Tunatafuta wafanyakazi

Tunatafuta wafanyakazi

Kweli utaratibu mnaotumia una hali ya kutokuwa na uaminifu, maana nimetuma binti na kaka wakaenda huko walipo hawa watu wakaambiwa watoe 3,000 za form, wametoa hizo hela na wakawaona hao waajiri matokeo yake wanaambiwa kazi zipo lakini mnatakiwa mtoe hela kama 70,000, na mwingine kaambiwa 80,000/ ndipo waunganishwe na waajiri. Jamani hivi kweli mtu hajapata kazi atapata wapi hiyo hela? Na kisha mfano mtu anatoa hiyo hela akienda kwa mwajiri akakuta kazi hakuna je atarudishiwa hela na dalali?
Naomba muache tabia hii ya kuchukuwa kila anayekwenda hapo kumwambia atoe hela 3000/= si vyema na mtu anatoka hajapata kazi na form ni photocopy tu?


Sio kweli ,nakuomba ufikiri zaidi kusema uongo hapa hakusaidii kitu zaidi ya kuonyesha ujinga na uwezo finyu wa kufikiri

Tafadhali kama una kazi waache wanaosaka wasake ajira kwa amani usiwachanganye watu kwa ongo zako zisizo na maana
 
kumbe ndo hawa wametoa vipeperushi kibao,mwishoni eti ,kuna fom za kujaza,unailipia hyo form sh 3000,km sio wiz huo ni nn?
 
wizi mtupu hawa baadae wata request hela za interviw na training kuweni makini
 
information za kutosha basi jamani,kama office location, qualification nk
 
assistens naye anatakiwa.....hakuna kazi hapo usituchosheeee.....nna uhakika una ndugu mia 5 hawana kazi kama kazi haina hata vigezo si uwape ?????potelea mbaliiiiii:yell:
 
tumechoshwa na hii tabia ya watu kutumia matatizo ya wavuja jasho ili kujinufaisha,hii iko au mpaka tu dili nao ndo waache?
 
Acheni kuwachukulia wateja 3,000/= ati ya form. Form moja mmeitoa photocopy kibao kisha,watu mna wa charge tshs. 3,000/ awe amepata kazi au kashindwa kutoa hela ya udalali, ni dhambi kwanini msimhoji mtu na kumpa maelezo kwamba kuna makampuni wanatafuta watu na mnapotaja 80,000 kama mtu hana basi asiwe amepoteza na hela yake ya form- jirekebisheni tabia hii mbaya mnachuma 3,000 kwa watu wasiokuwa na ajira jamani hali mbaya...kuweni na huruma....
 
Tatizo nikwamba hakupita shule

Kumbe na wewe umeling'amua hili, maana hata kuandika hajui. nimesoma post nikaptwa na kichefufu.

Lenjentz kama uajiriwa basi boss wako kanunua mbuzi kny gunia.
 
Udereva wa kiwango gani, A,B,C au D? Kuna kijana wangu mtaani anatafuta kazi ya udereva ana CLASS D.
 
Kumbe na wewe umeling'amua hili, maana hata kuandika hajui. nimesoma post nikaptwa na kichefufu.

Lenjentz kama uajiriwa basi boss wako kanunua mbuzi kny gunia.


Na wewe umeandika nini sasa hongera kwa kutuonyesha Uchi wa akili yako,yako maneno ningekuambia lakini kwa kuwa uu mjinga endelea na ujinga wako
 
Back
Top Bottom