Tunapotoa misamaha huwa hatutoi kwa fulani na fulani, linaangaliwa kundi!

kwa moyo wa huruma nampongeza rais kuwaweka huru hawa jamaa (jk sijui kajisikiaje hahaaaaaaaa we saliiiiima)

japokuwa ametumia mabavu na kusigina nguvu ya mahakama, katumia vibaya ofiis yake

kwa kawaida ya tanzania hakuna atakaemuuliza wala kuleta vyokofyoko. yamepita wacha maisha yaendeleeeeeee
Una uhakika ni jk?
 
Bahati mbaya suala la babu Seya lilichukuliwa kisiasa hasa kujipatia umaarufu kisiasa lakini ukweli uliopo ni kuwa Rais ana mamlaka ya kusamehe mfungwa yeyote anayetumikia kifungo gerezani ieleweke ni kumsamehe kutumikia adhabu gerezani na siyo kufutia kosa Lowasa aliahidi kutoa msamaha kwa Babu Seya endapo angeshinda urais hiyo ilikuwa njia ya kujipatia umaarufu kisiasa leo Rais aliyepo madarakani katumia mamlaka yake kuwasamehe babu Seya hiyo pia ni kujipatia umaarufu kisiasa
 
Nijikite moja kwa moja kwenye msamaha wa Babu Seya na Nguza

Hapa naona kama rais Magufuli amefanya siasa kutokana na ukweli kuwa amepingana na hukumu waliyopewa hawa watu na ushahidi uliothibitisha makosa yao.Kama sivyo basi ipo vita ambayo ameamua kuianzisha kwa kusudi fulani ikiwa ni pamoja na kunusa kuwa huenda hukumu aliyopewa Babu Seya na mwanae haikuwa sahihi?

Ikiwa rais anapaswa kutoa msamaha kwa wafungwa. Huwa hasemi ninawasamehe fulani na fulani kama alivyofanya kwa babu Seya na mwanae tofauti na pale alipoanza mfano kusamehe wale wenye miaka 85 ns kuendelea kwa maana kuwa lile kundi lote limenufaika na msamaha tofauti na alivyofanya kwa Babu Seya na mwanae maana hawa pekee ndiyo walionufaika na msamaha na siyo kundi fulani.

Hapa rais alitakiwa ama atoe msaha kwa wafungwa wote waliowahi kuhukumiwa kutokana na kupatikana na hatia ya kulawiti ili kuleta maana.Hapa rais kwa mara nyingine ameteleza na ategemee kuzuka kwa mjadala mkubwa juu ya hili. Aidha tayari rufaa zote zilishakatwa hivyo hukumu ilikuwa imefikia tamati! Kwanini uwe ni msamaha wa kubagua? Vipi kwa hawa "walawiti" wengine?
Uko sahihi kabisa mkuu. Hapo hata kama aliwakusudia hao angesema wafungwa wote wa kulawiti waliotumikia vifungo vyao labda kwa miaka 15 na kuendelea hivyo angekuwa anazungumzia kundi badala ya watu wawili. Je wale waliofungwa wakati mmoja na Nguza wanajisikiaje kuona wenzao wanatoka nao wao kubaki wakati kosa ni moja na miaka waliyokaa gerezani ni sawa??
 
Hapa umenigisa raisi inawezekana kafanya uchunguzi wa kutosha kagundua ni kesi feki maana waliohukumu kesi wapo na waliokuwa wanapeleleza kesi wapo
Hapa hoja si kesi kuwa feki au lah...hapa hoja ni msamaha wa Rais..Rais anayo mamlaka ya kumsamehe mtu yeyote yule hata kama alikutwa na hatia mahakamani na bila masharti yeyote au kwa masharti.....
 
Uko sahihi kabisa mkuu. Hapo hata kama aliwakusudia hao angesema wafungwa wote wa kulawiti waliotumikia vifungo vyao labda kwa miaka 15 na kuendelea hivyo angekuwa anazungumzia kundi badala ya watu wawili. Je wale waliofungwa wakati mmoja na Nguza wanajisikiaje kuona wenzao wanatoka nao wao kubaki wakati kosa ni moja na miaka waliyokaa gerezani ni sawa??
Baba seya mgogoro wake unaanzia huko kwao Congo, wala hakuna uhusiano na suala la ubakaji

kwa lugha nyingine jamaa alikuwa political prisoner, hizo nyingine ni porojo tu.

