Tunamdanganya nani kwamba Corona imeisha? Angalia huyu mwanamke aliyetoka nchini kukutwa na Corona huko Namibia

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,704
6,499
Hii nchi maisha yetu yanawekwa hatarini ili kuwafurahisha Watalii, kwamba watalii ni muhimu sana kuliko Watanzania, kwamba bora tufe ila wazungu waje.

Haiwezekani Majirani zetu wote kwa sasa wawe na wagonjwa ila sisi hatuna, tuache kuwafurahisha Watalii, yaani data zina shushwa ili kufurahisha watalii.

Hii ni hatari sana
20200601_071930.jpeg
 
Tatizo sio corona kwisha,tatizo ni lazima maisha yaendelee,kuna maradhi zaidi ya corona,wakati wewe ukiwa unataka watanzania walindwe dhidi ya corona,usisahau kuna watanzania 6000+ hawana ajira,kupitia hizo ajira wanategemewa na familia zao,kula yao imekua ya tabu,hawaijui baadae ama kesho yao,Sasa sijaelewa lengo lako ni uwakinge na corona ila wafe na njaa ama?
 
Serikali ya CCM haijali maisha ya Watanzania. #Hapakazituu kama sie ni punda, ingawa hata wenye punda na wana akili huwa wanajali maisha ya punda wao.

Hivi kama asemayo Waziri Ummy yangekuwa ni kweli WHO na nchi mbalimbali si zingetuma wawakilishi wao kuja kujifunza kwetu tumewezaje kudhibiti haraka hivyo kutoka maziko ya usiku hadi kubaki na wagonjwa wanne tuu?

Wananchi shitukeni, mkiona serikali inawadanganya mchana kweupe imewaona nyie ni wapumbavu mtapiga makofi na hamuwezi kuhoji. Ujinga huo waachieni CCM walio amua kuweka akili zao mfukoni na kushangilia kila kitu hata kama ni kuswagwa kwenda machinjioni kama kondoo.

Octoba iwe mwisho wa kufanywa mazwazwa, maana hata ndani ya CCM wapo walio amua kuwa sasa basi.
 
Maisha yaendelee kwa kudanganya? Kuna wenzetu maisha yanaendelea ila wanatagaza kila kitu. Kwa nini tunaficha? shida iko kwenye kuficha

Shida wananchi wenyewe si ndo tusha kuwa Brainwash?

Huwezi kunywa sumu ukijua eti kwa vile una kiu.
 
Tuache kuwafurahisha watalii
Sina hakika kama watalii nao wanaweza kufanywa wajinga kama wanavyofanywa waTanzania.
Ni mtalii gani anayeweza kuamini taarifa za serikali isiyoamini katika kusema ukweli!

Mtalii anayeamua kuja hapa sasa hivi anakuja baada ya kujiridhisha na taarifa juu ya coronavirus iliyo tofauti na taarifa za uongo zinazotolewa na serikali.

Kwa mfano, atakuwa amejiridhisha kwamba coronavirus ina mwendo tofauti na ule unaoonekana katika nchi zilizoshambuliwa zaidi. Hata kama hajui sababu zinazosababisha hali iwe hivyo.
 
Maisha yaendelee kwa kudanganya? Kuna wenzetu maisha yanaendelea ila wanatagaza kila kitu. Kwa nini tunaficha? shida iko kwenye kuficha
Unafichwa nini?kwanini na wewe usifanye uchunguzi wako kujithibitishia,sio kila unachosikia kutoka kwenye vyombo vya habari unaamini tu,WH0 walitoa tamko mwezi march baada ya week mbili Afrika itaanza kuokota maiti mitaani,wakatabiri hali itakua mbaya kuliko uko kwao,mpaka sasa ni siku 90+,sioni maiti wala mgonjwa.
 
Hii nchi maisha yetu yanawekwa hatarini ili kuwafurahisha Watalii, kwamba watalii ni muhimu sana kuliko Watanzania, kwamba bora tufe ila wazungu waje,

Haiwezekani Majirani zetu wote kwa sasa wawe na wagonjwa ila sisi hatuna, tuache kuwafurahisha Watalii, yaani data zina shushwa ili kufurahisha watalii.

Hii ni hatari sanaView attachment 1465886
Kupungua sio sawa na kuisha. Kila siku unaambiwa imepungua na tuendelee kuchukua tahadhari lakini kwa akili zako za ufipa unataka kumaanisha imekwisha, wewe vipi lakini?
 
Namibia inatumika na mabeberu. Halafu Ummy alivyotuambia kuwa alihenyeka sana na Corona haoni aibu? Eti alihenyeka! Kwa lipi? Kwa kufanya nini? Zaidi nachojua aliruka ruka wiki mbili tu hapo baadaye sijamsikia tena ila leo eti nilihenyeka! Labda alihenyekea vingine ila siyo Corona.
 
Tatizo sio corona kwisha,tatizo ni lazima maisha yaendelee,kuna maradhi zaidi ya corona,wakati wewe ukiwa unataka watanzania walindwe dhidi ya corona,usisahau kuna watanzania 6000+ hawana ajira,kupitia hizo ajira wanategemewa na familia zao,kula yao imekua ya tabu,hawaijui baadae ama kesho yao,Sasa sijaelewa lengo lako ni uwakinge na corona ila wafe na njaa ama?

Mkuu hujamwelewa mleta mada na wewe umeanzisha topic nyingine katika uzi wake. Anasema tu corona haijaisha kama tunavoambiwa. Wanaofanya mass testing ndio tu wanaweza kuonesha kuongezeka au kupungua.

Unachokizungumzia wewe ndicho tulichoamua Tanzania. Kuendelea na shughuli za uchumi ndani ya maambukizi ya corona. Kiichumi hatukufanya uamuzi mbaya, kiafya tumefanya uamuzi mbaya. Kila nchi ilikutwa na chaguo hili na sisi tumechagua moja. Kisicho sahihi ni kusema corona imekwisha!! Matokeo yake hata barakoa, social distancing na hata kunawa mikono kumepungua sana!
 
Ukiona magari ya jeshi yanazunguka mitaani,huku wanajeshi wapo na silaha mkononi na mizinga mizito,broh hata kama hausikii milio ya makombora na maroketi usipe moyo kuwa Amani ipo.
 
Namibia inatumika na mabeberu. Halafu Ummy alivyotuambia kuwa alihenyeka sana na Corona haoni aibu? Eti alihenyeka! Kwa lipi? Kwa kufanya nini? Zaidi nachojua aliruka ruka wiki mbili tu hapo baadaye sijamsikia tena ila leo eti nilihenyeka! Labda alihenyekea vingine ila siyo Corona.
Anatuchosha sana anajua jinsi alivohenyeka mwenyewe asisingizie corona...
 
Back
Top Bottom