Tunamuonea Rais Kikwete?


Kwa wale mnaosubiri hilo Baraza la mawaziri linalokuja nakuombeni muanze kunywa Aspirin msije pata Heart attack bure
 
Wahenga wanasema "Choose your love and love your choice" JK tulimchagua wenyenye na tutake tusitake ni lazima tumpende no matter what! kama ilivyo boga, penda na maua yake!. Tumpende rais wetu na madhaifu yake!.
Pasco

Unataka kutuambia kwa vile tulimchagua kwa mapenzi yetu basi kusiseme hata kama tunaona anatuibia hatekelezi wajibu wake, NO a BIG NO. Hata mke wako uliyemchagua kuishi naye maisha yote huwezi kumpa uhuru wa kufanya atakavyo sembuse huyu wa mkataba wa miaka 10.

Rais hatakiwi kupendwa anatakiwa kuheshimiwa, na ataheshimika tu kwa kutovunja waliyokubaliana kwenye mkataba, kumbuka terms za mkataba wetu ni siku alipotuahidi, Give me your votes I will pay back this and this likiwemo la maisha bora. Yes of course wako watu kama wewe no matter what wrong is doing mtaendelea ku-appreciate hayo mabaya kwa interest zenu siwalaumu. Lakini kwa mtu aliye serious na uchungu na nchi yake na maisha ya baadae ya watoto wote wa taifa hili lazima atasema na kuchukia madhaifu ya rais wake. Wewe endelea kuyapenda madhaifu ya rais wako.
 
Tumshukuru JK yote aliyolitendea taifa hili!. Mnaweza kukuta hata huu utendaji wake ni zawadi kitoka kwa Mungu ili Watanzania tuupate ukombozi wa kweli wa pili baada ya ule wa kutupatia uhuru!.

I Love Tanzania,

Mungu ibariki Tanzania!.

Pasco.

Nahici umeteleza.. So nitaendelea kukupa kaheshima japo mh.. Wanikumbusha yule aliesema JK ni chaguo la Mungu..
 
Inabidi ianze kampeni ya kumpamba Rais wetu kwa maua na sifa; picha zake zibandikwe kila nyumba, magazeti yote yaanze kutangaza habari zake ili asijisikie mnyonge sana na kuwa hapendwi...
 
Kikwete ana wingi wa madini ya hallucination mwilini kwake
 
Hakika hapo ndio mimi binafsi nakili kuwa kasababisha watanzania wengi kufunguka na kuweza kutambua matatizo ya mfumo wao wa kitaifa,mkoa,wilaya,kata mpaka kijiji!!!
 
Inabidi ianze kampeni ya kumpamba Rais wetu kwa maua na sifa; picha zake zibandikwe kila nyumba, magazeti yote yaanze kutangaza habari zake ili asijisikie mnyonge sana na kuwa hapendwi...

TBC wameshaanza. Huwa wanaweka kanda kuonyesha anakotembelea na hotuba anazotoa. Mwisho wanasema ni kwa hisani ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Ni kama vile wanamtangaza zaidi na yale anayofanya kila siku. What a waste!
 
Kumbe mpo wengi msio na shukrani na msiotambua mambo bwelele ambayo Kikwete kawafanyia. Jamani karudisha 'chenji ya rada' hamshukuru?

Mzee, chenji ya rada hajairudisha yeye. Waingereza wenyewe ndio waliochunguza then wakasema. Huyu jamaa kairukia tu juu kwa juu lakini wazungu wale ndo waliianzisha hiyo ishu tena kabla hata che Nkapa hajatoka magogoni..
 

Red color: That's million dollar questions!

Ok watu wake wanatuambia jamaa huwa anajituma, anafanya kazi kwa bidii sana nk nk lakini ikiwa hatuoni matunda then kuna uwezekano huu:

1. Anafanya (kazi zake binafsi) kwa bidii sana lakini ni kwa faida yake mwenyewe (+familia, maswahiba zake)
2. Huwa anadhaniwa kufanya kazi kwa bidii kumbe anazuga - pseudonym
 

Bongolander!
Nakubaliana nawe maisha ndivyo yalivyo. na watanzania (na waafrica kwa ujumla) hatuna tabia ya kujifunza kutokana na makosa! Mfano Dr. Slaa sasa hivi watu wengi wanamuona kama the future candidate for the top office, badala ya kukaa na kujifunza namna ya kuja kuongoza nchi kwa ufanisi au abuni model ya serikali itakayofuta mapungufu yaliyopo, bado anang'ang'ania maandamano ya kila siku na falsafa ya people's power ambayo haitumiki na nchi yoyote humu duniani zaidi ya Libya ya sasa! Akiingia magogoni atakua na jipya lipi? anaweza kuumbuka zaidi ya JK! Dr Slaa akumbuke ku-manage expectations za watanzania after CCM itakuwa sii kazi ya kitoto!
 

Kaka

Swala kubwa linabaki kuwa WATANZANIA wengi wanapitia kipindi cha kuathirika kisaikolojia, watanzania hawa wameonewa, wametukanwa, hawajasikilizwa na hii inapelekea wananchi wengi kuwa na vidonda vya moyoni 'gubu' au grudge kwa sababu wamenyanyaswa, wameibiwa, wametapeliwa, wamegawanywa, wamedhalilishwa na hata matumaini ya maisha yao ya baadae yamesitishwa!

Ikifikia watanzania hawa waka 'tibiwa' yaani pale ambapo wezi wote wa taifa hiili watakapofungwa na kufilisiwa mali zao, pale ambapo ufisadi utakuwa historia....REBIRTH of real government will occur! government of the people for the people! wananchi watarudisha imani kwa viongozi wao

MKJJ utagundua ugonjwa hapo juu hausababishi matatizo kwa kikwete tu.....viongozi wengi nchi hii hawaaminiwi...yaani wanakuwa kama vile 'walewale' mbaya zaidi cancer hii imeingia mpaka nyumba za ibada!

Hata chadema ikishika nchi leo, swala la kwanza ni kudeal na hawa wezi wote...LA wasipofanya hivi....uchungu huu hautafutika kamwe!!!ambapo tutarudi kule kule

symtpoms za ugonjwa huu ni pamoja na watu kutojitokeza kupiga kura...na kuwa wabinafsi zaidi
 

mkuu....hiyo ni stereotyping, haijengi..inabomoa.

nadhani kila mtu awe judged kwa matendo yake na si asili yake....matendo yetu ni chaguo letu lakini asili zetu si chaguo letu(au mkuu ulipata nafasi ya kuchagua asili uliyo nayo, if YES hongera, binafsi sikupata).

i hope unaelewa namaanisha nini!!!!


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…