Tundu Antipas Lissu

Tundu Antipas Lissu

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,657
Baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa kuzungumza na Wanahabari jana. Wakili Msomi ndugu Tundu Lissu aliibukia Voice of America Idhaa ya Kiswahili akijibu Hoja za Slaa kwa style ile ile iliyozoeleka na Chama chake ya KUCHAFUANA.

Wengi mnajua alichoongea hasa hasa akimuingiza mchumba wa Dr. Slaa kuwa anahusika na move aliyoifanya Dr jana. Ninaamini kuwa kwa Chama makini kama CHADEMA walipaswa kuzipangua hoja za Slaa kuliko walivyomtuma Lisu kuongezea hoja juu ya hoja na kuibua interest za wadadisi kujua uadilifu wao.

Katika suala la Josephine kuhusishwa imefikia hata kumdhalilisha Dokta kwa kusema alitupiwa virago vyake nje akalazimika kulala ndani ya gari. Ina maana CHADEMA wanafuatilia mpaka mahusiano ya unyumba baina ya members wake!

Nimeshangazwa kuona kwamba Hoja na tuhuma alizotoa Slaa haizibiwi bali vijana wa CHADEMA mitandaoni wanatumia muda wao mwingi kubeza, kudhalilisha na kupaka matope hoja hizo. Kuna mmoja amefikia kusema kuwa TRENI LIMEKATIKA BREKI HALIWEZI KUSIMAMA akimaanisha kuwa Slaa hawezi kuzuia nguvu na mchakato wa mabadiliko. Sasa napata kuelewa maana ya maswali ya Dr. Slaa alipouliza kuwa Lowassa anakuja na kundi aina gani? Vijana wa Boda Boda au waliokosa ajira? Mwenye upeo finyu hawezi kupambanua hili swali.

Suala la ASSET na LIABILITY limekuwa hoja kubwa sana hadi kufikia kumuuliza alipotoka CCM 1995 alikwenda CHADEMA alikuwa asset? Aina hii ya udadavuaji wa Hoja imenifumbua macho kwamba asilimia kubwa ya wasomi wetu walihudhuria shule na hawakuelimika. Aina ya maswali wayaouliza mitandaoni ni picha tosha ya kukosa fikra.

MBELE KWA MBELE ni msemo ulioshika chati sana sasa. Ikumbukwe kwamba hawa wanaosema hivyo wanasukumwa na utashi wa watendaji wa serikali waliofeli kwenye utendaji wao na wakakimbilia CHADEMA ili warudi nafasi zao walizoondolewa.

Narejea kwako Tundu Lissu.

Unapoamua kuonyesha mwelekeo wa aina ya majibu yanayofaa kumjibu Dr. Slaa umeficha hekima yako na kuonyesha upumbavu wako.

Hufai tena kuendelea kuaminiwa na hufai kujiita Mzalendo wa nchi hii kwani umeshaonyesha dalili za ulevi wa kisiasa hata hujitambui. Tanzania ilikuwepo na itaendelea kuwepo kabla na baada yako na kikundi chenu.
 
Umepoteza muda wako kuandika haya yote wakati ukijua ni upuuzi. Na kawaida mpuuzi ufanya upuuzi bila kujua ni upuuzi na kujikuta amepuuzika.
 
Uanasheria wa Lissu uliisha pale tu alipoamua kuwa mwanasiasa, kaongea pumba tu, Dr. Slaa ametoa tuhuma nzito kwa Chadema, hizo blaablaa za kumshambulia mshumbusi ni wazi sasa hawana agenda na hawawezi kumjibu Dr.
 
sasa nyinyi maccm hivi kweli mna attempt kuizuia treni inayokwenda kwa kasi ya 200kph kwa kutumia kigingi?? wenyewe mnajiita wasomi!!! kigingi chenyewe Slaa!!!! hapo hata mkikingamisha container kwenye reli linakubwa na treni inaendelea kuchanja mbuga.

Mnatakiwa kuishi muutambue upumbavu wenu pale mtakaposhindwa kufunga magoli ya mkono hadharani.
 
Kila familia ina issues zake..kwanini uanze kujibu hoja na family attacks? Alipaswa ku stick na core agenda..sikuipenda hii tabia hata kidogo..
 
Kama cuf wameweza kumpotezea na kumsahau lipumba... Hivyo hivyo na chadema ni wakati wao mzr kumpotezea slaa
Umwmsahau na Hamadi Rashid kule Visiwani. Kama CDM walimfualitia Slaaa katika mahusiano yake na falilia yake, walitaka kufahamu aina ya Kiongozi wao kama anapokea maagizo kutoka jikoni.
 
Kila familia ina issues zake..kwanini uanze kujibu hoja na family attacks? Alipaswa ku stick na core agenda..sikuipenda hii tabia hata kidogo..
Kwa ajili ya kuepuka viongozi wanaongoza nchi kutokea jikoni kama ambavyo Baba wa Taifa aliwahi kuonya.
 
Hivi ni kwa nn Musa alikufa kabla ya kuwafikisha wana-Israel Kaanan?
 
Uanasheria wa Lissu uliisha pale tu alipoamua kuwa mwanasiasa, kaongea pumba tu, Dr. Slaa ametoa tuhuma nzito kwa Chadema, hizo blaablaa za kumshambulia mshumbusi ni wazi sasa hawana agenda na hawawezi kumjibu Dr.

Ni nzito kuliko za escrow account,, na kivuko cha mv dsm?
 
Mtaa post unalazimisha lissu amejibu hoja vzr sana tunataraji ss slaa ajabu ilikuwaje alishiriki kumleta white hair Leo amkatae na tuhuma za kuja wana watu nk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom