Tunatoa huduma ya e-Learning/Online Learning kwa shule za msingi, secondary na vyuo mbalimbali nchini Tanzania

TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
812
969
Kwa nyakati kama hizi ambapo janga la COVID-19 limeikumba dunia, shule na vyuo mbalimbali havina budi kubuni njia mbadala za kutoa elimu kwa wanafunzi wao. Hata hivyo taasisi mbalimbali za elimu duniani tayari zilishapiga hatua kubwa katika maendeleo ya kutoa elimu kwa njia ya mtandao - - e-learning/online learning au distance learning.

Sisi TANZANIA STUDENTS AND SCHOLARS FOUNDATION LIMITED tunatoa huduma ya kutengenezea taasisi mbalimbali za elimu nchini Tanzania - shule za msingi/sekondari, vyuo vya kawaida na vyuo vikuu, mfumo ambao utaziwezesha taasisi hizo kufundisha wanafunzi wao bila shida. Mfumo unazingatia "limited internet bandwidth, speed, and infrastructure" kwa kuangalia hali halisi ya ukuaji wa teknolojia hiyo hapa nchini.

Waalimu wa taasisi husika wataweza kufundisha wanafunzi wao kwa kutumia mjumuisho wa "electronic text, graphics, audio, videos, codes na hata live-streaming." Sio tu tunatengeneza mfumo, bali pia tunatoa "training" inayojitosheleza kwa 100% kwa taasisi husika namna ya kutumia mfumo huo. Sisi tutaendelea kusimamia, kurekebisha na kuupgrade mfumo kwa muda wote ambapo taasisi husika itakuwa ikiutumia. Kwa maana hiyo taasisi husika haihitaji kuwa na wasiwasi juu ya namna ya kushughulika na mfumo huo. Tunataka taasisi zijihusishe na kutoa elimu, technicalities zote ni kazi yetu.

Kwa taasisi au mtu ambaye anahitaji kuwa na mfumo wa kufundishia, awasiliane nasi kwa email address hii (right click ili ucopy address) au atume message inbox, au aulize maswali yake hapa. Kwa wale ambao wataonyesha nia tutawatumia andiko linaloeleza (complete proposal) jinsi ambavyo mfumo unafanya kazi.

Angalia baadhi ya mambo ambayo wanafunzi na waalimu wataweza kufanya kwa kutumia mfumo huo wa kufundishia:

1) Wizara ya Elimu imeshindwa kuandaa audio na video ya vipindi vya masomo mbalimbali? - JamiiForums

2) Wizara ya Elimu imeshindwa kuandaa audio na video ya vipindi vya masomo mbalimbali? - JamiiForums

Pamoja na kutoa huduma ya mfumo wa kufundisha kwa njia ya mtandao, huduma hiyo inaambatana na huduma zingine, baadhi yake ni:

- Mfumo wa kumanage habari za wafanyakazi/staff: Need Human Resource Information/Management System (HRIS/HRMS)?
- Mfumo wa application kwa ajili ya wanafunzi kujiunga na shule/chuo: College Online Application System (COAS)
- Mfumo wa kusajili habari za wanafunzi za kiakademia: Academic Registration Information System (ARIS)

TANZANIA STUDENTS AND SCHOLARS FOUNDATION LIMITED - - A creative journey towards infinite possibilities!, tuna uzoefu mkubwa kuhusiana na mifumo ya kutoa elimu kwa njia ya mtandao tangu 2012. Kwa maana hiyo, tupo pamoja na wewe bega kwa bega kuhakikisha unaendelea kutoa elimu kama kawaida hata katika wakati huu wa janga la COVID-19.

tf.
 
Back
Top Bottom