Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 57,582
- 96,521
G Sam, wewe ndio unapayuka na huenda wewe ndio hujui lolote.Mkuu elewa kuwa kwenye wafungwa wote aliotoa msamaha rais katoa kwa makundi maalum (wengi wao) Tatizo pale kwa Babu Seya na Papii katoa kwa wao pekee kwenye hilo kundi lao! Usipayuke bila kufanya utafiti na mpaka naandika humu nimejiridhisha vya kutosha.Nguza na Papii wamesamehewa wao kama wao na ndipo mimi ninapohoji. Kama angewaweka kwenye kundi fulani nisingehoji. Acha kujifanya unajua!
Numero uno, wewe huwezi kumpangia Rais do and don'ts, ni katiba ndio inampangia.
Aliyoyafanya leo yote ni kwa mujibu wa katiba na orodha ya wanufaika ameikabidhi kwa Waziri mkuu kwamba asimamie hili zoezi asipenyezwe hasiyehusika wala asikatwe jina mnufaika yeyote yule.
Kuwataja kwa majina Babu Seya na Papii Kocha hao ni wafungwa wenye public interest that's it hakutaka muwaone uraiani mkaanza hadithi kibao, yeye ameweka wazi mwenyewe, lakini alikuwa na uwezo wa kuwaweka kwenye list ya msamaha bila kuwatangaza., ila kitendo cha kuwatangaza amekata mzizi wa fitina ili kesho ukiwaona Sinza wanakunywa mtori pale La Chalz msije hapa JF kuanzisha thread ambazo hazina kichwa wala miguu.