Tunaomkumbuka Rev. Mtikila (RIP)- tunyooshe vidole

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Nadhani ni wakati wa kumuenzi Mchungaji Mtikila.
Huyu jamaa alikuwa anafungua kesi kila kona katika hali ya kutaka kusimamia misingi ya kisheria na kikatiba!
kwa kila lililopindishwa Marehemu Mtikila Enzi za uhai wake alilazimisha linyooshwe!
Mimi leo kwa Tanzania hii, Napata angalau sekunde chache za kumkumbuka, mtu huyu aliyepigania misingi ya utawala bora.
R.I.P Mtikila.
 
RIP Mchungaji Mtikila
 
Mtikila Pamoja na Mapugufu yake Mengi lakini alikuwa na Ujasiri wa kuzungumza anachokiamini bila ya kujali athari!

1) Alitangaza hadharani Chuki zake kwa Uislam mpaka akasambaza Andiko la 'Ugaidi' wa Jk na Mie nilipata Nakala Siku anaisambaza kwny Mkutano wa Jukwaa la Viongozi wa Kikristo 2010. Aliwahi pia kuandika Andiko la Chuki sana la udini kwa Mwinyi 1988 akaliwasilisha NEC ya CCM japo Hakuwa Mwana CCM
2) Hakuwa anaukubali Muungano kwa Ujumla wake sio Akina Seif wanazunguka Mara Mkataba Mara Serikal 3

3) Alikuwa Hamkubali Nyerere na Hilo alilisema Tangu Nyerere akiwa Rais

4) Pamoja na Ukongwe wake hakuwahi kuwa CCM tangu kuzaliwa kwake kwa kuwa aliamini haifai

5) Aliamini Mkapa ni Raia wa Msumbiji na akiongea hadharani tangu Mkapa akiwa Rais

6) Aliamini System ya CCM ilimuua Kolimba na akaamini ya Chadema ilimuua Chacha wangwe na yote hayo Alisema hadharani
7) Alimpinga Kagame Tangu 1994 wakiingia
Madarakani
8) 2015 alimpinga hadharani Edward Lowassa na Muda mfupi baadae ajali ya kawaida ya barabarani ilipoteza uhai wake

Masuala ya Katiba Mpya, Tume huru ya Uchaguzi, Mgombea Binafsi ndio yalikuwa Msingi wa Mapambano yake!

Alikuwa akipeperusha Bendera ya Tanganyika kwenye Maisha yake yote

Nawaza tu Utawala huu sijui Kama na Yeye angenywea Kama kina Mbowe au angeleta Ubishi akumbane na Magu!

Mzee wa 'Kanakwamba'
 
Kwa msio jua MTIKILA kupitia taasisi yake ya liberty international aliwasaidia sana wahutu, pia walikuwa wanafanya utafiti kutafuta ukweli juu ya mauaji ya kimbali ya wanyarwanda, nje ya hapo yeye na taasisi yake kawasaidia sana watu waliokuwa na migogoro ya ardhi....kwa kumbukumbu tu kwenu marehemu john garang yule kiongozi wa SPLM yaani kile chama cha sudan kusini alipokuja Tanzania alifikia kwa mtikila
 
Mara ya mwisho namsikiliza alisema idadi sahihi ya watanzania ni million 58.5 so hizo takwimu za kupikwa kwenye kinachoitwa sensa.
 
Kwa msio jua MTIKILA kupitia taasisi yake ya liberty international aliwasaidia sana wahutu, pia walikuwa wanafanya utafiti kutafuta ukweli juu ya mauaji ya kimbali ya wanyarwanda, nje ya hapo yeye na taasisi yake kawasaidia sana watu waliokuwa na migogoro ya ardhi....kwa kumbukumbu tu kwenu marehemu john garang yule kiongozi wa SPLM yaani kile chama cha sudan kusini alipokuja Tanzania alifikia kwa mtikila

1996 pale IFM aliwahi kubebwa na kutolewa Ukumbini na Maafisa Usalama Baada ya kumbana na kumdhibiti kwa hoja Balozi wa Rwanda alieleta Propaganda zake eti Watutsi laki nane waliuawa na Wahutu
 
1996 pale IFM aliwahi kubebwa na kutolewa Ukumbini na Maafisa Usalama Baada ya kumbana na kumdhibiti kwa hoja Balozi wa Rwanda alieleta Propaganda zake eti Watutsi laki nane waliuawa na Wahutu
AlisiAlisimama na wahutu mpaka dakika za mwisho za uhai wake, wengi waliokuwa wanakimbilia TAnzania walikuwa wanafikia kwa MTIKILA, hata alipokufa mitandao ya kihutu ilionyesha nasikitiko sana, ule waraka wake juu ya mwanyarwanda walio penya TAnzania ulileta sekeseke sana na uliwafumbua macho watu wengi sana
 
Back
Top Bottom