Tunamlaumu sana Rais lakini tutakuja kumkubali tu

East African

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
704
992
Ndugu wananchi wenzangu
Poleni kwa tishio la njaa, ukame, ukosefu wa hela mfukoni na mengineyo mengi.
Ila nionavyo mimi hali hii ya ukosekanaji wa hela mfukoni ni kama ya muda mfupi. Serikali inachofanya hapa ni kufumua mfumo fulani wa kiuchumi na kuanzisha mpya ambao hatukuuzoea.
Naamini kuanzia mwaka 2018 hadi 2020 tutaona nchi inabadilika sana na tutaanza tena kuona huyu Rais jinsi alivyokuwa makini. Kila mtu atakubali kwa kuwa huduma za kijamii zinaimarika sana, usafiri wa anga na reli utaboreka na umeme utakuwa sio issue tena. Hivyo tusichoke tuendelee kupambana kutafuta hela kwa jasho na hela itapatikana.
Amini niyasemayo na muweke akiba ya maneno
 
Ni hivi, kiongozi anapokua madarakani lazima akosolewe, hakuna ujinga mtupu wataalamu wanasema, ata wale viongozi waliodhaniwa hawakufanya kitu ukiangalia baada ya kutoka madarakani walionekana wamefanya mambo makubwa. Ni vizuri kutafakari mambo kwa upana zaidi. Kimsingi, hali ngumu ya maisha ndiyo inayolalamikiwa na sera zilizopo hazionyeshi matumaini ya kupambana na umasikini bali zinaonekana kama vile zinapambana na masikini kama ilivyowahi kuelezwa kwenye thread moja sikumbuki ni ya nani.Hivyo ni haki ya wananchi kukosoa viongozi wao, wananchi ndiyo waajiri wa viongozi na si vinginevyo hivyo ni haki yao ku appraise performance yao.
 
Watu wanaangalia waliposimama. Ni suala la wazi inawezekana hata leo akitangaza ajira hata 100000 vilio vyote vinakufa kinatafutwa kilio kipya. Malalamiko yametamalaki kila kona hata mwenye nguvu anaacha kufanya kazi anahamasishwa kulalamika na kunung'unika. Malalamiko yaliwasababisha watoto wa yakobo kuzunguka jangwani miaka arobaini safari ya siku Saba.
 
Ndugu wananchi wenzangu
Poleni kwa tishio la njaa, ukame, ukosefu wa hela mfukoni na mengineyo mengi.
Ila nionavyo mimi hali hii ya ukosekanaji wa hela mfukoni ni kama ya muda mfupi. Serikali inachofanya hapa ni kufumua mfumo fulani wa kiuchumi na kuanzisha mpya ambao hatukuuzoea.
Naamini kuanzia mwaka 2018 hadi 2020 tutaona nchi inabadilika sana na tutaanza tena kuona huyu Rais jinsi alivyokuwa makini. Kila mtu atakubali kwa kuwa huduma za kijamii zinaimarika sana, usafiri wa anga na reli utaboreka na umeme utakuwa sio issue tena. Hivyo tusichoke tuendelee kupambana kutafuta hela kwa jasho na hela itapatikana.
Amini niyasemayo na muweke akiba ya maneno

Siyo kweli kwamba tunamlaumu sehemu kubwa ya Watanzania tunamkubali, unaowaona humu ni JF siyo picha ya Tanzania, isistosshe wanalipwa kufanya wanayofanya, hivyo wako kazini!
 
Swala ni muda tu, hata hizo ndege wanazozisema nawaambia baada ya miaka 5 ijayo mtaanza kuona ATCL ni shirika kubwa sana EA. Tusilalamike sana tukosoe positive.
 
