Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,833
- 71,300
Sasa imekuwa kama mchezo wa mazoea, yaani kabla ya 30th March CAG kwenda kumsomea Rais ripoti yake ya ukaguzi kisha kuikabidhi Bungeni na mchezo unaishia hapo.
Mwaka unaofuata hakuna taarifa ya utekelezaji wa ripoti ya nyuma bali watu wanakaa kusikiliza ripoti nyingine.
Ripoti iliyopita ilijaa madudu mpaka yale ya wazi kabisa ya mfano tamasha la urithi lakini ni kama zilipendwa kwa sasa.
Je, hii inatokana na udhaifu wa bunge letu hasa kamati ya PAC ambayo kwa mfumo wa mabunge ya jumuia ya madola lazima iongozwe na upinzani?
Inaonekana Mwendazake aliua upinzani na hasa bungeni ili kamati hii iwe dhaifu isiwajibishe serikali yake kwenye upotevu na uzembe utakao ibuliwa na CAG.
Ni aibu kubwa kwa taifa mtu wa aina hiyo kumtaja kama mzalendo na eti aliipenda nchi yake. Ujinga mtupu, anastahili kuitwa mwizi na haini.
Leo ni 2022 na kusubiri nchi iendelee kupoteza dira hadi 2025 eti kisa uchaguzi wakati tunajua 2020 haukufanyika uchaguzi huo nao ni ujinga pro max, taifa linalojitambua linachukua hatua positive pale linapogundua linapoteza hadhi yake kisa kusubiri baadae.
Ripoti za CAG bila kufanyiwa kazi kila zitokapo ni ubadhilifu mkubwa.