Tunaposema maendeleo ya watu badala ya vitu, msikilizeni boss wa IMF, Christine Lagarde

Freesoule

JF-Expert Member
Jun 18, 2013
269
272
Tunapozungumzia maendeleo ya watu badala ya maendeleo ya vitu, CCM na wapambe wa Rais Magufuli huwa hawaelewi kabisa. Trevor Noah kutoka The Daily Show with Trevor Noah anamhoji mkurugenzi wa shirika la fedha duniani (IMF), Bi Christine Lagarde kuelekea mkutano ujao wa mataifa 20 yenye uchumi mkubwa zaidi duniani (the G20).

Trevor Noah anamuuliza Bi Christine Lagarde kwa nini ni muhimu kuwekeza kwenye huduma za kijamii kama hospitali na shule badala ya sekta za kiuchumi zinazotumia mafuta (fossil fuels) ambazo pengine zinadaiwa kukuza uchumi kuliko sekta za kijamii kama hospitali na shule.

Bi Christine Lagarde anaanza kujibu kwa kusema "Kwanza kabisa inasaidia kwa kupunguza matabaka. Kama watoto wadogo kutoka sehemu zote ulimwenguni, hasa zile zenye kipato cha chini, wataweza kwenda shule, watakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi". Anazidi kusema kuwa "wanawake, kwa mfano, badala ya kutembea maili kadhaa kuchota maji, kama ilivyo katika nchi nyingi, wataweza kufikiwa na barabara na kuzitumia hizo barabara kusafirisha maji bila kupoteza muda; ikiwa watoto wanazaliwa hospitalini ambako kuna huduma inayofaa, ni wazi kuwa watakuwa mahala pazuri zaidi maisha yao yote. Kwa hiyo kwa kufanya hivyo unaboresha maisha ya watu, siyo leo, pengine si kesho, lakini ndani ya miaka mitano au kumi ijayo, kwa sababu hilo ni muhimu sana kwa ajili ya baadaye"

Hii ni sehemu ndogo ya wazo zima lakini hata IMF inatambua wazi kuwa ni muhimu zaidi kuwekeza kwenye miradi ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja. Nilitegemea sisi ambao ndio tunapigana na umasikini tungekuwa na uelewa mpana zaidi juu ya hili lakini siyo picha ninayoiona hapa kwetu Tanzania.

Mazungumzo yapo hapa chini na unaweza kutazama hasa kuanzia dakika ya 3:00.

Na tunapoengelea maendeleo ya watu, lazima iwahusishe watu wa madaraja ya chini moja kwa moja.
Sasa mtu ana nunua ndege anakwambia watu wa chini ambao hawafikirii hata kupanda hiyo ndege watakuja kunufaika pale faida itakapopatikana ndio iende ikajenge hospitali, je isipopatikana?
 
Hiyo kauli ya maendeleo ya vitu sijaielewa mpaka leo inamaanisha nini labda mnisaidie. kikawiada vitu vinavyojengwa ni kwa ajili ya watu na maendeleo yao kama ni barabara, reli, nadaraja yote yanajengwa kwa ajili ya watu, hiyo kauli ya maendeleo ya vitu ina mashiko gani?

Maendeleo ya vitu daima hupelekea maendeleo ya watu ila leo watanzania tunalishwa yasiyolika na tunameza bila kutafuna. ni wapi marekani utakuta hakuna lami, reli au viwanja vya ndege? serikali yao ilijenga miundombinu hiyo ili kuwanufaisha watu, kwa nini sio kwetu tz?

Miradi ipi ambayo serikali imeanzisha haiwanufaishi watu? mradi wa SGR umetoa ajira nyingi kwa watanzania, barabara zimerahisha usafirishaji, n.k hiyo yote ni kuonesha miundombinu lazima ilete maendelo ya watu. unachopinga ni nini? Taja walau mradi mmoja ambao watu hawanufaiki au hawatonufaika ukikamilika?
 
halafu kibaya ziadi watanzania wengi hawafahamu kuwa elimu na afya si sekta za kuongeza pato la taifa ila za kusaidia tu jamii. zitakapojengwa hospitali na shule ni nani atazihudumia kama hakuna uzalishaji kwa sekta za mafuta, nishati na miundombinu? tunataka tufike mahali tuuze elimu kwa gharama kuongeze pato la taifa? hiyo kauli ya huyo mama mfaransa imekaa kushoto sana. kwa hiyo uzalishaji usifanyike kuhudumia sekta zisizozalisha?
 
