Tunaposema Mbowe siyo gaidi, tunamaanisha hivi

Kumekuwa na kundi moja la wananchi wanaoamini kuwa Mbowe amekamatwa kihalali kabisa Katika makosa anayotuhumiwa nayo ya ugaidi na ushahidi usio na shaka yoyote utatolewa mahakamani kuthibitisha tuhuma zake

Kuna wale tusioamini kabisa kuwa Mbowe ni gaidi na tunaamini pia kuwa, mashitaka haya anayotuhumiwa nayo ni njama tu za watawala ambao ni wanaccm, wakishirikiana kwa karibu Sana na Jeshi "lao" la Polisi Katika kumbambikia kesi kwa kinachoaminika kuwa ni kutaka kudhoofishsa juhudi zake kubwa za kupigania Katiba mpya ya nchi, kwa kumkalisha kipindi kirefu mahabusu, (ifahamike kuwa watuhumiwa wa ugaidi hawana dhamana) baada ya kumwona kama ni "mwiba" wa kuongoza mapambano ya kudai Katiba mpya ya nchi, ambayo watawala wetu hawataki hata kuisikia!

Hebu tujaribu kuchamhua kwa kina makundi haya mawili na tujaribu kuona ni kundi lipi ambalo tunadhani lipo sahihi.

Kwanza tuchambue kundi la kwanza la mapolisi walio-frame makosa hayo wskishirikiana kwa ",karibu" Sana na watawala wetu wa chama cha Sisiem.

Tunaambiwa na Polisi wa nchi hii kuwa Mbowe aligundulika kuwa ni gaidi tokea mwezi Agosti mwaka Jana, baada ya kubainika kuwa anafadhili kikundi cha kigaidi kwa kutumia pesa ya kitanzania shilingi laki sita tu!

Hivi kweli Polisi wetu "wakishirikiana" kwa karibu Sana na watawala wetu wapo serious kweli??

Mbowe isemekane kuwa ni mfadhili mkuu wa kikundi cha kigaidi tokea mwezi Agisti mwaka Jana, halafu asikamatwe Katika kipindi chote hiki, hadi wasubiri aende kwenye kongamano la Katiba mpya Mwanza, inakaribia mwaka mzima sasa, ndipo wamkamate, tena kwenye hoteli aliyofikia jijini Mwanza, tena usiku wa manane, ndipo wadai kuwa wamemkamta "gaidi" Mbowe na watamfikisha mahakamani kujibu mashitaka yake??

Jambo la pili, kama kweli Mbowe alipanga njama za kulipua vituo vya mafuta, mbona sasa hatuelezwi ni lini alipanga njama hizo??

Kama kweli Mbowe ni gaidi, mbona kuna tofauri kubwa mno Kati ya gaidi Mbowe wa TZ na vikundi vingine vya kigaidi vya kimataifa, kama vile Al qaeda, Al Shabaab, Boko haram na ISIS Katika utekelezaji wake wa vikundi vya kigaidi??

Kama kweli Mbowe angelikuwa gaidi, kwa tafdiri ya nemo ugaidi, tungeshashuhudia maafa makubwa ya vifo vya watu na uhahibifu wa hali ya juu wa mali za wananchi.

Kwa kuwa ugaidi ni vitendo vya kikundi fulani cha watu na wala ugaidi siyo suala la "individual as a person" basi tungeendelea kuona vitendo vya vifo vya watu na uhahibifu mkubwa wa mali za watanzania Katika kipindi hiki ambacho "gaidi" Mbowe yupo mahabusu.

Hayo ni maoni yangu Katika tafsiri i ya neno ugaidi na ninavyoona Mimi ugaidi una tafdiri tofauri kabisa kwa Polisi wetu wa nchi hii
Nikuhakikishie, hakuna mwananchi anayeamini kuwa Mbowe ni gaidi, awe mwananchi wa kawaida, awe polisi, awe kiongozi wa serikali, awe mwanaCCM kindakinda au mwanaCCM maslahi.

Nimeongea na baadhi ya makamanda wa polisi na baadhi ya wakuu wa TISS, wote wanasema ni hadithi ya kutengeneza.

Hata wale wanaoshangilia mashtaka ya Mbowe, siyo kwa sababu wanaamini ni gaidi bali wanafurahia Mbowe kuteseka.
 
Back
Top Bottom