Gerad2008
JF-Expert Member
- Jun 9, 2009
- 583
- 284
Makamba asiwaone watanzania watoto wadogo. Ni kweli kwamba tangu uhuru mihimili hii mitatu yaani Bunge ,Serikali na Mahakama hazijawahi ongozwa na mwana mama. Kwa lengo jema hilohilo aliloonyesha kuwa wakati umefika kwa bunge kuongozwa na mwanamke basi na Mwaka 2015 wamteue mgombea urais wa CCM mwanamke. Kama wataona huko ni mbali basi watupatiea basi hata Waziri Mkuu mwanamke ili kuonyesha wanajali sana usawa wa kijinsia.
Sababu nyepesi alizotoa Makamba ni janja ya CCM kumpitisha aliyependekezwa na wenye nchi yaani MAFISADI kwa lengo la kulinda masalahi ya wenye Chama kwa sasa yaani MAFISADI tena. Habari kwamba Anna Makinda alishauriwa na MAFISADI kuchukua fomu kumtoa Bosi wake ziliandikwa kabla ya tukio la Jana na hii inanifanya niamini kwamba kuna mpango mahsusi ulioandaliwa na MAFISADI kutwaa nchi yetu.
Njaa za viongozi wa CCM ambao Elimu zao zinatia shaka ndizo zinataka kuifikisha nchi yetu nzuri pabaya. Nchi ipo mikononi mwa walevi wa madaraka, wezi, na waporaji ambao wanataka kutunyonya hadi tone la mwisho.
Kutugeresha watanzania eti wakati umefika wa kuwa na spika mwanamke ni uchuro ambao kwetu sisi wenye kuona mbali tunajua ni yale yale ya kumwona mtanzania Mbumbumbu na mazezeta. Hili goli hutufungi mgosi tumeliona na kulidaka na tunarudia kusema"WATANZANIA HATUDANGANYIKI TENA". Hatua zote mnazopiga za kutaka kutufanyia ubaradhuli na ufedhuli kwa sababu mtu mnataka kukata ya tamaa zenu mbaya za mali tumeziona na tuko macho tukizifuatilia. Tumeanza asubuhi hii 2010 na ikifika jioni 2015, tutakuwa tumewazunguka na hamtakwenda mahali lazima tuwabwage Mafisadi na chama chenu cha kifisadi ambacho kamwe hakimtaki yeyote aliye safi bali wachafuzi wa hali ya hewa ya uchumi wa nchi yetu.
Mnachofanya sasa hivi ni kuboresha hali ya umaskini wa mtanzania kwa kunyanganya hata ile rasilimali kidogo aliyopewa na muumba wetu kupitia mikataba mibovu ya madini, kuuza mali asili ya nchi yetu kwa waarabu kwa lugha inayonuka ya uwekezaji. Laana mnayopata kutokana na machozi ya watanzania waliohamishwa maeneo waliyozaliwa tangu mababu kwa kisingizio cha kupisha wawekezaji zitakuwa juu ya watoto wenu na vizazi vyenu. Mtatafuta wala hamtaridhika na mtakula hamtashiba na mwisho wa siku tunairudisha nchi mikononi mwa watanzania wenye nia na dhamira njema na nchi yao.
Watanzania tujipange kwa mwaka 2015, tuhakikishe tumemaliza uzia kwa mustakabali wa watanzania woote.