Karandinga
Member
- Jun 25, 2008
- 66
- 1
Najua wengi wenu humu bado umri wenu ni mdogo hivyo hamkubahatika kusomeshwa na huyu SHUJAA aliyeamua kuweka mbele UZALENDO mbele ya UBINAFSI na aliamua kuinvest JASHO na DAMU yake kwa ajili ya nchi hii tangu alipoamua kuondoka kwao Jamaica miaka ya 60..
Prof Edwards ndie mwanzilishi wa KITIVO CHA BIASHARA pale UD na amewasomesha watu wengi na wengine leo ni mawaziri na mabosi wa mashirika mbali mbali Tanzania
Hakuishia hapo aliamua kwenda kuanzisha chuo cha BIASHARA kule Arusha na leo serikali yetu ya KIFISADI inajidai ni chake na kwa kusudi walimnyima huyu mzee URAIA huku majitu kama akina Subash Patel wakipewa uraia, waliamua kumtelekeza wakati anaumwa mpaka umauti ulipo mfika
Sisi wana JAMII FORUMS tunapenda kuinyesha hii serikali ya kidhalimu kuwa in this day and age ambayo we cant find HEROES kuwa tutamuenzi na tunauomba uongozi wa UD wamuenzi halau hata kwa kukipa kitizo cha BIASHARA jina lake
Inna Lillahi Wa Inna Illahi Raj'uun
Mwenye picha tafadhalini wekeni hapa na btw huyu jamaa alioa Mwanamke wa Kitanzania enzi hizo...mazishi yameahirishwa mpaka WEEKEND ijayo...kama kuna watu wenye michango na ideas za namna ya kumuenzi huyu Shujaa tafadhalini leteni mawazo yenu mimi niko close na jamaa wanaotaka kumfanyia kitu japo Serikali bado imegoma hata kutuma salam za rambi rambi
May The Almighty rest his soul in eternal peace...So Jah Seh