Tunavyofikiri around mikataba: Process ya makubaliano mapya na Maximo

Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
64
Yani Maximo mwenyewe ndio amewaambia TFF, jamani eeh, slow down guys, msinipe mkataba wa miaka miwili. Ngojeni tuone mafainikio baada ya mwaka unaokuja.

Na kama wewe ni mwajiri unatafuta mtu wa miaka miwili, halafu kwenye interview candidate anakwambia nipe mmoja, inakuonyesha 1) candidate aidha hana long term commitment na organization yako, au 2) hajiamini.

Mimi sijawahi kuandika mkataba wa serikali or anything like that lakini hata kwa kuangalia ESPN tu, shoo za michezo, you know kwamba ni mwajiri ndio ana dictate urefu mkataba, sio the candidate jamani!

Halafu Tenga anamtetea Maximo kwamba mapungufu ni ya kibinadamu. Public relations blunder. Husafishi madudu ya mtu kwa kigezo cha "mapungufu ya kila binadamu." Hell no. The dude needs improvement in some areas, period. Hatujajua ethos za PR. Hakuna cha human weaknesses kwenye competitive professions!
Maximo aongezewa mkataba Stars

na Wilbert Molandi
Tanzania Daima
March 19, 2009

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limerefusha mkataba wa kocha mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo wa kuinoa timu hiyo.

Rais wa TFF, Leodegar Chilla Tenga, alisema jana ya kwamba, Maximo ameongezewa muda wa miaka miwili, lakini kocha huyo kwa hiari yake ameomba apewe mwaka mmoja kwanza.

Kwa mujibu wa Tenga, Maximo ameomba kipindi hicho cha mwaka mmoja kulingana na programu yake kabla ya kuongeza mwaka wa pili.

Tenga alisema, makubaliano yaliyopo ni kwamba, Maximo ataendelea na mwaka mwingine wa pili kama Stars itapata tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini au Mataifa ya Afrika nchini Angola mwaka 2010.

Tangu Maximo aanze kuinoa Stars Agosti 19, mwaka 2006, Stars imecheza mechi 26 za ushindani na kirafiki na kushinda tisa, sare 11 na kufungwa sita.

Tenga alisema, kama upungufu kwa Maximo, utakuwa ni wa kawaida kama ilivyo kwa binadamu yeyote, hivyo kwa kipindi chote ambacho kocha huyo amekuwa na Stars, amekuwa mtu muhimu katika kujenga kikosi bora.

Maximo.jpg
Pep talk ya Maximo sijui ni lugha gani. Daily News kuna video
interview, Kiingereza chake ni kama changu, sijui cha machizi!​
 
Binafsi naungana na TFF kutaka kumuongezea muda mrefu kiasi kinachowezekana, unajua unaweza kuwa na kitu cha thamani mkononi na usijue kama unakitu cha thamani hivyo. Kipindi fulani nilitamani Maximo akatae kuongeza mkataba, halafu baada ya mwaka mmoja kupita nafikiri wote tungeona ni jinsi gani huyu bwana ni msaada kwa soka letu. Kwa level yetu kumpata huyu ni kama bahati tu, hebu nenda bbc sports kuna habari juu ya Maximo kuongeza mkataba na habari yake ndogo tu. Halafu uone kwa kutafuta kwetu kocha tungeweza kumpata wa level hii?, mimi namuheshimu sana kwa kujishusha kiasi hiki.
 
Kwa level yetu kumpata huyu ni kama bahati tu, hebu nenda bbc sports kuna habari juu ya Maximo kuongeza mkataba na habari yake ndogo tu. Halafu uone kwa kutafuta kwetu kocha tungeweza kumpata wa level hii?, mimi namuheshimu sana kwa kujishusha kiasi hiki.

Kwani level yetu ni ipi na level ya Maximo ni ipi?
 
Mwenyewe alitaka aondoke nyinyi mmeng'ang'ania kumbakisha shida yenu avurunde ili apate kuondoka kwa kumfukuza, keshaona wachezaji wa tz ni vifuu, hawafundishiki wala hawajitumi wanapende kusifiwa tu na kujipachika majina makubwa yanayozidi uwezo wao, kama TFF wapo serious wampe Maximo wachezaji siyo majina ya watu tu wanao piga mpira
 
Ndio maana nimeonyesha ni wapi uangalie, ukiona tuna level hiyo fine!. Ila watu hawachezi mpira kwa maneno, maneno yetu ni mengi na tunakwepa ukweli.

Sasa kwa nini hakwenda kufundisha huko kwenye level kubwa, vipi hakupata dili? Au asingependa kulipwa zaidi huko kwenye level yake?

World class coach angeacha kufundisha ligi kubwa aje kwenye hiyo uliyo iita "level yetu"?

Huyu Maximo sio kihivyo, hata akihojiwa utamjua. The other day kawalaumu makocha wa Tanzania kwenye vyombo vya habari eti wako "ashamed" of him, ndo maana hawaendi kuongea nae. Angekuwa a real professional asinge take a shot at local coaches. Wako ashamed, ndio nini hicho, kwani kawakopa hela?

Tanzania kumpata Maximo "ni bahati tu," kwani halipwi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom