Tundu Lissu ahoji sababu za Mwenyekiti Mbowe kutokuwepo kwenye mapokezi uwanja wa ndege

..mapokezi yake hayakuwa na masuala ya kiitifaki.

..mbali ya kuwa viongozi wa chama Mbowe na Lissu ni marafiki.

..kwa hiyo Lissu alikuwa akimuulizia rafiki yake aliyekuwa na shauku ya kukutana naye uwanja wa ndege.

..hakuwa akimuulizia Mbowe kama mwenyekiti wa chama.
Sure
 
Kiukweli sijui ni lini Lissu will grow into a mature politician?

Hilo ni la kuhoji in public, anadhani ananyenyekewa na wote?

P
Ndio maana Kuna Uzi humu nilishaandika kuwa Katu na kamwe Lisu hawezi akawa Rais wa nchi hii hata Kama angezaliwa kabla ya kupata uhuru,Sasa haraka yake ilikuwa ya Nini, au amekuja kwa ajili ya Mbowe. Hapo inaonyesha kuna migogoro Kama nilivyoandika humu,maana inaonyesha katika ujio wake kulikuwa na mfarakano na Mbowe ambapo Hadi Mbowe akasema hatakuwepo uwanjani lakini inaonyesha viongozi wengine wakafanya mazungumzo ya kuzuga na hao wajumbe wengine wa kamati kuu na kumwambia tayari tumeshaongea na Mwenyekiti na kuyamaliza na atakuwepo uwanjani kukupokea,Ndio sababu Lisu kwa uchanga wake wa Subira na kutokuwa na Subira Wala uvumilivu Wala stamini ya kifua chake akaropoka hayo aliyoropoka kusema kuwa mbona mlisema atakuwepo hapa Mwenyekiti kunipokea?
 
Tulisema Ila wanachadema wenye mihemko wakaishia kututukana. Na wengine wakasema protocal hairuhusu.

Gazeti la mwananchi limemnukuu Lissu akihoji alipo Mbowe, Lissu amehoji sababu za Mbowe Kutokuwepo.

Sasa ni rasmi ule mnyukano, makundi na mgawanyiko upo hadharani.

Kazi ndjo imeanza.

----

Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara) Tundu Lissu ametua nchini, akitokea Ubelgiji alikokimbilia baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 huku akimuulizia aliko Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alitajwa kuwepo kwenye orodha ya kumpokea katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Lissu amewasili leo Jumatano, Januari 25, 2023 na kupokewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika aliyeongoza na viongozi wa Kamati Kuu waliokwenda kumpokea uwanjani hapo.

Mara baada ya kutoka nje ya geti la kuwapokea wageni uwanjani hapo, Lissu alionekana kuwa mwenye furaha alisalimiana na viongozi kwa kuwashika mikono ghafla akauliza, " Mwenyekiti (Mbowe)yupo wapi? Si mliniambia atakuwepo? Eeeeh.

Hata hivyo, Mnyika alionekana kutabasamu huku baadhi ya viongozi walisikika wakimwambia kwamba atakutana naye Temeke viwanja vya Bulyaga katika mkutano wa hadhara alioandaliwa na chama hicho.

Lissu aliondoka nchini kwa mara ya kwanza Septemba 7, 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana jijini Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge.

Lissu alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma alipopatiwa matibabu ya awali na baadae kukimbiza jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

Januari 6,2018 alihamishiwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi hadi Julai 27, 2020 aliporejea nchini na kuwania urais lakini alishindwa na mgombea wa CCM, John Magufuli.

Hata hivyo Novemba 10, 2020, baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, Lissu aliondoka nchini kwenda Ubelgiji kwa madai ya kutishiwa usalama wake.

Chanzo: Mwananchi
Nyie jamaa bana.. hivi mbona bado mko local sana..
Hivi mnafikiri watanzania wa sasa wako bado na maujingaujinga ya cheap politics..

CHADEMA lazima mbadilike.
 
Kiukweli sijui ni lini Lissu will grow into a mature politician?

Hilo ni la kuhoji in public, anadhani ananyenyekewa na wote?

P
Usimlaumu Lisu mkuu, inawezekana ashaanza kuunganisha doti kuhusu kushambuliwa kwake.

Ngoja tuone mwisho wa lawama zake kwa mwenyekiti wake.

RIP Chacha Wangwe.
 
Kiukweli sijui ni lini Lissu will grow into a mature politician?

Hilo ni la kuhoji in public, anadhani ananyenyekewa na wote?

P
Boss sasa ni wazi bado unachuki ya waziwazi kwa Lisu. Hebu ieleze umma wa JF ni nini hasa alikukosea?! Kama ni ubunge na wewe pia ulijaribu kugombea kupitia Kawe na ukafanikiwa kupata kura 1, kama ni uwakili na wewe ni wakili ingawa hujawahi kuonekana Mahakamani ukitetea hata mshitakiwa wa uwizi wa kuku mtaani. Tatizo lako ni nini hasa against TAL?
 
Back
Top Bottom