Na tunapoengelea maendeleo ya watu, lazima iwahusishe watu wa madaraja ya chini moja kwa moja.
Sasa mtu ana nunua ndege anakwambia watu wa chini ambao hawafikirii hata kupanda hiyo ndege watakuja kunufaika pale faida itakapopatikana ndio iende ikajenge hospitali, je isipopatikana?
Well said
 
marekani wote wana uwezo wa kupanda ndege ? ufaransa kwa huyo bibi wote wana uwezo wa kupanda ndege?
 
Na tunapoengelea maendeleo ya watu, lazima iwahusishe watu wa madaraja ya chini moja kwa moja.
Sasa mtu ana nunua ndege anakwambia watu wa chini ambao hawafikirii hata kupanda hiyo ndege watakuja kunufaika pale faida itakapopatikana ndio iende ikajenge hospitali, je isipopatikana?
kwa hiyo serikali inunue ndege pale kina mtu akapokuwa ana uwezo wa kupanda?
 
kwa hiyo serikali inunue ndege pale kina mtu akapokuwa ana uwezo wa kupanda?
Serikali hususani hizi nchi zetu maskini ingetakiwa ifanye vitu vya msingi kwa ajili ya manufaa ya watanzania wengi wa hali ya chini.
Mabiashara ya ndege wangewaachia akina precision huko na makampuni mengine binafsi huko
 
Hiyo kauli ya maendeleo ya vitu sijaielewa mpaka leo inamaanisha nini labda mnisaidie. kikawiada vitu vinavyojengwa ni kwa ajili ya watu na maendeleo yao kama ni barabara, reli, nadaraja yote yanajengwa kwa ajili ya watu, hiyo kauli ya maendeleo ya vitu ina mashiko gani?

Maendeleo ya vitu daima hupelekea maendeleo ya watu ila leo watanzania tunalishwa yasiyolika na tunameza bila kutafuna. ni wapi marekani utakuta hakuna lami, reli au viwanja vya ndege? serikali yao ilijenga miundombinu hiyo ili kuwanufaisha watu, kwa nini sio kwetu tz?

Miradi ipi ambayo serikali imeanzisha haiwanufaishi watu? mradi wa SGR umetoa ajira nyingi kwa watanzania, barabara zimerahisha usafirishaji, n.k hiyo yote ni kuonesha miundombinu lazima ilete maendelo ya watu. unachopinga ni nini? Taja walau mradi mmoja ambao watu hawanufaiki au hawatonufaika ukikamilika?
Mkuu, umesema hujaelewa ueleweshwe halafu ukasema tunalishwa yasiyolika. Kweli unataka kueleweshwa au umeelewa ila unataka tu mjadala? Anyway, ntaenda na statement yako ya kwanza.

Nikuulize wewe, hivi kutatua tatizo la maji kwenye miji na majiji mbalimbali nchini na kununua Boeing Dreamliner, kipi ni kipaumbele?

Maendeleo hupatikana kwa kulikuza tabaka la watu wa uchumi wa kati (middle class income) ambao ndio hutumia hata hizo huduma za ndege na treni za kisasa.

Fair enough, ujenzi wa SGR na ununuzi wa ndege unaleta ajira kwa Watanzania, lakini kwa gharama ipi? Wengi wa watoa kauli ya maendeleo ya watu badala ya vitu (akiwemo Julius Nyerere) si kwamba wanapinga kuwa na miundombinu ya kisasa, la hasha. Ila ni kuwa, unapojenga miundombinu kama hiyo utumie hekima. Kujenga hiyo miundombinu kwa kutumia fedha za umma pekee si busara. Uzoefu unaonyesha kuwa ni bora kushirikiana na sekta binafsi (PPP) au uwekezaji wa sekta binafsi. Ukifanya hivyo, mapato ya serikali yanakuwa yanaenda kuboresha huduma kwa wananchi kama vile afya na elimu huku hiyo miradi ikiendelea. Upo hapo?

Ila kinachofanyika sasa ni kuwa fedha za ndani na zile tunazokopa zinaenda kugharamia hiyo miradi mikubwa, ikiziacha huduma muhimu kwa jamii zikikosa fedha. Ndiyo maana unaona hakuna ajira mpya, kukosekana kwa dawa, elimu ikisuasua, kilimo kinapwaya, sijui tutaje vingapi. Ila nadhani mwenyewe pia ni shahidi.

Rais Magufuli alipokuja hadharani na kusema SGR itajengwa kwa fedha za ndani ilikuwa ni ukosefu wa uelewa wa masuala ya maendeleo, na hao wanaoitwa washauri sijui huwa wanafanya kazi gani. Lakini kuna tetesi kuwa bwana Jiwe huwa hashauriki, yeye ni kutumbua tu. Anatengeneza matatizo na kuleta suluhisho ili sifa zimwendee yeye, hana tofauti na hulka ya Rais Trump wa Marekani. Kwa hiyo hata ushauri kama huu sijui kama anaweza kuuzingatia. Hawezi kusoma hata picha haoni, kama wasemavyo wabongo.

Anyway, kwa kumalizia, kauli ya maendeleo ya watu badala ya vitu ndiyo maana yake hiyo. Kwamba maendeleo ya vitu hayawezi kuchukua nafasi ya kwanza. Mapato ya serikali yanapaswa kuwahudumia wananchi moja kwa moja, kwani huwezi kusubiri ujenge SGR kwanza au ATCL ije kupata faida ndipo uwatibu watu, uwapeleke vijana shule, au ndipo uwapatie watu maji safi na salama. Hayo ni mambo ambayo hayawezi kusubiri, labda kama unataka kushuhudia vifo n.k.
 
Hiyo kauli ya maendeleo ya vitu sijaielewa mpaka leo inamaanisha nini labda mnisaidie. kikawiada vitu vinavyojengwa ni kwa ajili ya watu na maendeleo yao kama ni barabara, reli, nadaraja yote yanajengwa kwa ajili ya watu, hiyo kauli ya maendeleo ya vitu ina mashiko gani?

Maendeleo ya vitu daima hupelekea maendeleo ya watu ila leo watanzania tunalishwa yasiyolika na tunameza bila kutafuna. ni wapi marekani utakuta hakuna lami, reli au viwanja vya ndege? serikali yao ilijenga miundombinu hiyo ili kuwanufaisha watu, kwa nini sio kwetu tz?

Miradi ipi ambayo serikali imeanzisha haiwanufaishi watu? mradi wa SGR umetoa ajira nyingi kwa watanzania, barabara zimerahisha usafirishaji, n.k hiyo yote ni kuonesha miundombinu lazima ilete maendelo ya watu. unachopinga ni nini? Taja walau mradi mmoja ambao watu hawanufaiki au hawatonufaika ukikamilika?
Kwahiyo ukisha nunua ndege na kujenga barabara, nini kitabebwa sasa maana viwanda migodi hakuna
 
unataka kumaanisha nini, ? embu eleza hizo pumba unazotaka kueleza, manake naona hujielewi.
huoni umeandika takataka ambazo zinakutapisha mwenyewe, ajabu kwelikweli kwenye jamii na wewe unaitwa msomi. Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya utalii , kwa watalii wa ndani na watalii wa nje na moja ya njia za kukuza na kuimarisha utalii ni kuendeleza miundombinu hususani viwanja vya ndege na kuboresha huduma za ndege. leo taifa linanufaika na utalii kwa sababu ya serikali kuwa na ndege za kuhudumia watalii.

mapato yanayotokana na utalii ambayo yamechagizwa na ununuzi wa ndege yameongezeka na matunda yake yameonekana katika kuendelea kuhudumia huduma za jamii kama afya( ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya 260 na hospitali za wilaya 67), maji( miundombinu ya maji inajengwa kwa kasi), elimu( elimu bure, mikopo elimu ya juu, uboreshaji wa elimu ya veta), hayo ni baadhi tu ya faida za kununua ndege. kwa mawazo yako huduma za jamii zitaboreshwaje bila kuwa na chanzo cha mapato na za uzalishaji?
 
kwa hiyo serikali inunue ndege pale kina mtu akapokuwa ana uwezo wa kupanda?

