Tundu Lissu ahojiwa kwa kumwita Rais Magufuli "Mtakatifu". Aachiwa...

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,456
2,000
Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameachiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam na pia polisi mkoa wa kipolisi Ilala.

Amehojiwa ni kwanini anamwita Mheshimiwa kuwa ni Mtakatifu.

Amehoji akiita "lile jina" ambalo limemfanya awe na kesi kadhaa mahakama ya Kisutu ni shida. Je, na hili la Mtakatifu ni shida?

Amehojiwa aeleze maana ya Mtakatifu akaeleza ni asiye na hatia mbele ya Mungu na wanadamu.

Amehojiwa pia kuhusu kikosi kazi kinachotesa watuhumiwa wanaokuwa chini ya polisi lakini huchukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha mateso na kurejeshwa alfajiri Central.

Amewaambia yeye ameongea na walioteswa na kuna wapo walio tayari kutoa ushahidi kuhusu ukatili wa kikosi kazi hicho.

RCO wa Ilala amekana na kusema kuwa watuhumiwa huwa hawateswi.

Lissu pia amehojiwa kuhusu sakata la kupotea Ben Saanane na polisi wanavyoweza kumtafuta amewaambia watafute mawasiliano yake ya mwisho waseme Saanane yuko wapi.

Lissu amekuwa polisi akiwa na Wakili Fred Kihwelo tangu saa nne hadi saa kumi na nusu.

Polisi wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu maelezo hayo.

Anaandika Lissu.

Waheshimiwa nawasalimu kwa heshima zote. Muda mfupi uliopita nimetoka Kituo Kikùu cha Polisi, Central, Dar, nilikokuwa tangu asubuhi. Niliitwa kuhojiwa juu ya mambo mawili: kauli nilizotoa wakati wa press conference ya wiki iliyopita kwamba watu wanaomkosoa Mtakatifu Rais wetu mitandaoni wamekuwa wakikamatwa, kushikiliwa kwa muda mrefu bila kufikishwa kortini na kuteswa na kikosi kazi maalum kinacho-operate kutoka kwenye nyumba moja iliyoko Mikocheni, Dar.

Polisi wanadai kauli hizo ni za kichochezi. Aidha wanadai kumwita Magufuli Mtakatifu Rais ni uchochezi mwingine. Sababu ya pili ya kuitwa Central ni kutoa taarifa za kusaidia polisi katika upelelezi wao kuhusu kupotea kwa Ben Saanane.

Kuhusu uchochezi, nimewaeleza polisi kwamba ni kweli kuna kikundi maalum ambacho kinatesa watu wanaotuhumiwa kwa tuhuma za makosa ya mtandaoni na makosa ya ugaidi na ujangili.

Ushahidi ni mkubwa sana juu ya suala hili. Walioteswa wapo na ndio waliotueleza mambo mabaya waliyofanyiwa. Wengine niliwakuta mimi mwenyewe nilipokamatwa Juni mwaka huu na kulala Central wakati wa Uchochezi One.

Kuhusu Mtakatifu Rais, nimewakumbusha kwamba nilipomwita Dikteta Uchwara walinikamata. Sasa nimemwita Mtakatifu Rais nayo shida, inakuwaje?

Na by the way, tangu kesi ya Dikteta Uchwara One ilipoanza, mashahidi wao wameshindwa hata kuieleza Mahakama maana ya maneno 'Dikteta Uchwara.' In short, hakuna uchochezi wowote ambao nimefanya. Ni mbinu zao tu za kutaka kutufunga midomo ili tusimseme huyu Mtakatifu wao anayedhani kinachotokwa kinywani mwake ndio sheria ya nchi.

Kuhusu Ben Saanane, nimewaambia timu ya wapelelezi (hawa wako tofauti na walionihoji kuhusu uchochezi) kwamba kuna kila sababu ya kuamini kwamba kupotea kwa Ben Saanane kuna uhusiano na wale waliomtumia message kwamba 'his days are numbered' kwa kuendelea kwake kuhoji uhalali wa PhD ya Magufuli. Katika mazingira ya sasa ya kisiasa ambapo kila anayemsema Magufuli vibaya anakamatwa na kuteswa haiwezi kuwa ajabu kwamba Ben Saanane amepotea katika mazingira ya utata namna hii.

Kitu muhimu hapa ni 'motive', nani atakuwa na sababu ya kumpoteza Ben Saanane. Walionihoji walikuwa 'very polite', lakini kilicho muhimu zaidi ni kwamba tuendelee kupaza sauti zetu serikali hii ituambie Ben yuko wapi. Hadi sasa hawajasema kama wamemkamata na/au wanamshikilia.

Hawajasema kama ametoka nje ya nchi hii au la, na wao ndio wanaodhibiti exit points zote. Hawajasema mawasiliano yake ya mwisho yalikuwa lini, na nani, wapi na yalikuwa yanahusu nini. Wao ndio wana technical capabilities za kutuambia majibu ya maswali haya.

Tuendelee kupiga kelele ili watoe actionable information kwa umma kuhusu Ben Saanane. Baada ya kuchukua maelezo kwa karibu masaa sita wameniachia kwa dhamana na wameahidi kuniita watakaponihitaji muda wowote.

Niwatakieni Merry Christmas and Happy New Year 2017.
Tundu
 

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,549
2,000
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana polisi muda huu baada ya kumshikilia kwa saa kadhaa leo.

Alikuwa ameshikiliwa kwa mahojiano juu ya Press Conference aliyofanya na kuitaka serikali ieleze alipo Ben Saanane na pia kuhusu watu saba waliookotwa Mto Ruvu na kuzikwa bila uchunguzi.

Walimhoji pia kuhusu uwepo wa Makambi ya Mateso ambayo aliyatamka siku ya Press Conference.

Aidha RCO ilala amechukua maelezo yake kuhusu Ben kwa hoja kuwa Polisi Ilala wamefungua rasmi jalada la Uchunguzi kuhusu
Ben Saanane

Ameachiwa kwa dhamana ya Polisi kwa kuwekewa udhamini na mtu mmoja.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
17,510
2,000
Napenda kweli maswali kati ya mtetezi na mlalamikaji yanavyokua katika kesi za Lisu (hua nacheka na kutabasamu).

Mtu anakaaga kimya kwa kufanywa ajione mjinga kusimama kizimbani kulalamika.
I hope na hii itafika huko, hizi episodes ziendelee.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,920
2,000
Kwa kweli nchi yetu sasa inapitia kipindi kigumu sana.

Huyo Bwana akiitwa lile jina lingine imekuwa ni shida hadi watu wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka....

Sasa kumbe hata ukinwita hili jina la heshima kubwa la Mtakatifu nalo kumbe ni shida hadi unakanatwa na Polisi na kupelekwa kituoni kuhojiwa!

Duh.... Sasa wananchi tunakuwa tumechanganyikiwa tusijue tumwite jina gani Bwana yule?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom