Tunaofunga Kwaresma hii tukutane hapa

Islam005

JF-Expert Member
Nov 1, 2008
3,288
3,320
Kwaresma ni kipindi kitakatifu cha kukumbuka mateso ya bwana Yesu, wakristo tunakumbushwa kumrudia Mungu huku tukitafakari kwa kina maisha yetu katika imani. Wenzetu wana mwezi wa Ramadhani sisi tuna Kwaresma.

Tuliopanga kufunga tuwe tunapeana updates na kutiana moyo. Haijalishia utafanikiwa kufunga siku ngapi.

Pia tuambie kitu gani hutafanya kabisa mwezi huu, binafsi napanga nisiguse hata chupa moja ya ulabu au pombe ya aina yoyote.

UPDATES:

Day 1 haijaenda vizuri kwangu sijui shetani amefanikiwaje kutaka kunirudisha nyuma, nimefanya vitu viwili ambavyo sikutaka kufanya, anyway bado sikati tamaa naamini nina uwezo kabisa wa kusimamia msimamo wangu ngoja niongeze maombi. Pombe sijagusa nashukuru
 
Wale st peters kesho misa saa ngapi nitakuwa maeneo hayo?
Saa 12 asubuhi kwa ajili ya watoto na wanafunzi, saa 11 jioni kwa ajili yetu watu wazima! Hii nimekujibu kwa kanisa la St. Peter's pale Oyster bay, sasa sijui kama ulimaanisha hilo!
 
Saa 12 asubuhi kwa ajili ya watoto na wanafunzi, saa 11 jioni kwa ajili yetu watu wazima! Hii nimekujibu kwa kanisa la St. Peter's pale Oyster bay, sasa sijui kama ulimaanisha hilo!
Asante mkuu maana kuna shughuli zitanibana mitaa hiyo hadi saa 10 hivyo itabidi nisali hapo nashukuru.
 
Kwaresma ni kipindi kitakatifu cha kukumbuka mateso ya bwana Yesu, wakristo tunakumbushwa kumrudia Mungu huku tukitafakari kwa kina maisha yetu katika imani. Wenzetu wana mwezi wa Ramadhani sisi tuna Kwaresma.

Tuliopanga kufunga tuwe tunapeana updates na kutiana moyo. Haijalishia utafanikiwa kufunga siku ngapi.

Pia tuambie kitu gani hutafanya kabisa mwezi huu, binafsi napanga nisiguse hata chupa moja ya ulabu au pombe ya aina yoyote.
Mkifungua mtupe mwaliko
 
Kufunga kwa mtu anayemfuata Kristo ni kila siku haijarishi nikwaresma au sio kwaresma kiukweli ni kwamba

Ukiona unaishi maisha matakatifu kipindi cha kwaresma tu wewe sio mkristo we ni mpagani tu kama wapagani wengine

Hatuwezi mkristo kufanana na upande wa pili ambao wanaacha kula nguruwe kipindi cha mfungo tu

Ukiacha kuishi maisha matakatifu kisa sio kwaresma we ni MPAGANI SIO MKRISTO
 
Back
Top Bottom