Tunawachekea Wachina huku wakitubamiza!

Tunawachekea Wachina huku wakitubamiza!

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331
mbwambo.jpg

Tafakuri Jadidi

Tunawachekea Wachina huku wakitubamiza

Johnson Mbwambo

Toleo la 324
6 Nov 2013

324_wachina.jpg

  • Wenzetu Niger, Gabon, Chad tayari wanajuta

WIKI iliyopita vyombo vya habari nchini viliripoti kukamatwa kwa pembe za ndovu 706 katika nyumba moja ya Mikocheni, Dar es Salaam wanakoishi wafanyabiashara watatu wa Kichina.
Operesheni ya kuwakamata Wachina hao na pembe hizo iliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

Pembe 706 za ndovu maana yake ni kwamba tembo wapatao 353 waliuawa nchini. Katika nchi kama Tanzania ambayo idadi ya tembo katika mbuga zake inapungua kwasi, huhitaji kuwa mtaalamu kufahamu kuwa tukiwachekea Wachina tembo watakwisha kabisa nchini.

Labda nikumbushe hapa kwamba hiyo si mara ya kwanza kwa Wachina kukamatwa na pembe za ndovu. Na wala pembe za ndovu si biashara pekee haramu ambayo Wachina hujishughulisha nayo Tanzania; kwani rekodi zinaonyesha kuwa, hushiriki pia katika biashara haramu za magogo na madini.

324_pinda.jpg
Kukamatwa kwa Wachina hao watatu wakiwa na pembe hizo 706 kumekuja siku chache tu baada ya Waziri Mkuu wetu, Mizengo Pinda kurejea nyumbani kutoka katika ziara ya kiserikali ya “mafanikio makubwa” ya nchini China.

Akiwa China, Waziri Mkuu Pinda aliambiwa ya kuwa zaidi ya Watanzania 120 wamo katika magereza mbalimbali ya nchi hiyo kwa kukamatwa na madawa ya kulevya. Baadhi yao tayari wameshahukumiwa vifo na wanasubiri tu kutekelezwa kwa adhabu hizo.

Tumefahamishwa kwamba, juhudi zote za Pinda za kuwaombea Watanzania hao wasinyongwe zimegonga mwamba kwa kuwa Serikali ya China “haina mzaha na wafanyabiashara wa dawa za kulevya.”
Kimsingi, ukiondoa unyama na athari za biashara ya madawa ya kulevya kwa jamii, kosa la kushiriki biashara hiyo haramu ni jinai tu kama yalivyo makosa ya kujishughulisha na biashara nyingine haramu kama vile pembe za ndovu, madini au magogo, na hivyo yote yanastahili adhabu kali.

Lakini wakati ambapo zaidi ya Watanzania 120 wamo katika magereza ya China kwa kukamatwa na madawa ya kulevya, sitashangaa kuambiwa kwamba hakuna hata Wachina watano waliofungwa katika magereza ya Tanzania kwa kukamatwa wakishiriki katika biashara haramu za pembe za ndovu, madini au magogo!
Kwa maneno mengine, sitashangaa pia kuona Wachina hao watatu waliokamatwa na pembe 706 za ndovu wakiachiwa katika mazingira ya kutatanisha au kila wakifikishwa mahakamani kesi zao kupigwa danadana, na mwishowe kuachiwa huru!

Kwa mtazamo wangu, kiwango cha ushiriki wa Watanzania katika biashara haramu ya madawa ya kulevya huko China kinalingana kabisa na kiwango cha ushiriki wa Wachina katika biashara haramu za pembe za ndovu, magogo na madini hapa nyumbani Tanzania.
Tofauti pekee ni kwambva kule China wanapokamatwa Watanzania hufungwa magerezani, na ndiyo maana idadi yao imefikia zaidi ya 120, lakini hapa Tanzania ni nadra kuwakuta Wachina wapo magerezani kwa kukamatwa na pembe za ndovu, madini au magogo!

Ni kwa nini hali iko hivyo? Ni kwa sababu Serikali ya Tanzania inaiona China kuwa ni “rafikiye mkubwa” na mwekezaji mwenye nia njema na nchi yetu, na hivyo haitaki kuiudhi kwa namna yoyote ile kama vile kuwafunga gerezani raia wake wanaokamatwa nchini wakifanya biashara haramu.
Kwa hiyo, wakikamatwa Wachina hapa Tanzania, zitafanyika juhudi za chini chini za kidiplomasia kuwaachia huru; lakini wakikamatwa Watanzania kule Beijing, diplomasia hiyo haifanyi kazi kwao kuwanusuru Watanzania wenzetu na vifo au vifungo! Kwa maneno mengine, ni diplomasia ya upande mmoja tu.

Ndugu zangu, ninachojaribu kueleza hapa, na ambacho nilishawahi kukieleza huko nyuma ni kwamba; China si rafiki wa kweli wa Tanzania kama ambavyo watawala wetu wanajaribu kutuaminisha.
Labda niende mbali zaidi na kusema kuwa, katika dunia ya sasa hakuna kitu kama “rafiki wa kweli” kwenye mahusiano ya kimataifa. Kila nchi huwa inajali kuangalia na kulinda maslahi yake tu, na hivyo mahusiano yanapaswa kuwa ya “nipe nikupe”.

Kwa bahati mbaya, watawala wetu wanajipendekeza mno kwa China kiasi kwamba “tunachotoa” hakilingani na “tunachopata”. Na bahati mbaya zaidi, watawala wetu wanashindwa hata kujifunza kutoka kwa nchi kama Niger, Chad na Gabon ambazo ‘zimelizwa’ na Wachina katika uwekezaji, na sasa zinahaha kurekebisha mikataba ya kifisadi zilizoingia nayo.

Sitaki msomaji wangu nikuchoshe kukuelezea kinachoendelea Gabon na Chad kuhusu mahusiano ya sasa ya kiuwekezaji ya nchi hizo na China, lakini mfano wa Niger unanishawishi nikusimulie kidogo.
Mwaka 2008 Niger ilikuwa chini ya mtawala dikteta na fisadi mpenda fedha kupindukia anayeitwa Mamadou Tandja. Huyu aliingia mikataba kadhaa ya siri na mashirika ya mafuta ya China iliyowezesha nchi hiyo kuchimba mafuta Niger na kuyapeleka China.

Mikataba hiyo ilibaki kuwa siri hadi dikteta huyo alipopinduliwa na wanajeshi mwaka 2010, na ndipo mikataba hiyo ilipoanikwa hadharani na kubainika kuwa kumbe Mamadou Tandja alilipwa binafsi na Wachina dola milioni 300 kama “bonasi” ya kusaini mikataba hiyo ya kifisadi, na ndiyo maana ilifanywa siri!
Hivi sasa watawala wa Niger – moja ya nchi masikini kabisa duniani ingawa ina mafuta, imeiwekea ngumu China, na inaendesha nayo majadiliano mapya kurekebisha mikataba yote hiyo ya Mamadou Tandja ili iwe na manufaa kwa taifa hilo.

“Mafuta ndiyo utajiri pekee tulionao Niger. Tukiyatoa kiholela kwa wageni, hatutaweza kamwe kujiondoa kwenye umasikini,” ndivyo Waziri wa Mafuta wa Niger, Foumakoye Gado, alivyokaririwa na gazeti la New York Times toleo la Septemba 17, 2013.

Sina hakika majadiliano hayo mapya kati ya Niger na China kuhusu mikataba hiyo ya kifisadi ya Mamadou Tandja yamefikia wapi; lakini lililo dhahiri ni kwamba, nchi hiyo imewageuzia kibao Wachina na imechukua hatua kujihami, na hilo ni funzo kubwa kwa watawala wetu Tanzania.
Ni funzo kubwa kwa watawala wetu Tanzania kwa sababu nasi tuna mikataba na Serikali ya China ambayo, mpaka sasa, inafanywa siri, na pengine itaendelea kufanywa siri mpaka hapo Serikali ya CCM itakapotoka madarakani.

Mfano wa mikataba hiyo inayofanywa siri ni ule wa ujenzi wa bandari mpya huko Bagamoyo utakaofanywa na Serikali ya China. Kwa sababu ya usiri wake, kuna minong’ono mingi mno kuhusu yaliyomo kwenye mkataba huo.
Kwa mfano, kuna madai kuwa China itagharimia ujenzi wa bandari hiyo itakayokuwa kubwa na ya kisasa kushinda nyingine zote Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa sharti kuwa menejimenti ya bandari hiyo iwe ya Kichina kwa miaka 35!

Kama hilo ni kweli, na kwa kuzingatia ushiriki wa Wachina katika biashara haramu za pembe za ndovu, magogo na madini barani Afrika, basi, maana yake ni kwamba watakuwa wamejipatia bandari yao wenyewe ya kusafirisha magendo hayo kupeleka nyumbani China bila kubugudhiwa na vyombe vyetu vyovyote!

Kama bado hawana bandari wanayoisimamia wenyewe hapa nchini ya kupitishia magendo yao, na bado pembe nyingi za ndovu wanaouawa hapa nchini na majangili zinaishia China (kama ilivyo pia kwa magogo), hali itakuwaje siku wakiwa na bandari yao (Bagamoyo) wanayoisimamia wenyewe kwa miaka 35?
Tuambizane ukweli; taifa lolote linalotia saini mikataba ya siri na watawala madikteta na mafisadi wa Afrika kama vile Mamodou Tandja wa Niger, ni taifa ambalo urafiki wake na bara la Afrika ni wa kutilia shaka.
Ndugu zangu, China si rafiki mwema kama tunavyodhania!
Tafakari.

^^
Mfadhili wako anapofumba macho huku anakuibia..ukifumbua macho ukasema asante..basi ujue ulipewa ubongo kwa makosa
^^
 
Haya ndio maneno ya kuwaambia walipiga kura. ccm hii LAZIMA ING'OKE 2015
 
Nadhani ukisema "TUNAWACHEKEA" wachina ni neno lenye upole sana na litashindwa kuakisi hali halisi nadhani "TUNAJICHEKELESHA" kwa Wachina....
 
wachina watatuua na sumu toka kwenye bidhaa zao.
 
mbwambo.jpg

Tafakuri Jadidi

Tunawachekea Wachina huku wakitubamiza

Johnson Mbwambo

Toleo la 324
6 Nov 2013

324_wachina.jpg

  • Wenzetu Niger, Gabon, Chad tayari wanajuta

WIKI iliyopita vyombo vya habari nchini viliripoti kukamatwa kwa pembe za ndovu 706 katika nyumba moja ya Mikocheni, Dar es Salaam wanakoishi wafanyabiashara watatu wa Kichina.
Operesheni ya kuwakamata Wachina hao na pembe hizo iliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

Pembe 706 za ndovu maana yake ni kwamba tembo wapatao 353 waliuawa nchini. Katika nchi kama Tanzania ambayo idadi ya tembo katika mbuga zake inapungua kwasi, huhitaji kuwa mtaalamu kufahamu kuwa tukiwachekea Wachina tembo watakwisha kabisa nchini.

Labda nikumbushe hapa kwamba hiyo si mara ya kwanza kwa Wachina kukamatwa na pembe za ndovu. Na wala pembe za ndovu si biashara pekee haramu ambayo Wachina hujishughulisha nayo Tanzania; kwani rekodi zinaonyesha kuwa, hushiriki pia katika biashara haramu za magogo na madini.

324_pinda.jpg
Kukamatwa kwa Wachina hao watatu wakiwa na pembe hizo 706 kumekuja siku chache tu baada ya Waziri Mkuu wetu, Mizengo Pinda kurejea nyumbani kutoka katika ziara ya kiserikali ya "mafanikio makubwa" ya nchini China.

Akiwa China, Waziri Mkuu Pinda aliambiwa ya kuwa zaidi ya Watanzania 120 wamo katika magereza mbalimbali ya nchi hiyo kwa kukamatwa na madawa ya kulevya. Baadhi yao tayari wameshahukumiwa vifo na wanasubiri tu kutekelezwa kwa adhabu hizo.

Tumefahamishwa kwamba, juhudi zote za Pinda za kuwaombea Watanzania hao wasinyongwe zimegonga mwamba kwa kuwa Serikali ya China "haina mzaha na wafanyabiashara wa dawa za kulevya."
Kimsingi, ukiondoa unyama na athari za biashara ya madawa ya kulevya kwa jamii, kosa la kushiriki biashara hiyo haramu ni jinai tu kama yalivyo makosa ya kujishughulisha na biashara nyingine haramu kama vile pembe za ndovu, madini au magogo, na hivyo yote yanastahili adhabu kali.

Lakini wakati ambapo zaidi ya Watanzania 120 wamo katika magereza ya China kwa kukamatwa na madawa ya kulevya, sitashangaa kuambiwa kwamba hakuna hata Wachina watano waliofungwa katika magereza ya Tanzania kwa kukamatwa wakishiriki katika biashara haramu za pembe za ndovu, madini au magogo!
Kwa maneno mengine, sitashangaa pia kuona Wachina hao watatu waliokamatwa na pembe 706 za ndovu wakiachiwa katika mazingira ya kutatanisha au kila wakifikishwa mahakamani kesi zao kupigwa danadana, na mwishowe kuachiwa huru!

Kwa mtazamo wangu, kiwango cha ushiriki wa Watanzania katika biashara haramu ya madawa ya kulevya huko China kinalingana kabisa na kiwango cha ushiriki wa Wachina katika biashara haramu za pembe za ndovu, magogo na madini hapa nyumbani Tanzania.
Tofauti pekee ni kwambva kule China wanapokamatwa Watanzania hufungwa magerezani, na ndiyo maana idadi yao imefikia zaidi ya 120, lakini hapa Tanzania ni nadra kuwakuta Wachina wapo magerezani kwa kukamatwa na pembe za ndovu, madini au magogo!

Ni kwa nini hali iko hivyo? Ni kwa sababu Serikali ya Tanzania inaiona China kuwa ni "rafikiye mkubwa" na mwekezaji mwenye nia njema na nchi yetu, na hivyo haitaki kuiudhi kwa namna yoyote ile kama vile kuwafunga gerezani raia wake wanaokamatwa nchini wakifanya biashara haramu.
Kwa hiyo, wakikamatwa Wachina hapa Tanzania, zitafanyika juhudi za chini chini za kidiplomasia kuwaachia huru; lakini wakikamatwa Watanzania kule Beijing, diplomasia hiyo haifanyi kazi kwao kuwanusuru Watanzania wenzetu na vifo au vifungo! Kwa maneno mengine, ni diplomasia ya upande mmoja tu.

Ndugu zangu, ninachojaribu kueleza hapa, na ambacho nilishawahi kukieleza huko nyuma ni kwamba; China si rafiki wa kweli wa Tanzania kama ambavyo watawala wetu wanajaribu kutuaminisha.
Labda niende mbali zaidi na kusema kuwa, katika dunia ya sasa hakuna kitu kama "rafiki wa kweli" kwenye mahusiano ya kimataifa. Kila nchi huwa inajali kuangalia na kulinda maslahi yake tu, na hivyo mahusiano yanapaswa kuwa ya "nipe nikupe".

Kwa bahati mbaya, watawala wetu wanajipendekeza mno kwa China kiasi kwamba "tunachotoa" hakilingani na "tunachopata". Na bahati mbaya zaidi, watawala wetu wanashindwa hata kujifunza kutoka kwa nchi kama Niger, Chad na Gabon ambazo ‘zimelizwa' na Wachina katika uwekezaji, na sasa zinahaha kurekebisha mikataba ya kifisadi zilizoingia nayo.

Sitaki msomaji wangu nikuchoshe kukuelezea kinachoendelea Gabon na Chad kuhusu mahusiano ya sasa ya kiuwekezaji ya nchi hizo na China, lakini mfano wa Niger unanishawishi nikusimulie kidogo.
Mwaka 2008 Niger ilikuwa chini ya mtawala dikteta na fisadi mpenda fedha kupindukia anayeitwa Mamadou Tandja. Huyu aliingia mikataba kadhaa ya siri na mashirika ya mafuta ya China iliyowezesha nchi hiyo kuchimba mafuta Niger na kuyapeleka China.

Mikataba hiyo ilibaki kuwa siri hadi dikteta huyo alipopinduliwa na wanajeshi mwaka 2010, na ndipo mikataba hiyo ilipoanikwa hadharani na kubainika kuwa kumbe Mamadou Tandja alilipwa binafsi na Wachina dola milioni 300 kama "bonasi" ya kusaini mikataba hiyo ya kifisadi, na ndiyo maana ilifanywa siri!
Hivi sasa watawala wa Niger – moja ya nchi masikini kabisa duniani ingawa ina mafuta, imeiwekea ngumu China, na inaendesha nayo majadiliano mapya kurekebisha mikataba yote hiyo ya Mamadou Tandja ili iwe na manufaa kwa taifa hilo.

"Mafuta ndiyo utajiri pekee tulionao Niger. Tukiyatoa kiholela kwa wageni, hatutaweza kamwe kujiondoa kwenye umasikini," ndivyo Waziri wa Mafuta wa Niger, Foumakoye Gado, alivyokaririwa na gazeti la New York Times toleo la Septemba 17, 2013.

Sina hakika majadiliano hayo mapya kati ya Niger na China kuhusu mikataba hiyo ya kifisadi ya Mamadou Tandja yamefikia wapi; lakini lililo dhahiri ni kwamba, nchi hiyo imewageuzia kibao Wachina na imechukua hatua kujihami, na hilo ni funzo kubwa kwa watawala wetu Tanzania.
Ni funzo kubwa kwa watawala wetu Tanzania kwa sababu nasi tuna mikataba na Serikali ya China ambayo, mpaka sasa, inafanywa siri, na pengine itaendelea kufanywa siri mpaka hapo Serikali ya CCM itakapotoka madarakani.

Mfano wa mikataba hiyo inayofanywa siri ni ule wa ujenzi wa bandari mpya huko Bagamoyo utakaofanywa na Serikali ya China. Kwa sababu ya usiri wake, kuna minong'ono mingi mno kuhusu yaliyomo kwenye mkataba huo.
Kwa mfano, kuna madai kuwa China itagharimia ujenzi wa bandari hiyo itakayokuwa kubwa na ya kisasa kushinda nyingine zote Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa sharti kuwa menejimenti ya bandari hiyo iwe ya Kichina kwa miaka 35!

Kama hilo ni kweli, na kwa kuzingatia ushiriki wa Wachina katika biashara haramu za pembe za ndovu, magogo na madini barani Afrika, basi, maana yake ni kwamba watakuwa wamejipatia bandari yao wenyewe ya kusafirisha magendo hayo kupeleka nyumbani China bila kubugudhiwa na vyombe vyetu vyovyote!

Kama bado hawana bandari wanayoisimamia wenyewe hapa nchini ya kupitishia magendo yao, na bado pembe nyingi za ndovu wanaouawa hapa nchini na majangili zinaishia China (kama ilivyo pia kwa magogo), hali itakuwaje siku wakiwa na bandari yao (Bagamoyo) wanayoisimamia wenyewe kwa miaka 35?
Tuambizane ukweli; taifa lolote linalotia saini mikataba ya siri na watawala madikteta na mafisadi wa Afrika kama vile Mamodou Tandja wa Niger, ni taifa ambalo urafiki wake na bara la Afrika ni wa kutilia shaka.
Ndugu zangu, China si rafiki mwema kama tunavyodhania!
Tafakari.

