Tunatengeneza aina mpya ya upinzani

Tunatengeneza aina mpya ya upinzani

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,842
Reaction score
10,765
Baada ya kuona mfumo wa vyama vingi unanyima uhuru wa wenye dola kujiamria mambo watakavyo wenyewe, tumebuni mkakati unao kuhakikisha kuwa ifikapo mwishoni mwa 2020 Tanzania haitakuwa na vyama vya upinzani vyenye nguvu.

Kwamba wakati huo majukwaa yote kipindi cha uchaguzi yataimba sifa njema kuelezea mambo makubwa na ya kushangaza yaliyofanywa na watawala.

Hakutakuwa na wenye nguvu ya kuonyesha upande wa pili wa shilingi kitu ambacho miaka yote tangu kuanza kwa harakati za vyama vingi kimekuwa kikitumika kama dira ya chama tawala pale kinapoingia madarakani.

Sasa ingawa jambo hili laweza kuonekana ni jema machoni pa wanaoendesha pokea pokea, lakini kimsingi maneno ya Trump yanapata maana kubwa.

Rais huyu mbabe na mzalendo wa kweli kwa taifa lake anajipambanua kama NABII wa kisiasa wa kizazi chetu, hasa pale anapoongelea nchi zinazoongozwa na watu weusi.

Hili laweza kuwa ni kosa ambalo tutakuja kulijutia siku zijazo. Kwa nini nasema hivi?

Upinzani wa kweli hujengwa kwa wananchi, SIO WANASIASA. Wanasiasa ni kama wachezaji wa Simba na Yanga ambao hufanya majukumu yao kwa kutarajia ujira.

Sasa pale maslahi ya mwajiri yanapokuwa madogo kulinganisha na mwajiri mwingine, ndipo huamua kuhamia upande wa pili na kumtosa mwajiri wa kwanza.

LAKINI NI WAPENZI NA WANACHAMA WANGAPI AMBAO HUHAMA PAMOJA NA MCHEZAJI? Ndivyo ilivyo kwa wanasiasa. Jana alikuwa CCM, leo anahamia CHADEMA.

Jana alikuwa CUF leo anahamia ACT Wazalendo. Lakini wanachama walio wengi, japo wanapatwa na majonzi mioyo yao itabaki kuwa huko huko walikolelewa.

Ni wanasiasa wachache sana ambao waliweza kuhama na mashabiki wao kwenda chama kingine, mfano mh. Lowassa alipohamia CHADEMA.

Lakini nini kilitokea aliporudi alikotoka? Watu walishabaini siasa chafu zinazoendelea, hivyo hawakuwa na shamrashamra na bashasha kama ilivyokuwa hapo awali.

Ndivyo ilivyokiwa kwa Mh. Sumaye wakati akihamia upinzani, lakini haikuwa habari alipoamua kurejea alikokulia. Watanzania hawakutaka kushiriki dhambi ya ujinga wa kuwa shabiki wa mtu, wawe wanavutwa na upepo huku na kule.

Hayo yote ni dalili kwamba watu wameanza kuamka kwenye mambo ya kisiasa na hawana muda tena wa kusimamia siasa chafu.

Kama huelewi nasema nini angalau tazama jinsi zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa lilivyofanyika. Siku ya uchaguzi haikuwa na tofauti na siku nyinginezo kwa sababu watu hawakujishughulisha na zoezi hilo.

Walipima kwa vichwa vyao wakaona ya kuwa kinachoendelea ni ubatili.

Sasa baada ya zoezi la kuua upinzani kama ilivyoahidiwa kukamilika, kitakachokuwa kimekufa si upinzani bali ni wanasiasa wa upinzani.

Nazungumzia wale watu wanaosimama mbele ya jamii kama viongozi wao, wasemaji wao, watu wanaowaleta pamoja. Upinzani halisi utaendelea kuwepo, tena zoezi hili litauimarisha zaidi mioyoni mwa watu.

Ni ajabu kuwa hata wale waliokuwa wakijinasibisha kama sehemu ya chama tawala wanahoji kinachoendelea. Maana yake wanaonyesha kutoridhishwa na yanayotukia, kitu ambacho kinawafanya wa-sympasize na upinzani, waanze pia kujifananisha nao.

