beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo amekutana na Waandishi wa habari kuzungumzia hali ya ya kampeni zake ilivyo mpaka sasa na kile kinachoendelea kuelekea Uchaguzi Mkuu mnamo tarehe 28/10/ 2020. katika Mkutano huo ambao waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walihudhuria, Tundu Lissu ametolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali.
Aidha, akianza kutoa tathmni ya kile kinachoendelea katika kampeni zao Tundu Lissu alisema "Kwa ujumla tumefanya kazi kubwa sana na nyie ambao mpo kwenye msafara huu mmeona na Watanzania wameona. Tumefanya mikutano mingi kuliko mikutano yote aliyofanya mpinzani wetu Mkuu Rais Magufuli pamoja, Makamu wake pamoja na Waziri Mkuu kwa combined. Yaani mikutano ambayo tumeifanya sisi ni mingi kuliko ambayo wameifanya wao kwa ujumla wao.
Mikutano yetu imekuwa na mafanikio makubwa sana kuliko ambavyo sisi wenyewe tulitegemea mwanzoni, hakuna mkutano ambao imebidi tusafirishe mtu yeyote. Mikutano yetu imehudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya Watanzania ambao wametembea wao kwa miguu yao, wamekuja kwa vyombo vyao wamekuja kwa namna mbalimbali za usafiri kwa kujitegemea. Mikutano yote ya Chama cha Mapinduzi watu wanakwenda kwa kulazimishwa, wanapeleka watoto wa shule baada ya kuwalazimisha kwa kufunga shule, kutisha waalimu, wanafunga Maofisi ya serikali na kulazimisha wafanyakazi kwenda kumsikiliza Magufuli.
Wataalamu wetu wa mahesabu na watu ambao wanafuatilia wanafanya survey za muelekeo wa Upigaji kura wanatuambia kwamba kwa jinsi ambavyo mikutano yetu imekwenda ya kampeni, kwa jinsi ambavyo tumefanya mikutano yaetu tunashinda uchaguzi huu kwa asilimika kati ya 65 hadi 75 huo ni mtazamo wa watua ambao tumewaopa kazi wa kufanya survey ya Wapiga kura nchi nzima.
Hali yetu ni nzuri sana. Kwahiyo, Magufuli nje ya Tume ya Uchaguzi, nje ya wasimamizi wa Uchaguzi aliowateua. Makada wa CCM ndio Wakurugenzi na Wasimamizi wa Uchaguzi, nje ya kufanya vurugu, nje ya kuiba kura hawezi akashinda uchaguzi huu kwa sababu hana kibali cha Watanzania tena. Kwahiyo kwa sababu hana kibali cha Watanzania na kampeni yake inadoda kila mahali tunaona sasa vitendo ambavyo tulivitabiri mwanzoni. Tulisema kwamba hawa watu hawawezi wakashinda Uchaguzi ulio huru na haki na tayari tunaanza kuona dalili hizi aidha kuharibu uchaguzi, au kufanya wizi mkubwa wakitumaini kwamba labda pengine atabaki madarakani.
Daftari la Wapiga kura limetolewa siku chache zilizopita kwa kuangalia haraka haraka wachunguzi wetu wanalifanyia uchunguzi wa kina nataarifa zitatoka kabla ya jumatatu hopefully. Lakini kwa kuangalia tu maeneo machache inaelekea kuna mamilioni ya Wapiga kura hewa ambao wameingizwa katika daftari la kudumu la Wapiga Kura, inaelekea kuna vitu hewa vya kupigia na kuhesabia kura kwa maelfu, wataalamu wetu wanalifanyia kazi na wanaendelea kulifanyia kazi tangu lilipotoka, taarifa ya kina itatolewa si muda mrefu lakini ushahidi wa mwanzo unaonesha kwamba wameandika majina ya watu wasiokuwepo, wameandika majina ya watoto wadogo wa shule na tumeona baadhi yao wakifundishwa namna ya kupiga kura na Hazani Zungu. Kwahiyo, wameandikisha wapiga kura wasioukuwa na sifa na wapiga kura wasiokuwepo kwa mamilioni na vituo hewa.
Sasa hii ni wazi kuwa wanafikiria wanaweza kuuiba uchaguzi ambao hawana uwezo tena wa kuushinda wanataka kufanya hivyo. La pili, ni kutumia vitendo vya kihalifu kama kubadilisha matokeo mahali ambapo wameshindwa, kutangaza wagombea wao kwa nguvu watu wetu wametuambia kuwa wanachoweza kufanya kingine ni hicho.
Vitendo vya tatu ambavyo tumeona vimekuwa vikiongezeka sana ni matumizi ya vyombo vya dola, taasisi za kiserikali kw waziwazi ambao wamekuwa na nia ya kuipitisha CCM au kuhakikisha uwezo wetu wa kufanya kampeni unapunguzwa au tunazuiliwa kabisa kufanya kampeni. Vitendo vilivyotokea jana ni mfano halisi wa vitendo hivyo. Jana ilikuwa tufanye mikutano kumi na kila mahali katika sehemu hizo kumi maelfu kwa maelefu wamekusanywa. Lakini asubuhi wakati tunaondoka uwanja wa ndege kuanza safari yetu pilot wa ndege yetu akaambiwa hawezi akatua Nachingwea, hawezi akatua Nanyumbu akaambiwa kuna kimbunga huko hali ya hewa sio nzuri. Kwahiyo, ili kumwepusha Mgombea Urais na madhara yanayoweza kuhatarisha usalama wake ni marufuku kutua Nachingwea na Nanyumbu baadae wakaongeza vituo vingine ambavyo hatuwezi kutua.
Tulipoanza safari kuelekea Mikutanoni baadae tukaambiwa Polisi wamepiga mabomu Kibiti na Rufiji ikiwa ni pamoja na kuwatawanya watu ikiwa pamoja na kuwanyang'anya vyombo vya matangazo. Kwahiyo, watu ambao tulikuwa tukazungumze nao wamepigwa na Mapolisi na Wanajeshi kwa namna ambayo clearly walikuwa hawataki tukazungumze na watu wa maeneo hayo. Kwa sababu tulipata habari kuwa mikutano imevunjwa kwa namna hiyo tukasema twende ambako mikutano haijavunjwa.
Hivyo, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'
Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"
Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo.