Tundu Lissu ahojiwa kwa kumwita Rais Magufuli "Mtakatifu". Aachiwa...

Hivi Think tank ya polisi ni nani ? Yaani yule anayewaelekeza polisi kwamba huyu akamatwe kwa kuwa kafanya hivi au vile , ni nani hasa ?
 
TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameachiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Mapema leo asubuhi Lissu alikamatwa na kupelekwa kituoni hapo ambapo ilielezwa kuwa alichukuliwa kwa lengo la kuhojiwa kuhusiana na mkutano aliofanya na waandishi wa habari kuhusu wa kupotea kwa Bernard Saanane.

Ben Saanane alikuwa Msaidizi wa Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa – alipotea ghafla takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo huku Lissu akiitisha mkutano na wanahabari tarehe 14 Desemba, 2016 na kuitaka serikali ieleza kama inamshikilia kijana huo au la.

Fredrick Kihweru mmoja kati ya wanasheria wa Chadema akitoa maelezo baada ya mahojiano ya polisi na Lissu kumalizika amesema, “aliitwa kuhojiwa juu ya Press conference aliyofanya na kuzungumzia suala la Saanane lakini pia wamemuhoji anamaanisha nini kumwita Rais John Magufuli jina la “Mtukufu.”

Itakumbukwa kuwa Lissu amekuwa akimtaja Rais Magufuli kama “mtukufu” mara kadhaa tangu aliposhitakiwa kwa kutamka kuwa “Dikteta uchwara anapaswa kupingwa kwa nguvu zote” kesi ambayo bado inaendelea mahakamani.

Wakili Kihweru amesema Lissu amehojiwa pia kuhusu hatua yake ya kuitaka Serikali iseme kama haimshikilii Ben Saanane na pia ieleze juu ya mawasiliano yake ya mwisho ya Ben alifanya na nani, wapi na waliwasiliana nini.

Baada ya mahojiano hayo Lissu ameachiwa kwa dhamana na anaweza kuitwa wakati mwingine atakapohitajika.
 
nimesoma ulicho kiandika hakika na wewe umeandika kichadema ....
Lissu na Mbowe wanajua Ben alipo
 
Nadhani salutation ya mtukufu siyo kosa la jinai
 
Iteni majina yote lakini ikulu hamgusi milele.....2020 ni kuchinjwa tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…