Tunatafuta social investors

Tunatafuta social investors

Tujikomboe Finance

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
212
Reaction score
81
Wapendwa,
Tunatafuta mtu au taasisi ya kuikopesha kampuni yetu fedha kwa ajli ya kutoa mikopo kwa kuzingatia ukuaji na ulengwa wa jamii (Social Performance). Tuna effective demand kubwa sana lakini hatuwezi kuitimiza kwa vile hatuna mtaji wa kutosha. Tumejaribu kwenda kwa benki masharti wanayotupa ni kama mbingu na ahera. Kiufupi benki za Tanzania hazitii moyo ubunifu wanapenda vitu ambavyo vimekuwepo tayari muda mrefu sana na vyenye majina makubwa ambavyo vingi wakati ule vilianzishwa kwa fedha za bure za kutoka kwa wafadhili.

Taasisi yetu inatoa mikopo ya:
  1. Biashara
  2. Ujenzi wa nyumba/ uboreshaji wa nyumba
  3. Mikopo ya kuchakata hati za nyumba/viwanja
  4. Ununuzi wa viwanja vya kujenga makazi
  5. Ada ya elimu

Mkopo tunaohitaji ni kati ya 85,000,000- 100,000,000 kwa kuanzia (kujenga uaminifu) na tupo tayari kulipa faida juu ya vile mtu angeweka hiyo fedha benki kama ni Savings account au FD.

Kama wewe huna tunaomba msaada wa contacts ndani na nje ya nchi ya ''social investors''
 
Jaribu kwenda WAT saccos kinondoni kwa mama SIWALE mnaweza pata mwanga na ushauri zaidi, huwa wanashughulika na hayo mambo
 
Back
Top Bottom