Kama ni hivyo, wawekwe kizuizini ili tubadilishane hawa na mateja, kwani tukiwapeleka mahakamani wataachiwa huru.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Okoa Tanzania kwa kuindoa ccm madarakani
 
^^
mfadhili wako anapofumba macho huku anakuibia..ukifumbua macho ukasema asante..basi ujue ulipewa ubongo kwa makosa
^^

hatuwachekei.tunawakenulia.tunawakenulia hata watusi.tunakenulia eac wakati eac ni bahima empire in the making.!!!!.NAKUBALIANA NA WEWE MKUU KWAMBA TUMEPEWA UBONGO KWA MAKOSA.
 
Mkuu BAK watawala wetu wamefunga macho na masikio yao hawaoni wala hawasikii na hata ukipiga kelele za madebe hawatasikia maana washapata chao na hawahitaji wewe au mimi tujue ni nini walichoingia kwenye mikataba yao na ina nini hiyo mikataba
Mpaka tuje kushtuka nchi itakuwa na picha za tembo na faru kwenye museum zetu kuwa hapo zamani za kale tuliwahi kuwa na tembo na faru na hapa kulikuwa na msitu mkubwa sana ila kuna watu walipita na mashine zao wakafyeka msitu wote au hapa kulikuwa na madini au gesi au mafuta ila tuliwakabidhi wachina na wamemaliza kila kitu
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu Rocky yote hayo ni majizi na mafisadi. Mali ya nchi wanaifanya kama ni mali yao binafsi kwa kukosa hata woga na kuamua kusaini mikataba na kuifanya siri kwa sababu wanajua fika kwamba mikataba hiyo ikiwekwa hadharani Watanzania hatutaikubali.

Wamehongwa mabilioni ya pesa na kuyaficha nchi za nje ikiwemo Dubai, Jersey Island na kwingineko. Haingii akilini kusaini mkataba wa kujengewa bandari na kisha kuwapa hao wajengaji mamlaka ya kuendesha bandari hiyo bila kuingiliwa na Serikali ya nchi husika kwa miaka 35!!!! Ni Serikali ya kifisadsi tu ndiyo inaweza kusaini mikataba isiyo na maslahi kama hii ya nchini kwetu, na huwezi kusikia nchi yoyote duniani inasaini mikataba ya kifisadi kiasi hiki.

Mkuu BAK watawala wetu wamefunga macho na masikio yao hawaoni wala hawasikii na hata ukipiga kelele za madebe hawatasikia maana washapata chao na hawahitaji wewe au mimi tujue ni nini walichoingia kwenye mikataba yao na ina nini hiyo mikataba
Mpaka tuje kushtuka nchi itakuwa na picha za tembo na faru kwenye museum zetu kuwa hapo zamani za kale tuliwahi kuwa na tembo na faru na hapa kulikuwa na msitu mkubwa sana ila kuna watu walipita na mashine zao wakafyeka msitu wote au hapa kulikuwa na madini au gesi au mafuta ila tuliwakabidhi wachina na wamemaliza kila kitu
 
Last edited by a moderator:
Bidhaa feki zinatoka China, simu feki, Nguo feki (nGuo zinapauka).

Mabomu ya kuuwa watanzania yalitoka China, refer Bomu la soweto Arusha

Mtwara, akina mama na Dada wanateswa na kubakwa ili Wachina wajenge Bomba la gesi

Dawa za matibabu feki kutoka china
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi tangu Shell BP ianzishe uchimbaji wa mafuta nchini Nigeria tangu 1958, leo hii Serikali yao inaweza kuja na takwimu ya kuonyesha kwamba nchi na raia wa Nigeria waliwahi kufaidika na utajiri wa mafuta hayo? Kwa nini unyonyaji wa nchi za magharibi tunauonea haya, lakini inapokuja suala la nchi za Mashariki ya mbali tunazisema vibaya kupindukia especially China - nakubali China inaweza kuwa na mapungufu yake lakini mengine tunaweka chumvi mno, nashangaa Waswahili wanapo walahumu Wachina kwa bidhaa feki wakati ni waswahili hawa hawa wanaokwenda China na kununua bidhaa hizo hafifu, wanahacha kununua high quality products maksudi kutokana na uchu wa kutaka kutajirika haraka haraka. Nakumbuka Balozi wa Uchina hapa nchini aliwahi kuwasema sana wafanya bihashara Watanzania wanao kwenda Uchina na kununua bidhaa feki ili waje wapate faida kubwa na kuwaharibia sifa Wachina.
 
Na ndiyo maana ili kukifanya kizazi kijacho cha Tanzania kutoweza kufikiri wamekuja na Div.Five au wenyewe wanaiita BIG Results Now.Ili watoto wao na vijukuu na vitukuu viendelee kutawala na kula pesa walizofisadi Baba zao na babu zao.Kwa sasa Tanzania tumeshauzwa siku nyingi tuombe Mungu tu aunusuru na balaa hili.Viongozi wetu hawaogopi hata aliyewaumba,sijui kama wanajua wanatengeneza tabaka la walionacho na wasionacho na mwisho wa siku vita ya walionacho na wasionacho inatengenezwa.:disapointed:
 
Operesheni Ondoa CCM na machine vinginevyo nchi itabaki vvumbi tupi machine si mali kitu na hivi sasa yameruhusiwa na CCM kufanya yatakayo kuanzia kuvua samaki katikaati ya kina ,kuvuna madini misitu na wanyama hawafai hata kwa gharama ya sindano
 
tunakushukuru mkuu kwa kulitambua hilo .
 
Mikataba feki na kila kitu feki ndiyo maana hawa watawala wanaojua fika hii mikataba jinsi ilivyojaa madudu wanajitahidi kila wawezalo kuzusha kila wawezalo kuhakikisha kwamba CHADEMA haichukui madaraka ya nchi maana kama CHADEMA wataingia madarakani na kuianika mikataba hii hadharani kuona jinsi hawa mafisadi walivyokuwa hawajali maslahi ya Tanzania na Watanzania, Watanzania wengi watalia machozi ya uchungu mkubwa na hawa mafisadi wote hawana mahali watapakapostahili kuishi ila lupango.

Ukiona watawala wanang'ang'ania kuendelea kuwepo madarakani kwa kila hila hata kutumia mabavu wakati kuna ushahidi wa kutisha kuonyesha kwamba uongozi wa nchi umeshawashinda basi jua hao watawala feki wanaogopa madudu yao yakianikwa hadharani basi utajiri wao wa mabilioni utawapeleka mahali pabaya sana.

Bidhaa feki zinatoka China, simu feki, Nguo feki (nGuo zinapauka).

Mabomu ya kuuwa watanzania yalitoka China, refer Bomu la soweto Arusha

Mtwara, akina mama na Dada wanateswa na kubakwa ili Wachina wajenge Bomba la gesi

Dawa za matibabu feki kutoka china
 
Hii Biashara ya Pembe za ndovu na Dawa za Kulevya sio bure..... Kuna malengo ya kukusanya Pesa nyingi ili kununua vibaraka wa kuvuruga upinzani Tanzania hasa CHADEMA.

Haiwezekani kuna Usalama wa taifa, kuna Polisi, kuna idara ya wanyama pori halafu wako kimya, Tembo wanaangamia..... Hii iliachwa biashara iendelee ili wapate pesa za kuvuruga CDM kwa kununua baadhi ya Viongozi... Pia Ni ajabu biashara ya Unga COcaine iachwe tu ishamiri
 
Back
Top Bottom