Hata mimi nililiona,
mtini lilivyonona,
Nkatamani limung'unya,
Pasi hata lidondoa.
Muda nikalivutia,
mikononi lijetua,
Nilile kwa kupembua,
chefuchefu lisijentia.
Tahamaki nastukia,Mwakijiji katungua.
Hata kama uliona, mtini, mezani sokoni
Jinsi lilivyonona, kutamani asilani
Kwa urefu na mapana, kuligusa si utani
Tunda hilo la mzee, kulitamani ni dhambi.
Hata karne ikifika, bado tunda sio lako
Mikono haitarefuka, kuikiuka miiko
Mipaka utaivuka, kufika kule kusiko
Tunda hilo la mzee, kulitamani ni dhambi
Kadi nyekundu pokea, hadi mwisho wa msimu
Mzee wamkosea, kumchukulia utamu
Usia wangu sikia, vya wazee vina sumu
Tunda hilo la mzee, kulitamani ni dhambi