Tunda gani hili?

Hili tunda linaitwa NGULULU,huliwa na watoto kama zabibu lina sukari na mlendamlenda,wakubwa pia tunayala na kuyatumia kama gundi ofisini kwa sababu ya kunatanata kwake,yanapatikana zaidi Moshi(v)vijiji vya Chemchem na Mikocheni.

Mmh hapana umeyafananisha
 
kwetu tunaita mishibili,
yanapendwa sana na ngedere na yakiwa mabichi hayaliki,
ndani yana mbegu mbili ama moja ya brown.
home sweet home
 
Moshi huoteshwa mpakani mwa shamba na mti wake ni mgumu sana,majani yake huliwa na mbuzi...mshana jr vipi kiimani mti wake au hilo tunda vina kazi yoyote?
Hauna shida kabisa huo ndio maana mazao yake huliwa na viumbe hai
 
Hauna shida kabisa huo ndio maana mazao yake huliwa na viumbe hai
Kwetu Tukuyu tunaziita Songwa, Mti wake ni Mgumu hatari. Walimu wakiagiza Fimbo shuleni enzi hizo, wale wanoko wanaleta hiyo Misongwa, huwa haikati migumu wakorofi mbona mtafurahi! Zikiwa Mbichi ni Chachu Chachu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom