Hata mimi huwa nashangaa. Kwa mtu anayefanya biashara kihalali hawezi kupata faida kwa kutoa huduma kwa bei hii. Ukichukua tu bei ya rim la karatasi 400 ni wastani wa elfu 900 au chini kidogo. Ina maana karatasi peke yake ni shilingi wastani wa sh. 22. Bado wino, umeme, kodi ya pango, mshahara, kodi t.r.a, na vingine vingi. Wengi wa hawa watu wanatumia malighafi za magendo nadhani. Kuna haja ya jukwaa hili kuwaelimisha watu mbinu za kushindana. Mbinu ya kushusha bei ni mbinu hatari sana ya kukabiliana na ushindani. Hebu fikiria wewe unatoa kwa sh 25. Wateja wanamiminika. Baada ya muda jirani zako nao kwa kuona wanakosa wateja nao wakashusha bei ikafanana na ya kwako au chini zaidi. wale wateja waliokuwa wanamiminika kwako wanapungua wanaenda na kwa wenzio. matokeo yake wote mtapata hasira au kuishia kuchumia tumbo maana mtagawana wateja na mtapata kidogo.