Tunda nimelitungua!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
[FONT=Times New Roman, serif]TUNDA[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelitungua, chini puu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nikalichukua, mikono juu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda ninaling’atua, utamu huu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda ninalilambua, uhondo mkuu![/FONT]

[FONT=Times New Roman, serif]Tunda linanizingua, kwenye miguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelibanjua, kwa utunduu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nililotungua, ni jekunduu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelichambua, ni tamu tuu![/FONT]

[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nikaliparua, bila kisuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda sitoliumbua, kwa wenzanguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda hili siyo mua, si karafuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda langu sio bua, na si kifuu![/FONT]

[FONT=Times New Roman, serif]Tunda limejichanua, uroda huu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelichambua, kwa mkoguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda msijebagua, kisa wivuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nililotumbua, sio vivuu![/FONT]

[FONT=Times New Roman, serif]na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
[/FONT]
 
Wee jamaa wewe...
Mbona mungu amekujalia sana??
Mtu mmoja vipaji lukuki.
Napenda riwaya na mashairi yako...
Nafikiria namna ya kuyakusanya yote,
kisha niyahifadhi katika maktaba yangu.
 
Hatimaye nimepata ile nafasi ya kukupa hongera kaka yangu na mungu akijalie upate muda mrefu wa kulilambua tunda lako. Usisahau kuhalalisha!
 
Wee jamaa wewe...
Mbona mungu amekujalia sana??
Mtu mmoja vipaji lukuki.
Napenda riwaya na mashairi yako...
Nafikiria namna ya kuyakusanya yote,
kisha niyahifadhi katika maktaba yangu.

Hongera sana;
1.kabla hujalikata na kulila ulilisafisha?
2.Ulilikagua kuona kuwa halina dalili ya mdudu ndani?
 
[FONT=Times New Roman, serif]TUNDA[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelitungua, chini puu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nikalichukua, mikono juu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda ninaling’atua, utamu huu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda ninalilambua, uhondo mkuu![/FONT]

[FONT=Times New Roman, serif]Tunda linanizingua, kwenye miguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelibanjua, kwa utunduu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nililotungua, ni jekunduu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelichambua, ni tamu tuu![/FONT]

[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nikaliparua, bila kisuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda sitoliumbua, kwa wenzanguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda hili siyo mua, si karafuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda langu sio bua, na si kifuu![/FONT]

[FONT=Times New Roman, serif]Tunda limejichanua, uroda huu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelichambua, kwa mkoguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda msijebagua, kisa wivuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nililotumbua, sio vivuu![/FONT]

[FONT=Times New Roman, serif]na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)[/FONT]

Hongera nakumiminia,
Kwa juhudi nakuaminia,
Hatimaye tunda umejipatia,
Jitihada nyingi umejifanyia.

Maswali yamejaa kichwani,
Mzee Mzima tunda la nini?
Ulichelewa nini ujanani?
Na tunda hili tunda gani?
 
Nimepitia ugani, fumbo sijafumbua,
Nauliza akilini, ubongo unaungua,
Jibu halipatikani, hakika wanisumbua,
Tunda hilo tunda gani, tunda ulotungua.

Tunda lako la ajabu, namna ulivyochukua,
Uhondo huo aghalabu, miguuni kuingia,
Mzee naomba jibu, kivipi uliparua,
Tunda hilo tunda gani, tunda ulilotungua.
 
Hongera nakumiminia,
Kwa juhudi nakuaminia,
Hatimaye tunda umejipatia,
Jitihada nyingi umejifanyia.

Maswali yamejaa kichwani,
Mzee Mzima tunda la nini?
Ulichelewa nini ujanani?
Na tunda hili tunda gani?
Wewe Charity, kumbe humo kiasi hiki karibu kwenye JF Jazz Band chini ya uongozi wa mtunga mashairi maarufu Bigirita. Nimefurahi
 
Tunda hili la mti gani
Tunda hili la mwaka gani
Tunda hili utamu gani
Tunda hili tunda gani?

hehehe, Mwanakijiji I salute you.
 
Tunda ni tamu mchana au usiku
Tunda linatia kiwewe zaidi usiku
Tunda linazua magomvi kila siku

Tunda ni tamu zaidi ukililamba
Tunda ni tamu ukipiga jaramba
Tunda ni tamu zaidi la Tanga
Tunda ni tamu husipotangatanga

Tunda ni la mmoja si la umoja
Tunda si la kura kama serikali ya umoja
Tunda mshirikiane ili mshibe pamoja
Mwenye kulitoa hasiudhike hata mara moja
 
Tunda hili la mti gani
Tunda hili la mwaka gani
Tunda hili utamu gani
Tunda hili tunda gani?

hehehe, Mwanakijiji I salute you.

tunda hili la ajabu,
kamwe hutapata jibu,
utapekua vitabu,
kulitafuta jawabu,
haitakuwa sababu,
jibu kuliratibu.
 
2.Ulilikagua kuona kuwa halina dalili ya mdudu ndani?
Tunda ukilikagua kichefuchefu kitakupata
Raha ya tunda kulitia kula kama bubu
Tunda husilimenye ndio raha yake
Tamu ya tunda husijue asili yake

Mengine matamu yanapomenywa na wengine
Mengine machungu ukiwa mchumaji wa kwanza
Tunda la kweli huridhike na utamu wake
Tunda la kweli asili yake hutojali

Ubaya wa tunda mdudu utamuona baada ya kushiba
 
Hongera nakumiminia,
Kwa juhudi nakuaminia,
Hatimaye tunda umejipatia,
Jitihada nyingi umejifanyia.

Maswali yamejaa kichwani,
Mzee Mzima tunda la nini?
Ulichelewa nini ujanani?
Na tunda hili tunda gani?
Promota unatisha!!!!
kama kazi umepata
application haitahitajika
umeula kwenye maisha

Promota nakuaminia
hutorusha hata mia
magumi tutayatumia
ukileta za kidunia

Misifa nakumiminia
.....Niendelee nisiendeleeee!!!
 
Tunda ni tamu mchana au usiku
Tunda linatia kiwewe zaidi usiku
Tunda linazua magomvi kila siku

Tunda ni tamu zaidi ukililamba
Tunda ni tamu ukipiga jaramba
Tunda ni tamu zaidi la Tanga
Tunda ni tamu husipotangatanga

Tunda ni la mmoja si la umoja
Tunda si la kura kama serikali ya umoja
Tunda mshirikiane ili mshibe pamoja
Mwenye kulitoa hasiudhike hata mara moja

hahahahaaa!!
mjomba sasa hapo, tarumbeta ukilipuliza huku unashuka hii mistari itakuwa balaaaaaa!
 
JF ikianzisha bendi itakuwa moto wa kuotea mbali... Maprojuza titokezeni kufadhili bendi ys JF
 
Nimepitia ugani, fumbo sijafumbua,
Nauliza akilini, ubongo unaungua,
Jibu halipatikani, hakika wanisumbua,
Tunda hilo tunda gani, tunda ulotungua.

Tunda lako la ajabu, namna ulivyochukua,
Uhondo huo aghalabu, miguuni kuingia,
Mzee naomba jibu, kivipi uliparua,
Tunda hilo tunda gani, tunda ulilotungua.

Hivi wengine mbona hatuna vipaji hata vya kudonoa
 
Hongera nakumiminia,
Kwa juhudi nakuaminia,
Hatimaye tunda umejipatia,
Jitihada nyingi umejifanyia.

Maswali yamejaa kichwani,
Mzee Mzima tunda la nini?
Ulichelewa nini ujanani?
Na tunda hili tunda gani?

Charity Hongera hiki kipaji ni cha kujifunza au cha kuzaliwa
Please naomba majibu ili nami nijifunze
La kama ni cha kuzaliwa basi mie ninefulia
 
Back
Top Bottom