Kabla ya serikali kununua ndege, hakukuwa na huduma za usafiri wa anga Tanzania? Jambo la kuchekesha ni motive ya Rais Magufuli kuifufua ATCL ati ni "aibu kwa nchi kutokuwa na shirika la ndege"! Kichekesho. Sijui kama kuna malengo ya kujiendesha kwa faida hapo.

Si lazima serikali ijihusishe na biashara ya usafiri wa anga, hata mataifa makubwa kama India yanaachana na hiyo habari, huku mashirika yenye uzoefu Afrika kama South African Airways yakisuasua kibiashara. Tena ubaya ni kuwa hii serikali inaua ushindani ikidhani ndio itafanikiwa, rejea suala la Fastjet Tanzania. Mashirika ya ndege yanayotoa mchango mkubwa kwa wenzetu Marekani, Asia na Ulaya ni mashirika binafsi.

The Indian government is planning to sell its struggling national carrier for $1 billion next year — a much lower price than it had initially hoped for
 
Katika watu waongo Ni huyo boss was IMF .Ulishawahi ona pesa zao wanakopesha kwa ajili ya huduma za jamii? Wakija kukubana ulipe mikopo yao Cha kwanza hutaka serikali ijitoe kutoa huduma za jamii kwani haziongizi pesa na hivyo kufanya mikopo yao isilipike.Hao IMF Sio waumini wa huduma za jamii mwongo mkibwa hiyo.Pesa wao hukopesha kwenye miradi ya maendeleo tu.
 
Hiyo kauli ya maendeleo ya vitu sijaielewa mpaka leo inamaanisha nini labda mnisaidie. kikawiada vitu vinavyojengwa ni kwa ajili ya watu na maendeleo yao kama ni barabara, reli, nadaraja yote yanajengwa kwa ajili ya watu, hiyo kauli ya maendeleo ya vitu ina mashiko gani?

Maendeleo ya vitu daima hupelekea maendeleo ya watu ila leo watanzania tunalishwa yasiyolika na tunameza bila kutafuna. ni wapi marekani utakuta hakuna lami, reli au viwanja vya ndege? serikali yao ilijenga miundombinu hiyo ili kuwanufaisha watu, kwa nini sio kwetu tz?

Miradi ipi ambayo serikali imeanzisha haiwanufaishi watu? mradi wa SGR umetoa ajira nyingi kwa watanzania, barabara zimerahisha usafirishaji, n.k hiyo yote ni kuonesha miundombinu lazima ilete maendelo ya watu. unachopinga ni nini? Taja walau mradi mmoja ambao watu hawanufaiki au hawatonufaika ukikamilika?
Ndege!we unafikiri watu wa Hali ya chini ambao ni % kubwa wapo watapanda?

Ova
 
Kwahiyo ukisha nunua ndege na kujenga barabara, nini kitabebwa sasa maana viwanda migodi hakuna
serikali kwa sasa haina ndege ya mizigo hivyo ndege zinazonunuliwa si za kusafirisha mizigo ila watu. ujenzi wa barabara unachochea ujenzi wa uchumi wa watu wa tabaka la chini kabisa ambao wengi wao ni wakulima na wafanyakazi. mkulima anahitaji barabara , reli n.k kusafirisha mazao yake sokoni? Pia kumbuka kuwa sekta binafsi haiwezi kujenga miundombinu hivyo serikali inatakiwa ifanye hivyo ila maji, afya, elimu zinaweza kutolewa na sekta binafsi na serikali kuingia nao ubia wa cost-sharing
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom