Tunalia na Rushwa! Mbona kwenye chaguzi serikali kimya juu ya rushwa?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Nashangaa sana tunasema kwamba kasi ya serikali hii awamu ya tano ni kupambana vikali na Rushwa lakini hatujiulizi ni hatua gani juzi uchaguzi wa Meya jiji la Tanga zilichukuliwa? Hapa rushwa ilitumika wazi wazi, nani aliyeenda kuhoji au kuchunguza kua huyo Meya alipatikanaje? Huyo msimamizi wa uchaguzi alihojiwa na nani kama sio analindwa? Nataka kusema kua hili suala la rushwa ni gumu sana, sina imani kama litawezekana kutokomezwa.

Huwezi kusema mizizi ya rushwa awamu hii itazibwa ilihali msimamizi wa uchaguzi wa mameya Tanga mpaka sasa yupo anatanua tu! Tuliona kwenye kura za maoni CCM kuna baadhi ya watu walikamatwa na TAKUKURU na kuhojiwa masaa kadhaa kisha wakaachiwa na wengine Leo ni mawaziri tunasema serikali hii hakutakua na Rushwa kweli? bado Mimi siamini katika hili! Sina mashaka na Rais wangu,tunajua kwamba anachukia sana rushwa lakini hatuoni sura za watendaji wake kua ni za kukataa rushwa. Mh Rais atafanya kazi katika mazingira magumu mno na ndio maana anaomba kila siku tmwombee.
 
Back
Top Bottom