi mimi ni mmojawapo tupo pamoja na mheshimiwa rais sio uyu mropokaji mkuu.

Kauli ya kupaza sauti nchi isusiwe misaada,unahisi yupo sawa na anamkomoa nani? Fikira zake anamkomoa mheshimiwa rais kumbe watakaoteseka wananchi wakiwemo ata wale waliomchagua yeye kule kwao Singida.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa majeshi enzi hizo alitoka wapi? Gavana wa Benki Kuu alitoka wapi? Waziri mkuu alitoka wapi? Na wengine wengi ambao unawajua. Huyo Nyerere alivyosema, na kama hamkumuelewa ni kwamba katika kutoa ajira dini au kabila sio, na wala havitakiwi kuwa kigezo cha mtu kuajiliwa au kutoajiliwa.
Hoja yangu! Wamejazana hawakujazana ni wapi katiba/sheria inapokataza mpaka muwe na hoja ya kwenda kushitaki huko mnakotaka kwenda?
Kinachatakiwa katika ajira za serikali ni "Qualifications" bila kujali ni mtoto wa kigogo au mlalahoi, wa dini gani, wala wa kabila gani. Wanaoanza kudodosa aliyopo kwenye position fulani ni kabila gani au dini gani badala ya kudodosa aliyopo kwenye position hiyo anaqualify au la huyo ndie anayetaka kuleta ukabila ktk hili. Hata hivyo nasubiri kwa hamu kuona mataifa yakitususa kwa kufunga balozi zao taifa moja baada ya jingine kutokana na hizo hoja za Tundu.
Katika teuzi za kisiasa, Rais amepewa mamlaka ya kuteua timu yake ambayo anaona itamfikishia malengo yake. Kama vile kocha wa timu ya mpira, masalan ya Taifa akishateuliwa ndie mwenye jukumu la kuteua na kutangaza wachezaji wa timu hiyo na falsafa ya uchezaji gani wa ushindi anaoutaka na anaouamini yeye (sio sisi), na mara nyingi huwa tunashauri kocha asingiliwe. Sasa kwa Rais kwa nini hatutaki kuheshemu na kumuacha achague timu ambayo anaona itamtimizia falsafa zake. Unapoona kuwa mchezaji fulani hakustaili kuteuliwa badala yake angechaguliwa fulani, unatofauti gani na huyo kocha mteule? Kumbe na wewe si una timu yako ambayo ungeitangaza kama nawe ungekuwa kocha mteule?


Post sent using JamiiForums mobile app
Wafia wa Katundu kalissu awatakuelewa mkuu, yeye mwenyewe kasahau alivyomsajiri marehemu dada yake ubunge wa viti maalum pale Chadema. Au anajua watanzania wasahulifu?

Uyu ana moral na ujasiri wa kusema ukabila na ukanda wakati chama chake ndio magwiji ya haya mambo, angeanza kukisafisha chama chake kwanza ndio angeeleweka. Ama kweli nyani haoni kundule.

Mwisho naomba kumuuliza Katundu kalissu kama kajisahulisha ili Lucy Awenya ni mtoto wa marehemu mzee Ndesamburo, Mukya ni Hawara wa mwenyekiti wake,Komu na Yule mama Komu na Salim Mwalimu ni ndugu anabisha? Kubenea kaingiza usajiri wake, na Ally Bananga diwani sombetini mkewe yupo viti maalum pale mjengoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom