Tundu Lissu ashinda kesi ya kupinga ubunge wake

Ha ha ha ha mkuu. Mbona umenichekesha hivi? But lakini we una tudola na tutanzania shillingi ili majambazi wakikuvamia angalao upate cha kuwapa? Jamaa alikuwa na hela sawa na mshahara wa mwaka kwa ofisa msomi wa serikali, yeye ilikuwa ni tuchenji twa kununulia kala kakitu katamu kalikoshikwa pabaya kama alinyojisemea mzee ruksa. Lakini hivi huhu jamaa ni mzima wa afya? Mke wake alishatangulia?
:yo:Mkuu huwa mnapata wapi haya maneno? Yani nimecheka mpaka basi, i reserve my comments :rockon:
 
Glory be to GOD!
Hongera sana Hon. Lissu, wanachama & wapenzi wa CDM, wananchi wote wa JMT! Siipi Mahakama hongera kwani wamefanya bali nampa Jaji hongera, kwa vile wenzake wengi tu wameiharibu mahakama kwa uchafu wa rushwa na dhuluma.

Mwisho asanteni sana JF mods.
 
Hongera Kamanda Lissu kwa ushindi Sasa kawatumikie wananchi wa jimbo lako na Tz kwaujumla, Hongera Sana Kamanda.
 
hapa me naona la mcng uongoz wa chadema kuzid kuongeza uimara kwenye chama coz kwa jnc inavyoonejana ccm kupitia nguv ya uma xo wanajrb kutaf njia nyngne ili hali wazd kuwa madarakani xo umajk.a wameshndwa k
 
Lissu kashinda, mpendazoe atashinda pia
huwezi kufananisha credibility ya Lissu na Lema!!! lisu hatukani,
 
Ingekuwa kweli, watu wangejua kuwa si kwamba tu haki inatendeka bali inaonekana kutendeka. Huu ndio msingi wa haki hata kama ikitendeka lakini watu wakahisi kuwa haitendeki kuna dosari kubwa. Kujazwa kwa jeshi la polisi siku ya hukumu ya Lisu kumelenga kuwapumbaza watu (kama wewe) kutokana na makosa yaliyofanywa kwenye hukumu ya Lema. Nia ni kuonyesha kwamba ni jambo la kawaida au desturi ya polisi jambo ambalo mimi na wewe tunajua si kweli. Ziko kesi zilizokuwa na msisimko mkubwa nchini na hazijawahi kuwa na ulinzi (usio shirikishi) kama huo. Wamelazimika kurudia waliyofanya Arusha (kwa gharama kubwa ya walipa kodi) ili tu kujaribu kujiosha (kwa maji taka). Wapo ambao wataamini lakini si kweli, hiki ni kiini macho, ni uhuni tu!
Kuhusu mahakama kufanya haki hili si suala la jumla, kila kesi inabidi kuchukuliwa kwa kadri inavyohukumiwa. Kwa ujumla msingi wa kutenda haki kwa mahakama ni imani ambayo jamii inakuwa nayo juu ya mahakama na hukumu zake. Kwa bahati mbaya kwa kipindi kirefu sasa jamii yetu imekosa imani na mahakama. Kila kona kuna malalamiko kuhusu hukumu za dhuluma zinazofanywa na mahakama. Kama nilivyowahi kueleza, waswahili husema "Baniani mbaya kiatu chake ni dawa", lakini kiatu cha baniani mbaya hakimgeuzi awe baniani mzuri japo ni dawa. Halikadhalika, "Kafiri akufaae si islam asiyekufaa". Pamoja na kukufaa kafiri anabaki kuwa kafiri wala si islam. Mahakama ya Tanzania ni baniani mbaya (hata kama kiatu chake ni dawa kwa kesi ya Lisu) na inabaki kuwa kafiri japo imefaa (pengine kuliko islam) katika kesi ya Lisu.
 
Katika siku za furaha kwangu,hii ni mojawapo,niliomba kwa uchungu sana haki itendeke na Lissu arejee bungeni.Tunashukuru kwa ushindi,Bunge litaendelea kuwa moto kama kawaida.Mkuu Isango ubarikiwe sana kwa taarifa za kitalaamu kabisa.Nashauri Chadema wamtumie huyu jamaa kwenye records,anafuatilia kwa makini sana
Bravo Lissu.Tv ya magamba imeonyesha still picture za kesi ya Lissu,aibu yao!
 
Tukumbuke na usemi wa Mbowe pale Arusha, tatizo sio mahakama bali tatizo ni hawa majaji wetu
 
Sikutaka kabisa kusoma JF jana kwa kuhofia dhulma za Arusha zingejirudia Singida Mashariki. What a relief that Tindu Lissu anarudi mjengoni kwenye vikao vya bajeti? Celina Kombani jiandae!
 
Tukumbuke na usemi wa Mbowe pale Arusha, tatizo sio mahakama bali tatizo ni hawa majaji wetu

Jaji mwenywe amekiri:
"Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia bila kutoa vielelezo dhahiri vinavyoonyesha tukio husika.

Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema
ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.

Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika."


Chanzo: Mwananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom