Tundu A. Lissu: Kila uchaguzi tangu mwaka '95 kumekuwa na matukio ya mawakala kutopokelewa barua zao za utambulisho, au kukataliwa kuapishwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
*Mh. Tundu A. Lissu akijibu maswali haya yaliyoulizwa

Maswali:
#We miaka ya nyuma mawakala walinyimwa barua au kutolewa nje?

#Miaka ya nyuma makada wakikuwa ndo wakurugenzi?

#Miaka ya nyuma raisi alitishia watakaotangaza upinzani?

Mh. Lissu anajibu kama ifuatavyo:

Majibu ya maswali haya ni ndio, ndio, ndio na ndio. Kila uchaguzi tangu '95, kumekuwa na matukio haya. Wagombea kunyimwa fomu za uteuzi au fomu kutopokelewa kwa sababu ya Wakurugenzi au watendaji wa Kata au Vijiji kukimbia ofisi haijaanza jana.

Kila uchaguzi tangu mwaka '95 kumekuwa na matukio ya mawakala kutopokelewa barua zao za utambulisho, au kukataliwa kuapishwa au fomu zao za viapo kukataliwa na wasimamizi wa vituo.

Na kumekuwa na matukio ya mawakala wetu kutolewa nje au matokeo ya uongo kutangazwa dhidi yetu.

Kuhusu Magufuli kutishia Wakurugenzi wanaotangaza wapinzani, wakati Mzee Freddie Sumaye wetu akiwa Waziri Mkuu, aliwahi kuwatishia maRC, maDC na Wakurugenzi wanaotangaza wapinzani washindi.

Ndio maana Masele alitangazwa mshindi Shinyanga Mjini badala ya marehemu Shelembi wetu mwaka '10. Na huo ni mfano mmoja tu. Fikiria pia wa David Kafulila '15.

Kwa hiyo tumetoka mbali sana na matukio haya.

Hata hivyo, kuna tofauti kubwa kati ya zamani na sasa. Moja, pamoja na kwamba yalikuwa yanatokea, matukio haya yalikuwa ni isolated cases mara nyingi. Hayakuwa sera rasmi ya serikali na hayakuwa yanaratibiwa wazi wazi na vyombo vya dola pamoja na Tume ya Uchaguzi.

Sasa ni sera rasmi ya serikali ya Magufuli, na vyombo vyote vya dola pamoja na Tume vinashiriki wazi wazi kuitekeleza sera hiyo. Sasa hakuna anayejificha tena, wote wako hadharani kuhakikisha hatushindi.

Pili, zamani tulikuwa dhaifu sana. Hatukuwa na chama kabisa katika maeneo mengi; hatukuwa na uwezo wa kuweka wagombea kwenye nafasi nyingi; hatukuweza kufanya kampeni kabisa sehemu nyingi; hatukuweza kuweka mawakala vituoni, n.k.

Udhaifu huu, kwa maoni yangu, ndio uliosababisha kusiwe na sera rasmi ya haya tunayoyaona sasa hivi. Hatukuwa tishio kwa watawala, kwa hiyo hakukuwa na sababu ya kuwa na sera ya ukandamizaji inayotekelezwa na vyombo vyote vya dola pamoja na Tume.

Sasa tuna nguvu kubwa, lakini wengi wetu hatujielewi na hatuelewi cha kufanya. Tuna chama karibu kila mahali na tuna uongozi wa chama wa uthabiti unaotofautiana karibu kila mahali.

Sasa tuna viongozi wa kuchaguliwa na wananchi katika ngazi zote, kuanzia kwenye vitongoji, vijiji na mitaa, Kata na Halmashauri hadi bungeni. Na kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita tulipata kura zaidi ya milioni sita za Urais.

Tuna uwezo wa kuweka wagombea na mawakala kwenye vituo karibu kila mahali. Tuna uwezo wa kufanya kampeni kwa ufanisi nchi nzima.

Kwa kifupi, tuna nguvu kubwa ambayo hatujawahi kuwa nayo miaka ya nyuma. Ndio maana serikali ya Magufuli imegeuza isolated cases za uonevu za zamani kuwa sera rasmi ya utawala wake.

Sasa tatizo ni nini wakati tuna nguvu kubwa??? Moja, hatujielewi. Zamani, kwa sababu tulikuwa wachache, Makao Makuu yalikuwa yanafanya sehemu kubwa ya kazi ya uhamasishaji na kampeni za uchaguzi hadi majimboni.

Tulikuwa dhaifu hivyo Makao Makuu yalikuwa na nguvu kubwa, na kila mtu aliangalia Makao Makuu itatufanyia nini. Na kwenye Makao Makuu kila mtu alimwangalia Mwenyekiti wa Chama atafanya nini.

Leo, wakati tuna chama na uongozi karibu nchi nzima, mtazamo na fikra zetu zimebaki vile vile: Makao Makuu na Mwenyekiti Mbowe watatufanyia nini!!! Kila kitu bado tunaangalia Makao Makuu.

Tunafanyiwa uhuni katika ngazi ya Vijiji, au Mitaa, au Kata au majimbo na watu wetu, viongozi na wanachama, wanaangalia Dar Es Salaam, badala ya kujiangalia wenyewe na kuchukua hatua pale pale unapofanyika uhuni. Hatujielewi.

Pili, hatuelewi mazingira ya sasa na tofauti kubwa kati ya zamani na sasa. Nimesema sasa ukandamizaji ni sera rasmi ya serikali ya Magufuli na CCM na vyombo vya dola pamoja na Tume.

Leo viongozi wetu karibu wote wa juu wako mahakamani. Wabunge wetu wengi wako mahakamani na wengine wameshatumikia vifungo.

Leo viongozi wetu wa ngazi mbali mbali wanatishiwa maisha yao; wengine wameshauawa na wengine, kama mimi, wamefanywa vilema au wanatibu majeraha makubwa.

Leo, karibu nchi nzima, kuwa mwanachama au kiongozi wa CHADEMA wa ngazi yoyote ile ni kukaribisha kila aina ya madhila kutoka kwa serikali na watendaji wake na, hasa, vyombo vya dola.

Kukamatwa bila kosa lolote, kama vile kuvaa nguo za chama au zenye picha za viongozi wetu, ni kitu cha kawaida. Mahabusu za polisi au magereza zimekuwa ndio sebule zetu, na Mahakama zimekuwa ndio vikao vyetu vya chama.

Mikutano ya kisiasa, mara nyingine hata ya ndani isiyokuwa na masharti yoyote ya kisheria, imepigwa marufuku. Watu wetu wanazungumza sana juu ya Dr. Slaa na operesheni za miaka ile, lakini wanasahau kwamba miaka ile hakukuwa na marufuku ya mikutano ya hadhara kama sasa.

Watu wetu wanalalamika sana juu ya kazi ya Wabunge wa upinzani wa sasa, lakini wanasahau kwamba hakuna Bunge Live tena na Spika Ndugai sio Spika Sitta wala Spika Makinda.

Kwa kifupi, hatuelewi mazingira ya sasa ya kisiasa na athari zake kwetu. Ndio maana tunanyoosha vidole vya lawama kwa viongozi wetu wa ngazi za juu, bila kujali kwamba wao ndio victims wa kwanza na wakubwa wa utawala huu wa kidikteta.

Tatu, kwa sababu chama kimekuwa kikubwa na tuko wengi kuliko zamani, tumeanza kujisahau sana. Wengi wetu wanafikiri tutashinda tu kwa sababu sisi ni chama kubwa na tunapendwa na wananchi.

Tumeacha kufanya yale yaliyotufanya tushinde chaguzi za nyuma. Kwa mfano, katika kila uchaguzi wa miaka ya nyuma, tulikuwa tunasindikiza wagombea wetu kwenda kuchukua au kuwasilisha fomu za uteuzi katika mamia na maelfu yetu.

Mkurugenzi anayekimbia ofisi wakati kuna maelfu ya watu nje wakimsindikiza mgombea wao kuchukua au kuwasilisha fomu za uteuzi ni Mkurugenzi jasiri sana.

Zamani tulikuwa tunahamasisha wananchi wasiondoke kwenye vituo vya kupigia na kuhesabia kura na kutangazia matokeo. Hii ilikuwa inatia pressure kwa matokeo ya haki kutangazwa mapema.

Leo ni wangapi wanaohamasisha watu wetu kubakia vituoni au kuhamia kwa Mkurugenzi kushinikiza matokeo halali yatangazwe mapema.

Leo tuna mifano mingi ya kujifunza namna ya kushinda uchaguzi katika mazingira magumu: Ubungo ya Mnyika '10; Arusha ya Lema '10; Nyamagana ya Wenje '10; Arumeru Mashariki ya Nassari '12; Tarime ya Chacha Wangwe '05 na Heche '15, n.k.

Lakini nani kati yetu anayetaka kujifunza na uzoefu huu; na nani kati yetu anayetaka kuufundisha uzoefu huu kwa wageni wengi wa kisiasa tuliowapata baada ya 2010 na, hasa, 2015; au hata kuutumia uzoefu huo katika chaguzi za sasa.

Nani aliye tayari kujifunza au kutufundisha kutokana na makosa mengi ambayo tumekuwa tunayafanya tangu '95 na tunayarudia rudia kila mara??? Kumbuka: wasiojifunza kutokana na historia yao hurudia makosa yao ya nyuma!!!

Nne, sasa tumeingiwa na ugonjwa mbaya unaoitwa kukata tamaa. Kwa watu walioanza siasa za upinzani wakati tumekuwa chama kubwa, hili sio jambo la kushangaza.

Kwa walioingia siasa hizi wakitegemea mteremko tu, na njia iliyopambwa kwa marumaru kuelekea Ikulu au bungeni, hili sio jambo geni. Imetokea kwingineko na lazima itokee na kwetu pia.

Watu wepesi na wanaotegemea mteremko na njia ya marumaru watakata tamaa. Wengine, kama Mtatiro, wataenda kule wanakoona kuna amani ya mioyo yao.

Lakini wengi, hasa ambao wanafahamu kwamba 'there's no easy walk to freedom', watabaki. Men will be separated from the boys. The boys will run away in fear and discouragement. Men will stay and stand up to be counted.

Tano, tususie chaguzi zijazo au tukomae??? Wanaolialia watasema tususie. Wanaotegemea barabara za marumaru watasema tuachane na uchaguzi mpaka Magufuli aondoke au tupate Tume ya Uchaguzi iliyo huru.

Hatujui kama Magufuli hatatuletea ya marafiki zake akina Nkurunzinza, au Kagame, au Kabila au Museveni. Wala hatujui tarehe kamili ya kupatiwa Tume huru. Kwa hiyo kususia kwa sababu hizo ni kuishi kwa matumaini ambayo hayapo. Boycott, in these circumstances, is the way of boys, not of men.

Kwa hiyo tusisusie. Lakini vile vile tusifanye siasa zetu kama ilivyokuwa kabla ya '15.

Moja, tusijiruhusu na tusiruhusu wagombea wetu kwenda kuchukua au kuwasilisha fomu za uteuzi wakiwa peke yao. Tuwasindikize kwa maelfu yetu.

Hatutakuwa tunafanya kosa lolote la jinai, lakini lazima wataleta maaskari kutupiga. Tukifanya hivyo kwenye majimbo matano au kumi watatutawanya kwa urahisi. Tukifanya hivyo kwa majimbo yote nchi nzima hawatatuweza. Hawana majeshi ya aina hiyo.

Najua gharama itakuwa kubwa, lakini lazima tuwe tayari kuilipa ili tuweze kuondoa utawala huu wa kidikteta. Hakuna namna nyingine iliyo rahisi katika mazingira halisi ya Tanzania ya Magufuli.

Pili, tusiruhusu viongozi na wagombea wetu kufanya makosa ya kijinga katika kuandika barua za utambulisho na, hasa, katika kujaza fomu za uteuzi.

Tuzingatie kila sharti la Sheria ya Uchaguzi, Kanuni zake na Maelekezo kwa Vyama vya Siasa na Wagombea tunayopewa wakati wa uchaguzi. Tufahamu: uchaguzi sio mikutano ya hadhara na kampeni tu. Uchaguzi ni pamoja na kujua na kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi. Uchaguzi ni pamoja na kufahamu kila karatasi ya uchaguzi na umuhimu wake.

Tatu, sisi ni mafundi hodari wa mikutano ya hadhara ya mchana. Usiku tunawaachia maCCM. Tunaimba 'hakuna kulala mpaka kieleweke', lakini giza likiingia tu tunarudi kulala na maCCM yanaamka kufanya kazi ya kutushinda uchaguzi. Tujitafakari kwenye hili.

Nne, lazima tufahamu namna ya kushinda uchaguzi siku ya Jumapili Kuu. Mawakala ni maaskari muhimu kwenye vita ya Jumapili Kuu. Tusipeleke maaskari ambao hawajafundishwa namna ya kupigana vita hiyo; au ambao hawajaandaliwa kabisa, au wameandaliwa nusu nusu.

Tano, kwa kuzingatia uzoefu wetu wa nyuma wa sehemu tulikoshinda na tulikoshindwa, tuhamasishe watu wetu wabaki kwenye vituo vya kupigia na kuhesabia kura na hasa katika vituo vya kutangazia matokeo.

Huu uhuni wa kubadilisha fomu za matokeo kwa nguvu ya mapolisi dawa yake ni nguvu ya umma. Tukifanya hivyo kila mahali katika kila kituo cha kupigia na kuhesabia kura na cha kutangazia matokeo, hawatatuweza.

Tukisubiri Mbowe afanye au atoe maelekezo katika kila kituo cha kila kijiji na mtaa, kila Kata na Jimbo la uchaguzi, tutapigwa asubuhi na mapema. Tujiongeze.

Sita, kama tumepata fomu zote za matokeo halali na kuyahakiki, tusisubiri kutangazwa. Tuyatangaze hadharani na mitandaoni na kila mahali ili dunia nzima ifahamu mapema.

Wezi wa kura na maharamia yanashamiri tunapokuwa kimya kusubiri Tume itutangaze. Again, tukifanya hivyo nchi nzima tutashinda. Tukifanya half-heartedly tutapigwa asubuhi na mapema.

Kujitangaza mapema hakuizuii Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo yake, ni kweli. Ya ZEC na Jecha Zanzibar hatujayasahau. Bali kujitangaza mapema kunahamasisha watu wetu kutetea ushindi wao pale ambapo tumeshinda.

Kujitangaza mapema kunaelekeza macho ya kila mtu na ya dunia nzima kwa Tume ya Uchaguzi na kwa vyombo vya dola. Wezi hawapendi kuangaliwa na kila mtu wanapofanya uhalifu wao.

Ukimya na giza vinarahisisha wizi. Tuache ukimya na tuondokane na giza wakati wa kutangaza matokeo.

Mwisho, tuwe na nidhamu. Haya yote hayawezekani kama hatuna nidhamu kama wanachama na viongozi. Hili nimelisemea sana siku za nyuma. Sihitaji kulirudia hapa.

Nawatakieni mjadala wenye faida na kila lenye kheri.

Wasalaam,

Tundu Lissu
Tienen, Belgium
 
Lissu anasema, ''Tano, tususie chaguzi zijazo au tukomae??? Wanaolialia watasema tususie. Wanaotegemea barabara za marumaru watasema tuachane na uchaguzi mpaka Magufuli aondoke au tupate Tume ya Uchaguzi iliyo huru. Kwa hiyo kususia kwa sababu hizo ni kuishi kwa matumaini ambayo hayapo. Boycott, in these circumstances, is the way of boys, not of men''.

Hii paragraph imenichekesha sana kwa sababu Lissu anawaita wanaosusia uchaguzi ni boys lakini wasiosusia uchaguzi anawaita men!

Leo Freeman Mbowe anaitwa boy (kavulana) kwa sababu ameamua kususia uchaguzi!

Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi!

Tutaona na kusikia mengi!
 
Asante Mh Lissu ,ila nime baki Njia panda kabisa ktk kukubaliana na Lissu au kuto kukubaliana nae.
 
Lissu anasema, ''Tano, tususie chaguzi zijazo au tukomae??? Wanaolialia watasema tususie. Wanaotegemea barabara za marumaru watasema tuachane na uchaguzi mpaka Magufuli aondoke au tupate Tume ya Uchaguzi iliyo huru. Kwa hiyo kususia kwa sababu hizo ni kuishi kwa matumaini ambayo hayapo. Boycott, in these circumstances, is the way of boys, not of men''.

Hii paragraph imenichekesha sana kwa sababu Lissu anawaita wanaosusia uchaguzi ni boys lakini wasiosusia uchaguzi anawaita men!

Leo Freeman Mbowe anaitwa boy (kavulana) kwa sababu ameamua kususia uchaguzi!

Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi!

Tutaona na kusikia mengi!

Katika Andiko lake ndicho ulucho kiona tu ?..
 
yani kwa kifupi lissu amesema Mbowe kazi imekushinda
 
Lissu anasema, ''Tano, tususie chaguzi zijazo au tukomae??? Wanaolialia watasema tususie. Wanaotegemea barabara za marumaru watasema tuachane na uchaguzi mpaka Magufuli aondoke au tupate Tume ya Uchaguzi iliyo huru. Kwa hiyo kususia kwa sababu hizo ni kuishi kwa matumaini ambayo hayapo. Boycott, in these circumstances, is the way of boys, not of men''.

Hii paragraph imenichekesha sana kwa sababu Lissu anawaita wanaosusia uchaguzi ni boys lakini wasiosusia uchaguzi anawaita men!

Leo Freeman Mbowe anaitwa boy (kavulana) kwa sababu ameamua kususia uchaguzi!

Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi!

Tutaona na kusikia mengi!
Ndo ulipoona tu hapo,bila shaka unapumuliwa kichogoni itakua
 
Ukifanya uchunguzi utagundua kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 walioshiriki kumchagua Rais ni wapiga kura wasiozidi milioni 15,hii inaonyesha kuwa karibu watu milioni 35 walikuwa passive, atawale shetani au Malaika wao haiwahusu. 2020 watanzania wengi zaidi watakuwa passive, kwani litakuwa ndiyo chaguo lao kutokana na hali ilivyo hivi sasa. Ili kulihamasisha kundi hili piganieni 'TUME HURU' ya uchaguzi, vinginevyo mshindi wa 2020 tunamjua, hivyo basi hatuna sababu za kwende kuungua na jua na kushinda na njaa bure 2020.
 
Naogopa kusoma huu Uzi, nasoma kwa uoga kama kuna MTU ananiona hivi
 
Ni mengi aliyoyagusia Mh Lissu yanayohitaji uchambuzi makini na utekelezaji ndani ya chama.
Katika nyakati ngumu kama hizi, ni muhimu sana chama kijizatiti na kuweka mipango imara kuhakikisha chama hakidhuriki zaidi ya kiasi cha kusambaratika kabisa.

Juhudi nyingi zinahitaji mipango tu ya ndani ya chama inayohitaji kufanyika kimya kimya, tena bila papala.
Makao makuu ya chama yakiwa imara, maana yake ni kuwa chama kitakuwa imara pia ngazi zote hadi shinani.
Hakuna tena nafasi ya kufanya mambo kwa kukurupuka na vurugu. Ni lazima pawe na mpangilio maalum unaotekelezwa kwa utulivu na umakini mkubwa.. Hiyo ndio ishara ya chama kilicho pevuka.

Matukio yooote ya unyanyasaji na uonevu aliyoyagusia Mh Lissu wananchi wanayaona, lakini yanahitaji kuwekewa kumbukumbu zenye ushahidi kila mara na popote yanapotokea. Chama kilichojipanga vizuri hakiwezi kushindwa kulifanya hili kwa makini.

Lakini swali gumu zaidi kuliko yote sasa hivi ni moja: je, upinzani unafanya nini ili chaguzi zifuatazo ziwe za haki? Wakati ndio huu umekwisha! Si lazima jibu liwekwe hapa, lakini swali linajadiliwa ndani ya vyama hivi sasa na kutafutiwa ufumbuzi?
 
Ukifanya uchunguzi utagundua kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 walioshiriki kumchagua Rais ni wapiga kura wasiozidi milioni 15,hii inaonyesha kuwa karibu watu milioni 35 walikuwa passive, atawale shetani au Malaika wao haiwahusu. 2020 watanzania wengi zaidi watakuwa passive, kwani litakuwa ndiyo chaguo lao kutokana na hali ilivyo hivi sasa. Ili kulihamasisha kundi hili piganieni 'TUME HURU' ya uchaguzi, vinginevyo mshindi wa 2020 tunamjua, hivyo basi hatuna sababu za kwende kuungua na jua na kushinda na njaa bure 2020.

"TUME HURU" siioni kabisa. Kwa hiyo inabidi nikubaliane na maoni yako haya - "2020 waTanzania wengi zaidiI WATAKUWA PASSIVE." Na huo ndio ukweli wenyewe.
 
Back
Top Bottom