Tundu Lissu ashinda kesi ya kupinga ubunge wake

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Tumeshafika mahakamani, wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida, na waandishi wa habari wapo wengi sana katika eneo la mahakama.

Polisi ni wengi sana, ndani na nje ya mahakama. Kilicho cha ajabu kidogo leo getini maofisa wote wakubwa wa jeshi la polisi wapo pale na kikosi maalumu kwa ajili ya kumkagua kila anayeingia mahakamani, tunapekuliwa hasa, hadi wabunge wanaoingia.

Kuna baadhi walikatazwa kuingiza magari yao mahakamani lakini baada ya vuta nikuvute, magari yapo mahakamani, na watu wamtinga ndani tunasubiri yatakayojiri.......... tutawajuza, leo kamanda nipo gado, Mungu amenijalia afya.

UPDATES:

Jaji amemaliza: LISSU AMESHINDA, MUNGU AWABARIKI MLIONIOMBEA NIWAFIKISHIE HAYA

HOJA YA TISA, Kama Mgombea wa walalamikaji (CCM) alikataa kusaini matokeo. Hoja hii haipaswi kunipotezea mud asana. Njau hakuhudhuria, aliwakilishwa na mlalamikaji wa kwanza ambaye alikataa kusaini matokeo. Wakili wa serikali alisema, kukataa pekee kusaini matokeo hakusaidii kutengua matokeo. Hivyo hata hoja ya tisa naitupilia mbali. Haikuwa sahihi.

Hoja ilitolewa hapa, kuwa mawakala walikula kiapo kwa hakimu. Walalamikaji walisema kuwa walipaswa kula kiapo kwa msimamizi wa uchaguzi. Je kuapishwa na hakimu kunabatilisha matokeo? Hoja zilizotolewa na mawakili wa serikali walisema Hakimu ana mamlaka ya kutoa viapo. Binafsi nasema kuwa waliotunga sheria hawakumaanisha kuwa Mahakimu hawaruhusiwi kuapisha mawakala, vinginevyo kungekuwepo fomu ya hakimu tu. Lakini fomu zinaonyesha hakimu, Msimamizi wa uchaguzi na Msimamizi msaidizi, fomu inatambulika kisheria, kwa sheria ya Uchaguzi. Hii haihusiani na zoezi la uchaguzi. Katika kesi ya Prince bagenda Vs Wilson masilingi, katika kesi hii mawakala walifanya kazi bila kuapishwa, na ilichukuliwa kuwa sehemu ya kutengua uchaguzi, angalia pg 240. Kwa lugha yake jaji alisema hawakuwa na mamlaka halali, lawful mandate, lakini ilisaidia kutengua, na mwanasheria wa serikali alihusika katika hili. Maelezo hayo yanatofautiana na kesi iliyo mbele yangu, jimbo la Singida mashariki mawakala walikula kiapo, na walikuwa na mamlaka halali. Hivyo hoja hii naitupilia mbali

HOJA YA KUMI, Hoja zote hazikutbithitishwa, HIVYO, UCHAGUZI ULIKUWA WA HAKI, NA TUNDU LISSU NI MBUNGE HALALI NA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA WA HAKI, HIVYO SIWEZI KUTENGUA.

Hoja ZOTE zimetupiliwa mbali, hukumu inasomwa sasa...
Isango said:
Leo ni siku ya hukumu, ni kesi ya uchaguzi, inatokana na uchaguzi uliofanyika tarehe 31/10/2010, waombaji ni Shabani selema, na Paskali Halu. Walileta mashahidi 24, na vielelezo saba, wanawakilishwa na Wasonga. Kimsingi wanapinga uteuzi wa Lissu kuwa mbunge wa Jimbo la Singida mashariki, wakidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi. Wakidai kuwa kulikuwa na dosari zilizofanya uchaguzi usiwe huru na haki, hivyo kumfanya Mgombea wao wa CCM asishinde.

Walalamikiwa, mlalamikiwa wa kwanza walisema kuwa yeye hakuwemo, au hakuwa mshirika wa tuhuma zilizofanywa. Walalamikiwa wote pamoja wanasema hakuna kitu cha msingi kinachoweza kuifanya mahakama itengue matokeo.

