Jana nilishuhudia mchezo baina ya Taifa Stars dhidi ya Lesotho kupitia luninga ya TBC kusema ukweli kiwango cha Tanzania Stars kilikuwa cha chini sana kulinganisha na timu pinzani. Jana hata timu ya Mbao kwa kiwango kile ingeweza kuifunga Taifa Stars. Nashauri tuwekeze hasa kwenye Soka tusiwe tunapata aibu kama ile ya jana. Kweli timu ya Lesotho itoke sare na Taifa Stars?.