Tunawachekea Wachina huku wakitubamiza!

Tunawachekea Wachina huku wakitubamiza!

Kabla ya Wachina kuongeza ushirikiano na sisi na hata sasa makampuni yenye kunufaika kutokana na utajiri wa rasilimali zetu takriban zote ni za ulaya na USA! Waandishi wengi huwa wanafumbia macho mambo yanayowahusu WAZUNGU!.... Richmond ilipigiwa makelele, wakaibadili jina na kuitwa Dowans nayo mkapiga makelele, mara Hillary Clinton akajitokeza hadharani kwa jina la Symbion! waandishi mkawekwa sawa kisha wote wakafyata mkia...
Dhahabu zote zinazozalishwa Tanzania zinakwenda kwa wazungu! Uranium etc zote hizi hazisemwi pengine kwa kuwa kiasi cha uchakavu kinarejea via NGOs na Baadhi ya Makanisa!
Akina Mbwambo et al hawaoni hawakemei! WHy Chinese? Jibu ni jepesi sana kuwa Western Nations wameingiliwa interest zao! na hawa waandishi wetu wachumia tumbo wote ni mapro west!
nchi ya Niger ilianza kuchimba mafuta muda mrefu sana, hata JKN aliwahi kuwashauri wajitenge ili wafaidike kutokana na rasilimali walizokuwa nazo, enzi hizo wachina walikuwa hawako Niger! si hitaji kufafanua hili...Nchi ya Equatorial Guinea tayari inang'aa ndani ya miaka 10 ya mkataba na wachina! Miaka 40 ya nchi za kimagharibi ziliwatumbukiza kwenye lindi la umasikini uliokithiri pamoja na utajiri mkubwa wa mafuta waliyonayo...
Nawaasa sana waandishi ambao wengi ni mapro west, mfumbue macho kisha muandike hoja zenye mashiko zenye kutujenga watanzania, zenye uzalendo wa dhaati!
Tulitarajia kuwa hoja ya Marehemu CHACHAGE kuwa Sera tulizoletewa kisha wabunge wachumia tumbo wa CCM wakaipitisha zikiwemo sera za ubinafsishaji, sera ya madini, zilikuwa na makusudio ya kukwapua rasilimali zatu...Prof alisema "Tunaandaliwa kuwekezwa"! Pengine waandishi na CCM wanapenda kukilimbitwa na wazungu, pengine kitu cha mchina kidogo hakiwafikishi kisawasawa?....Tafakuri pana inahitajika katika hili... Tanzania itanawirishwa kwa Watanzania wenyewe!
 
Back
Top Bottom