Issue ya kulawiti ilikuwa ni kum blackmail tu.
 
Naunga mkono hoja,mimi nimechukizwa,kufadhaika na kukerwa na msamaha huu.Najua sina jinsi ya kupinga hili lakini Raisi wangu amekosea ila naye ni binadamu.Najiuliza tu mwaka huo aliofungwa babu seya na mwanawe je hakukuwa na wafungwa wengine wenye kosa kama la hawa wakongo?
 
Nijikite moja kwa moja kwenye msamaha wa Babu Seya na Nguza

Hapa naona kama rais Magufuli amefanya siasa kutokana na ukweli kuwa amepingana na hukumu waliyopewa hawa watu na ushahidi uliothibitisha makosa yao.Kama sivyo basi ipo vita ambayo ameamua kuianzisha kwa kusudi fulani ikiwa ni pamoja na kunusa kuwa huenda hukumu aliyopewa Babu Seya na mwanae haikuwa sahihi?

Ikiwa rais anapaswa kutoa msamaha kwa wafungwa. Huwa hasemi ninawasamehe fulani na fulani kama alivyofanya kwa babu Seya na mwanae tofauti na pale alipoanza mfano kusamehe wale wenye miaka 85 ns kuendelea kwa maana kuwa lile kundi lote limenufaika na msamaha tofauti na alivyofanya kwa Babu Seya na mwanae maana hawa pekee ndiyo walionufaika na msamaha na siyo kundi fulani.

Hapa rais alitakiwa ama atoe msaha kwa wafungwa wote waliowahi kuhukumiwa kutokana na kupatikana na hatia ya kulawiti ili kuleta maana.Hapa rais kwa mara nyingine ameteleza na ategemee kuzuka kwa mjadala mkubwa juu ya hili. Aidha tayari rufaa zote zilishakatwa hivyo hukumu ilikuwa imefikia tamati! Kwanini uwe ni msamaha wa kubagua? Vipi kwa hawa "walawiti" wengine?
You're better than this, Rais ametowa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 8000, wafungwa maarufu ni Babu Seya na mwanaye na yule aliyehukumiwa kunyongwa anaitwa Matonya.

Nadhani ni vyema ukahoji ni kwa nini wengine wakifa wanaitwa marehemu na wengine wanaitwa hayati.

Hoja za kitoto hizi. Mkitaka kumbananisha Magufuli siyo kwa hoja dhaifu kama hizi. Too low.
 
Uko sahihi kabisa mkuu. Hapo hata kama aliwakusudia hao angesema wafungwa wote wa kulawiti waliotumikia vifungo vyao labda kwa miaka 15 na kuendelea hivyo angekuwa anazungumzia kundi badala ya watu wawili. Je wale waliofungwa wakati mmoja na Nguza wanajisikiaje kuona wenzao wanatoka nao wao kubaki wakati kosa ni moja na miaka waliyokaa gerezani ni sawa??
Wanavyo jisikia wajisikie lakini Rais anayo mamlaka ya kumsamehe mtu yeyote yule bila kuzingatia kundi au mtu mmoja.... kwenye kutoa msamaha kwa Rais hakuna masharti yeyote ya jinsi ya kutoa msamaha.... hata kama alikutwa na hatia mahakamani Rais anayo mamlaka ya kumsamehe...
 
You're better than this, Rais ametowa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 8000, wafungwa maarufu ni Babu Seya na mwanaye na yule aliyehukumiwa kunyongwa anaitwa Matonya.

Nadhani ni vyema ukahoji ni kwa nini wengine wakifa wanaitwa marehemu na wengine wanaitwa hayati.

Hoja za kitoto hizi. Mkitaka kumbananisha Magufuli siyo kwa hoja dhaifu kama hizi. Too low.
Mkuu elewa kuwa kwenye wafungwa wote aliotoa msamaha rais katoa kwa makundi maalum (wengi wao) Tatizo pale kwa Babu Seya na Papii katoa kwa wao pekee kwenye hilo kundi lao! Usipayuke bila kufanya utafiti na mpaka naandika humu nimejiridhisha vya kutosha.Nguza na Papii wamesamehewa wao kama wao na ndipo mimi ninapohoji. Kama angewaweka kwenye kundi fulani nisingehoji. Acha kujifanya unajua!
 
Back
Top Bottom