Haibishaniwi kuwa mgombea alishinda kupitia CHADEMA, kupitia jimbo la singida mashariki, na kumshinda mgombea wa CCM Bw. Njau ambaye alipata nafasi ya pili. Tofauti ya Kura kati ya Lissu na Njau ilikuwa kura 1626.

Mlalamikiwa wa pili, anaunganishwa katika kesi kama necessary paty, kwa kuwa mlalamikiwa wa pili ni Msimamizi wa uchaguzi.

Hoja katika kesi zilikuwa 11.
Bado inafafanuliwa hoja ya sita na inaelekea kutupwa
Hoja ya tano nayo imetupwa, pamoja sana
Hoja 4 nayo imetupwa, maombi yazidishwe kila mtu kwa imani yake
Pamoja na kuchelewa sana, sasa jaji Moses Mzuna, ndo anatinga mahakamani, nitaendelea kuwajuza, ila naomba watu ambao hawapo mahakamani waache kutuma threads zingine zinawachanganya wasomaji.

Ving'ora vya jeshi la polisi vinalia nje, vitisho kila kona utadhani kuna msafara wa Rais wa Marekani humu
 
Ni matumaini yangu kwamba leo ndiyo siku ya hukumu.

Jamani wale mliopo Singida tunaomba mtupe updates.
 
asante sana kaka......tuko pamoja..

juu ya hukumu hiyo kuna fitina kubwa sana ila nasubiri jaji ahukumu...
 
Tumeshafika mahakamani, wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida, na waandishi wa habari wapo wengi sana katika eneo la mahakama. Polisi ni wengi sana, ndani na nje ya mahakama. Kilicho cha ajabu kidogo leo getini maofisa wote wakubwa wa jeshi la polisi wapo pale na kikosi maalumu kwa ajili ya kumkagua kila anayeingia mahakamani, tunapekuliwa hasa, hadi wabunge wanaoingia. Kuna baadhi walikatazwa kuingiza magari yao mahakamani lakini baada ya vuta nikuvute, magari yapo mahakamani, na watu wamtinga ndani tunasubiri yatakayojiri.......... tutawajuza, leo kamanda nipo gado, Mungu amenijalia afya.
sawa kamanda...tunafuatilia kupitia kwako...wewe ndiyo jicho letu huko kwa kamanda wetu Lissu...keep us informed everytime dude!
 
isango kama una skype sema ili tufanye utaratibu wana jf wawe wanasikiliza live toka huko...
 
ukiona hovyo ujue matokeo wanayajua, hii ni kama ilivyokuwa wakati wa lema. wanajua matokeo ya kumvua ubunge Mh. Lissu yataamsha hasira za wananchi ndo maana wameandaa mabomu ya kuwapiga. Nchi hii !!!!!! kweli kazi ipo.
 
Namshauri akate rufaa kwa sababu kuja kusikilizwa tena mwaka 2014. Wanatakiwa aendelee kututumikia watanzania nchi nzima tunamuhitaji.
 
Eee Mungu ingilia kati huu mkakati wa magamba kubaka Demokrasia unatisha. Taarifa zinazovuma sasa za kutumia mahakama kuwavua ubunge baadhi ya wabunge machachari wa upinzani ni mbaya na zinatia hasira na ghadhabu. Kuna kila sababu ya kusubiri kitakachojiri.

Lakini kama itakuwa kama yale ya Lema ni lazima uongozi wa CDM uchukue hatua.Huu mkakati hautakoma, unaweza kuhamia kwa Sugu na kwa wabunge wengine. Kumbukeni kila mbunge wa CDM matokeo yake ya uchaguzi yamepingwa mahakamani na magamba na ulikuwa ni wito wa Mzee Makamba,
 
Kinachotuangusha watanzania ni UOGA na UBINAFSI.... Kwa mtindo huu hakuna haja ya kuwa nchi ya kidemokrasia, manake watawala wameshindwa hilo. Huu ni sawa na udikteta kutoa chaguo la wananchi kwa maslahi binafsi ya kikundi cha watu wachache. Afadhali wangekua madikteta kwa maslahi ya wananchi walio wengi, lakni wao wanakua madikteta kwa maslahi yao binafsi ili pale watakapokua wakila kusiwe na mtu jasiri wa kuwapigia kelele... Ifike mahala tuseme BASI kwa huu ukandamizaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom