Tunatengeneza aina mpya ya upinzani

Tunatengeneza aina mpya ya upinzani

Mkuu, uliona mbali sana. Uliandika uzi huu mwezi February, lkn karibu yote uliyonena ndo yametokea.

Huko ccm kuna watu ambao wanadhaniwa kuwa wanataaluma ya siasa, akina Bashiru Ally, lkn wamefanya mambo ya ajabu sana.

Nadhani watakuwa wanajua kuwa wananchi wengi ni wapinzani mioyoni na ndo sabb wakafanya rafu nyingi kwny uchaguzi, maana walijua fika bila hivyo hawashindi.

Matendo waliyofanya kwny uchaguzi mkuu mwaka huu, sijui Kama wanafahamu yalivyoathiri nafasi yao ktk mioyo ya wananchi walio wengi
Kweli kabisa mkuu, ni kwamba wamezidi kuimarisha upinzani kuliko kuudhoofisha. Wamechukua wrong approach ambayo itazidi kukiangamiza chama badala ya kukijenga.

Kosa jingine ni kuruhusu chama kimjenge mtu na si taasisi. Akipatikana na dosari mtu huyu maana yake anguko lake ni anguko la taasisi nzima.
 
Mkuu usizunguke sana, tatizo la siasa za nchi yetu kwa sasa ni rais Magufuli, yeye ndiye asiyeweza siasa za ushindani hivyo anaamini akijenga miradi kadhaa na kuitangaza, basi watu wote watamkubali yeye au chama chake cha ccm.

Kwakuwa ana madaraka makubwa anayoyapata kupitia katiba outdated, basi anayatumia madaraka hayo kufurahisha nafsi yake, na kulazimisha atakacho yeye na genge lake na wanaofaidika na madaraka yake.

Hata wale wanaojua fika afanyacho sio sawa wako kimya kwa hofu. Ukitaka kujua Magufuli analazimsha kurudisha watu usingizini huku wakiwa wameshaamka, angalia idadi ya watu wanaoenda kujiandikisha kupiga kura ilivyo ndogo.

Nakuhakikishia atakapotoka madarakani rais Magufuli kila kitu kitabadilika na katiba mpya itapatikana. Kwa sasa watu washikilie msimamo wa tume huru ya uchaguzi, ambayo ni lazima ipatikane au uchunguzi uwe sio halali. Kutoka hapo kila kitu kitabadilika.
Mkuu bado unao huu mtazamo wako?
 
Back
Top Bottom