Tunda la mzeituni

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
7,325
9,182
Tunda hili navyosikia ndio tunda walilokula Adam na Hawa na ndio hilihili Mungu aliwakataza wasile.

Kama ni Kweli hilo ndio tunda lenyewe naomba nielezee kidogo na kama sitakuwa sahihi mnisahihishe.

Kwanijuavyo ni kuwa maana ya lile tunda walilokatazwa ni kutokufanyana, kwa bahati mbaya wakafanyana na Mungu akawaambia mtazaa kwa uchungu nawe mwanaume mtakula kwa jasho ndio ukawa mwanzo wa kuzaliana mpaka leo kisa tunda (utamu)

Sasa hili tunda la mzeituni ambalo watu ndio wanasema walikatazwa Adam na Hawa wasile na ndio linauzwa dar kwa sh4000/= , hili ni la wapi? Je, ukila hautodhurika? Hamna tafsiri au maana ya ukila hilo tunda la mzeituni?. Mnaojua mtupe matumizi ya hilo tunda na ni kwa nini linauzwa bei kubwa hivyo kuzidi tufaa?

Kama tunda alilowakataza Adam na Hawa linaitwa mzeituni kwanini walipewa adhabu ile? Kwa nini waliambiwa wakaijaze dunia? Kwa nini maandiko mengi ya Biblia inakataza usizini? Je, hamuoni hiyo ndio ilikuwa dhambi ya asili (kuzini) na wala sio kula lile tunda la mzeituni linalouzwa Dar 4000/=?

Kama ni tunda hilo (mzeituni) ndio walikatazwa na sisi tumelijua kwanini bado tunakula?.

Nakaribisha muongozo.
 
Tunda waliokula lilikuwa tunda halisi na sio kulalana kama mnavyosema.
Ukisoma Bible kwa makini utaelewa baada ya kula tunda na Mungu kugawa adhabu kwa kila mmoja, mbeleni tunasoma; basi Adam akamjua mkewe akapata mimba.
Kwa maana hiyo hakumjua kabla. Ungekuta tunda linaloongelewa ni ngono, basi mbeleni tungeambiwa Adam akamjua mkewe kwa mara ya pili
 
Back
Top Bottom