SueIsmael
JF-Expert Member
- Dec 11, 2013
- 932
- 1,281
halafu kibaya ziadi watanzania wengi hawafahamu kuwa elimu na afya si sekta za kuongeza pato la taifa ila za kusaidia tu jamii. zitakapojengwa hospitali na shule ni nani atazihudumia kama hakuna uzalishaji kwa sekta za mafuta, nishati na miundombinu? tunataka tufike mahali tuuze elimu kwa gharama kuongeze pato la taifa? hiyo kauli ya huyo mama mfaransa imekaa kushoto sana. kwa hiyo uzalishaji usifanyike kuhudumia sekta zisizozalisha?
Serikali inajukumu la kuhakikisha elimu bora na kuhakikisha afya bora kwa wananchi wake. Hii ni kwa kushirikiana na Sekta Binafsi. Hata hivyo kwa kuwa ni Sekta za huduma muhimu, hapa ndio kodi za wananchi zinatakiwa zitumike kwa ufasaha. Sekta za viwanda, biashara na miundombinu zinapaswa kujengwa na sekta binafsi. Serikali kazi yake ni kuhakikisha mazingira bora ya uwekezaji, kutoa dira ya muda mfupi na muda mrefu, kusimamia sera na kukusanya kodi. Serikali haipaswi kufanya biashara!
Hiyo elimu unayotaka tuuze, ni elimu ipi? umuuzie nani? Tusipowekeza kwenye hiyo elimu ipaswavyo, tutaendelea kuimport wataalam kwenye hizo sekta zinazozalisha na watanzania wengi tutabaki vibarua, mamantilie na wachache kwenye nafasi za kati. Na hata hali hiyo haitodumu kwa muda mrefu maana teknolojia inakuja kunyakuwa hizo kazi ndani ya miaka michache.
Tunaleta mchezo kwenye maisha ya watu. Sasa hivi watanzania tunazidi milioni 55, huku nusu ya idadi ya watu ni chini ya miaka 30. Do the math