Lisu alijibu kutokana na swali mtangazaji alilomuuliza..yuko sahihi
ASSET na LIABILITY
Warning: UKAWA sio business entity, kafanyeni biashara zenu huko! UKAWA ni mabadiliko period!
ASSET na LIABILITY
Warning: UKAWA sio business entity, kafanyeni biashara zenu huko! UKAWA ni mabadiliko period!
binafsi Lissu kanisikitisha sana, siamini huu kama ndo uwezo wake kwa sasa, yaani anasema Dr anasema mshenga hasemi mposaji, kama Dr ndo alikuwa mposaji sasa si kisha goma hataki tena kuposa, sasa vipi chama kiendelee na mikakati? mtu akigoma haoi tena humlazimishi, badala yake chama kikaendelea tu kuoa, hapo si kweli kuwa tayari walishapanga?
Baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa kuzungumza na Wanahabari jana. Wakili Msomi ndugu Tundu Lissu aliibukia Voice of America Idhaa ya Kiswahili akijibu Hoja za Slaa kwa style ile ile iliyozoeleka na Chama chake ya KUCHAFUANA.
Wengi mnajua alichoongea hasa hasa akimuingiza mchumba wa Dr. Slaa kuwa anahusika na move aliyoifanya Dr jana. Ninaamini kuwa kwa Chama makini kama CHADEMA walipaswa kuzipangua hoja za Slaa kuliko walivyomtuma Lisu kuongezea hoja juu ya hoja na kuibua interest za wadadisi kujua uadilifu wao.
Katika suala la Josephine kuhusishwa imefikia hata kumdhalilisha Dokta kwa kusema alitupiwa virago vyake nje akalazimika kulala ndani ya gari. Ina maana CHADEMA wanafuatilia mpaka mahusiano ya unyumba baina ya members wake!
Nimeshangazwa kuona kwamba Hoja na tuhuma alizotoa Slaa haizibiwi bali vijana wa CHADEMA mitandaoni wanatumia muda wao mwingi kubeza, kudhalilisha na kupaka matope hoja hizo. Kuna mmoja amefikia kusema kuwa TRENI LIMEKATIKA BREKI HALIWEZI KUSIMAMA akimaanisha kuwa Slaa hawezi kuzuia nguvu na mchakato wa mabadiliko. Sasa napata kuelewa maana ya maswali ya Dr. Slaa alipouliza kuwa Lowassa anakuja na kundi aina gani? Vijana wa Boda Boda au waliokosa ajira? Mwenye upeo finyu hawezi kupambanua hili swali.
Suala la ASSET na LIABILITY limekuwa hoja kubwa sana hadi kufikia kumuuliza alipotoka CCM 1995 alikwenda CHADEMA alikuwa asset? Aina hii ya udadavuaji wa Hoja imenifumbua macho kwamba asilimia kubwa ya wasomi wetu walihudhuria shule na hawakuelimika. Aina ya maswali wayaouliza mitandaoni ni picha tosha ya kukosa fikra.
MBELE KWA MBELE ni msemo ulioshika chati sana sasa. Ikumbukwe kwamba hawa wanaosema hivyo wanasukumwa na utashi wa watendaji wa serikali waliofeli kwenye utendaji wao na wakakimbilia CHADEMA ili warudi nafasi zao walizoondolewa.
Narejea kwako Tundu Lissu.
Unapoamua kuonyesha mwelekeo wa aina ya majibu yanayofaa kumjibu Dr. Slaa umeficha hekima yako na kuonyesha upumbavu wako.
Hufai tena kuendelea kuaminiwa na hufai kujiita Mzalendo wa nchi hii kwani umeshaonyesha dalili za ulevi wa kisiasa hata hujitambui. Tanzania ilikuwepo na itaendelea kuwepo kabla na baada yako na kikundi chenu.
binafsi Lissu kanisikitisha sana, siamini huu kama ndo uwezo wake kwa sasa, yaani anasema Dr anasema mshenga hasemi mposaji, kama Dr ndo alikuwa mposaji sasa si kisha goma hataki tena kuposa, sasa vipi chama kiendelee na mikakati? mtu akigoma haoi tena humlazimishi, badala yake chama kikaendelea tu kuoa, hapo si kweli kuwa tayari walishapanga?