Watu wanaangalia waliposimama. Ni suala la wazi inawezekana hata leo akitangaza ajira hata 100000 vilio vyote vinakufa kinatafutwa kilio kipya. Malalamiko yametamalaki kila kona hata mwenye nguvu anaacha kufanya kazi anahamasishwa kulalamika na kunung'unika. Malalamiko yaliwasababisha watoto wa yakobo kuzunguka jangwani miaka arobaini safari ya siku Saba.
Umeona eeeh mkuu
 
Hizo fedha za kuweka mambo vizuri kuanzia 2018 ziko wapi wakati uchumi umeanguka, uzalishaji ndani ya nchi uko hoi na nchi za kigeni hazitoi fedha? Unafahamu miradi mingi ya maendeleo imekwama?
Kama ambavyo raia wamekaukiwa fedha serikali nayo ni hivyo hivyo haina pumzi.
Serikali hii haina sera yoyote ya kiuchumi inayofahamika na inaendeshwa si kwa kufuata utaalamu bali matakwa ya mtu mmoja ambaye hajawahi kuwa mchumi na hayuko tayari kusikiliza mawazo mbadala.
Epuka kuamini vitu kirahisi hasa kwenye masuala ya kuendesha uchumi wa nchi.
 
We unazungumzia 2018 je watakaokufa mwaka huu sababu ya hii hali nao watakuja kufaid na kumkubali?

Anatakiwa kubalance mambo maana hawez kuyatoa yote wakati 1, taratb yatakwsha, lakn sio njaa iachwe hvhv watu wateseke na wafe, Ajira hatoi vjana wateseke mpaka basi je hz chuki na maumivu unafkr hata ukija kumfanyia zuri huyu mtu atasahau? Hawez kusahau kamwe!
 
Hizo fedha za kuweka mambo vizuri kuanzia 2018 ziko wapi wakati uchumi umeanguka, uzalishaji ndani ya nchi uko hoi na nchi za kigeni hazitoi fedha? Unafahamu miradi mingi ya maendeleo imekwama?
Kama ambavyo raia wamekaukiwa fedha serikali nayo ni hivyo hivyo haina pumzi.
Serikali hii haina sera yoyote ya kiuchumi inayofahamika na inaendeshwa si kwa kufuata utaalamu bali matakwa ya mtu mmoja ambaye hajawahi kuwa mchumi na hayuko tayari kusikiliza mawazo mbadala.
Epuka kuamini vitu kirahisi hasa kwenye masuala ya kuendesha uchumi wa nchi.
Sera kuwa nzuri sio sababu ya kuendelea. Kilichokosekana Tz ni udhubutu wa kufanya mambo kwa ujasiri.
 
Labda kama ingekuwa kwamba hiyo nafasi utaichukua wewe ukifika huo mwaka hapo sawa vinginevyo sioni mwenye akili hiyo unayoisemea wewe!!No plan, No vision No creativity & future plan=0
 
Hizo fedha za kuweka mambo vizuri kuanzia 2018 ziko wapi wakati uchumi umeanguka, uzalishaji ndani ya nchi uko hoi na nchi za kigeni hazitoi fedha? Unafahamu miradi mingi ya maendeleo imekwama?
Kama ambavyo raia wamekaukiwa fedha serikali nayo ni hivyo hivyo haina pumzi.
Serikali hii haina sera yoyote ya kiuchumi inayofahamika na inaendeshwa si kwa kufuata utaalamu bali matakwa ya mtu mmoja ambaye hajawahi kuwa mchumi na hayuko tayari kusikiliza mawazo mbadala.
Epuka kuamini vitu kirahisi hasa kwenye masuala ya kuendesha uchumi wa nchi.
Nina wasiwasi hujui hata mana ya sela umekalilishwa tu. Angalia fiscal policy ilivyotengamaa, Angalia monetary policy inavyosifiwa na IMF angalia tax base ilivyo. We hujui lolote kukalilishwa na akina mbowe ambao hawajui lolote zaidi ya kuhamisha ukuta na katafunua tu
 
Lini hasa hayo mambo yatakuwa mazuri?
Kama leo wananchi tunateseka na njaa, halafu rais anajiapiza kabisa kwa kusema hatatoa Chakula, unategemea kuna mema tena hapo?
 
Tuchukulie ni kweli sijui lolote, fafanua tax base itakayofanikisha hayo aliyoyaandika punga mwenzio.

Back
Top Bottom