Tunatakiwa tuwe wastaarabu tunaposhuhudia mapambano ya mpira uwanja wa Taifa

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Leo kupitia kipindi cha michezo asubuhi sikuamini masikio yangu niliposikia kuwa panapokuwa na mashindano makubwa ya mpira mfano Yanga dhidi ya Simba, Simba dhidi ya Azam, Azam dhidi ya Yanga n.k. wastani wa viti 500-800 huharibiwa na watzamaji katika mechi moja.

Mbali na uharibifu wa viti hivyo sasa ukienda kwenye vyoo ndo utakuta maajabu. Taarifa ilisema kuwa wastani wa gharama ya kiti kimoja ni Ths.60,000. Ukichukulia viti 500x60,000= Tshs.30,000,000(Millioni thelathini).

Utafiti umefanyika kuwa ni nini chanzo cha uharibifu huu?. Matokeo ya utafiti umesema kuwa watazamaji tunakosa ustaarabu tunapokuwa mpirani. Naomba niulize swali?. Hivi mtu mzima unaweza ukayafanya hayo nyumbani kwako?.

Kuaamua kuharibu viti vya nyumbani na kukojolea/kunya kwenye makochi?. Niliwahi kuhudhuria mechi moja kati ya Yanga dhidi ya Simba uwanja wa Taifa niliyoyakuta chooni sitayasahau maishani mwangu. Ndugu zangu tunatakiwa tuwe WASTAARABU pindi tunapokuwa tukishuhudia mapambano makubwa ya mpira. Uharibifu wa kitu chochote ina maana unateketeza hela ya mlipa kodi.
 
Baadhi ya watu sio wastaarabu in nature, unakuta mtu Mfano ameingia choo cha public na kina maji kabisa ya kuflash ila anamaliza haja anatoka bila kujali atakaekuja nyuma yake
 
Back
Top Bottom