Kwa sababu kazi ya viongozi wa upinzani, mfano wabunge ni kuwasemea wenye mawazo mbadala, kuikosoa serikali, kuonyesha mapungufu na maeneo yaliyosahahulika n.k. wakiondolewa ama kunyimwa nguvu, wananchi waliowakilishwa na hawa watakosa jukwaa la kusemea madukuduku yao.

Watajikuta wakijaza chuki mioyoni mwao pasipo nafasi ya kupumua. Tusijidanganye, pale wabunge wa upinzani walipojenga hoja zao bungeni ziliweza kuwafurahisha wenye mtazamo huo na hivyo kuwatuliza mioyo, hata kama hazikufanyiwa kazi.

Ni jambo la kawaida kwa mwanadamu kutafuta sehemu ya kusemea kero zake ili apate pumziko la nafsi. Sasa mzazi akimnyima mwanae uhuru wa kujieleza ama kutoa kero zake, kifuatacho ni ama kujinyonga, ama kuasi mamlaka yake.

Hii ndio aina ya siasa tunayoitengeneza. Tuwe wakweli tu, wakati wa Mwalimu Nyerere watu walikuwa hawajaelimika kiasi cha kupima mambo, lakini nyakati hizi mambo ni tofauti.

Huwezi kuwanyamazisha watu kwa kuwaondolea platform ya kutolea dukuduku zao. Ni heri kuwapa uhuru wa kusema wakatuliza nafsi kuliko kuchukizwa na maneno yao na hivyo kuwataka wafunge midomo na kukaa kimya!

Ni mtazamo tu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Michezo ya CCM kututengenezea wapinzani sijui wananchi mtakuja kushtuka lini

Ona sasa hivi wana vyo symphathize na kina membe au kinana

Yaaani ni sawa na future generation ianze ku sympathize na kina bashiru

ajabu kweli kweli vijana wa nchi hii
 
Mkuu usizunguke sana, tatizo la siasa za nchi yetu kwa sasa ni rais Magufuli, yeye ndiye asiyeweza siasa za ushindani hivyo anaamini akijenga miradi kadhaa na kuitangaza, basi watu wote watamkubali yeye au chama chake cha ccm.

Kwakuwa ana madaraka makubwa anayoyapata kupitia katiba outdated, basi anayatumia madaraka hayo kufurahisha nafsi yake, na kulazimisha atakacho yeye na genge lake na wanaofaidika na madaraka yake.

Hata wale wanaojua fika afanyacho sio sawa wako kimya kwa hofu. Ukitaka kujua Magufuli analazimsha kurudisha watu usingizini huku wakiwa wameshaamka, angalia idadi ya watu wanaoenda kujiandikisha kupiga kura ilivyo ndogo.

Nakuhakikishia atakapotoka madarakani rais Magufuli kila kitu kitabadilika na katiba mpya itapatikana. Kwa sasa watu washikilie msimamo wa tume huru ya uchaguzi, ambayo ni lazima ipatikane au uchunguzi uwe sio halali. Kutoka hapo kila kitu kitabadilika.
 
Je, haki ya kuto kuishi kutokana na nguvu kubwa ya watu wasiojulikana ni sawa? je nikweli watu wasiojulikana wameshindikana ama hawatakiwi wajulikane
 
Upinzani wa kweli hujengwa kwa wananchi, SIO WANASIASA. Wanasiasa ni kama wachezaji wa Simba na Yanga ambao hufanya majukumu yao kwa kutarajia ujira.

Huwezi kuwanyamazisha watu kwa kuwaondolea platform ya kutolea dukuduku zao. Ni heri kuwapa uhuru wa kusema wakatuliza nafsi kuliko kuchukizwa na maneno yao na hivyo kuwataka wafunge midomo na kukaa kimya!

Ni mtazamo tu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Naunga mkono hoja
P
 
Upinzani wababaishaji. Twende na Chama kinachojielewa
Kwa CCM ndo wanao jielewa?. To hell no!, Wako vile kwakuwa wana dola, wanacho fanya chaweza kufanywa na kundi lolote au mtu yeyote mwenye mamlaka ya dola.
 
Napita tuu
IMG-20200216-WA0058.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom