Tunakokwenda kuna siku Rais wa JMT, ataitwa kuhojiwa na Bunge. Kumbe Rais anaweza kuamrishwa na Bunge na kupangiwa cha kufanya?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Naomba kuanza na angalizo, hii ni thread ya swali na sio statement.

Baada ya CAG kuitwa Kuhojiwa Bungeni licha ya kuwa na kinga ya kikatiba, nilisema humu, tunakokwenda, kuna siku Rais wa JMT ataitwa Kuhojiwa Bungeni.

Dalili za awali zimeanza.
Leo Rais wa JMT ameamrishwa na Bunge, asipeleke Bungeni Ripoti ya CAG iliyosainiwa na CAG Prof. Mussa Assad kwa hoja kuwa Bunge halifanyi kazi na Prof. Assad, hivyo rais ameamriwa asipeleke ripoti hiyo yenye saini ya Prof. Assad na badala yake rais ameamriwa na kupangiwa kazi na Bunge, amsimamishe kazi CAG kwa uchunguzi, ateue Kaimu CAG, zichapwe ripoti mpya, zisainiwe upya ndipo Bunge litapokea.

Amri yenyewe ya kumuamuru rais wetu ni hii
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametoa ufafanuzi juu ya azimio la Bunge la kutokufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa Bunge limeazimia kutofanya kazi na kutoshirikiana na CAG na sio ofisi ya CAG. Kwa mantiki hiyo, ripoti itasomwa endapo haijasainiwa na ASSAD. View attachment 1062521

========

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Bunge lilitangaza kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na si ofisi yake.
Ndugai ametoa kauli hiyo leo mchana Alhamisi Aprili 4, 2019 baada ya kuwatambulisha wageni walioalikwa bungeni, akiweka sawa hali ya sintofahamu iliyoibuka baada ya Bunge kutangaza kutofanya kazi na Profesa Assad.

“Hakuna wakati wowote ambao Bunge limekataa kufanya kazi na taasisi ambayo ni ofisi ya CAG. Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Profesa Assad basi. Tusiripoti tofauti tukauchonganisha umma na kuuchanganya,” amesema Ndugai.

Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa Bunge ni dhaifu.
Chanzo: Mwanan,chi
Japo haijatolewa expressly but impliedly lakini amri ni amri, Rais wa JMT hawezi Kuamrishwa na yoyote, na huwezi kuitenganisha ofisi ya CAG na CAG kama ambavyo huwezi kuitenganisha Ikulu na rais.
,
Ripoti ya CAG ni lazima isainiwe na CAG na ndio mwenye mandate. Ripoti ikiisha kabidhiwa kwa rais wa JMT, ni lazima iwasilishwe Bungeni ndani ya siku 7. Isipo wasilishwa ni ukiukwaji wa katiba.

Ofisi ya CAG iko kwa mujibu wa katiba, Bunge kufanya kazi na CAG ni takwa la kikatiba, Bunge letu limepata wapi uwezo wa kuchagua litafanya kazi na Nani?!

Sasa limefikia hatua ya kumuamuru rais asiwasilishe ripoti yenye saini ya Prof.Assad na badala yake itapokelewa only if sahihi itabadilishwa!, Huku sio kumpangia kazi rais?. Huku sio kumuamrisha rais wa JMT?.

Kwa mujibu wa Katiba yetu Rais wa JMT ni executive president, ni head of state and the Commander in Chief of Defense Forces and Security, hapangiwi, haamrishwi na yoyote, anaweza kutokea ushauri wa yoyote, lakini katika kufikia maamuzi, rais hufikia maamuzi yeye mwenyewe at his own accord. Sasa hili Bunge linalomuamrisha rais wetu, limepata wapi uwezo huo na mamlaka hiyo?!

Kama mimi ndio Rais Magufuli, ningeiwasilisha hiyo Ripoti hivyo hivyo ilivyo na sahihi ya CAG, Prof. Assad halafu nilione hilo Bunge kidume liikatae.
Kitakacho fuata ni kwa rais kulivunja Bunge. CAG yupo hadi mwaka 2023.

Amri yoyote ya kumuamuru rais wa JMT ni amri batili, na ikitokea Rais Magufuli akaamrishwa na akaamrishika, then nitaamini lao moja na hii ita set a very bad precedence ya undermining mamlaka ya Rais wa JMT.

Alihamisi Njema.

Paskali
 
Kaka umenena vyema.. natamani Raisi aende kama mgeni akae nani mule ripoti isomwe.. ikikataliwa.. guess iweje😀

Mimi binafsi hii drama inanishangaza sana.. Spika amechaguliwa na wananchi na anagomea wananchi kupata habari za ukaguzi.. kisa neno "dhaifu".

Nikisikiaga maneno mengine anayotamka na wenzake wakiwa pale kwenye kiti.. huwa nashangaa hawatambui kuwa wananchi wanayasikia pia.

Viongozi wengi wanapambana awamu hii isichafuliwe.. ila kama Bungeni kupo hivi.. at times mtu unatamani kipengele cha katiba kitumike kiwafutilie mbali.. wote waache kutupa drama zinazo poteza muda wa wao kutuwakilisha ili tusikie mema yapi wanayatenda huko..

Tupate habari za mendeleo tukisoma magazeti au kusikiliza habari na sio kufundishana adabu(hii haihusu Wabunge wanaovunja sheria bungeni)

Haya yanaboa na kuharibu kiaina kuzidi kuvutia watu kupenda kuendelea kushangilia lori linaloendeshwa vizuri na Raisi wetu.

Hakuna ubishi neno "dhaifu" linatuonesha wengi limeshupaliwa kuficha maovu.. na kuna maovu yapi huko?
 
Paskali kaka yangu, mbona unasahau mapema???
Baada ya report ya Richmond, maazimio ya mjengoni yalimtaka Rais (JK wakati huo) ampige chini

AG (Johnson Mwanyika)
Mkuu wa PCCB (Edward Hossea)
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati & Madini (Arthur Mwakapugi)
JK alibidi kuwapiga chini AG na Katibu Mkuu (W); sijui nini kilitokea Director HOsea aka-save.

Miaka ikaenda, kuna wakati Katibu Mkuu Nishati & Madini Jairo nae akaingia kwenye 18 za Naibu Spika wakati huo; Job Ndugai; tume ikaundwa, nakumbuka Mkiti alikuwa Ramo Makani... Jairo alibidi kutumbua kiingie mchanga.

Kuna nyakati tena, katibu mkuu (W) Afya, madam Blandina Nyoni, wabunge walikomaa nae na hakupona... the list goes on...
Anyway, huenda Paskali angekuwa Prezdaa angeamua vinginevyo; nakuombea siku ukikalia kiti cha enzi pale magogoni au chamwino, huenda ungefanya vinginevyo.

Anyway, bendera ya kijani, njano, nyeusi, njano na bluee, itaendelea kupepea.

Shalom
 
Huwa unapata picha gani kuwaona wakuu wa mihimili yote ikulu kwenye shughuli ambazo kimsingi zinawahusu media reporters na waandamizi wa ikulu tu?

Unadhani hili linatokea kwa bahati mbaya kipindi ambacho CAG amemkabidhi report Rais? Unajuwa yaliyomo? Unakumbuka ccm imeiondoa serikali kwenye transparent government?, speaker iko Dodoma ila remote iko Dar.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka umenena vyema.. natamani Raisi aende kama mgeni akae nani mule ripoti isomwe.. ikikataliwa.. guess iweje

Mimi binafsi hii drama inanishangaza sana.. Spika amechaguliwa na wananchi na anagomea wananchi kupata habari za ukaguzi.. kisa neno "dhaifu".

Nikisikiaga maneno mengine anayotamka na wenzake wakia pale kwenye kiti.. huwa nashangaa hawatambui kuwa wananchi wanayasikia pia.

Viongozi wengi wanapambana awamu hii isichafuliwe.. ila kama Bungeni kupo hivi.. at times mtu unatamani kipengele cha katiba kitumike kiwafutilie mbali.. wote waache kutupa drama zinazo poteza muda wa wao kutuwakilisha ili tusikie mema yapi wanayatenda huko..

Tupate habari za mendeleo tukisoma magaeti au kusikiliza habari na sio kufundishana adabu( hii haihusu Wabunge wanaovunja sheria bungeni)

Haya yanaboa na kuharibu kiaina kuzidi kuvutia watukupenda kuendelea kushangilia lori linaloendeshwa vizuri na Raisi wetu.

Hakuna ubishi neno "dhaifu" linatuonesha wengi limeshupaliwa kuficha maovu.. na kuna maovu yapi huko?
Hongera kwa kuwa mzalendo kwenye ili
 
Ripoti ya CAG ni lazima isainiwe na CAG na ndio mwenye mandate. Ripoti ikiisha kabidhiwa kwa rais wa JMT, ni lazima iwasilishwe Bungeni ndani ya siku 7. Isipo wasilishwa ni ukiukwaji wa katiba.

Katiba inasema endapo Rais hatawasilisha hiyo ripoti ndani ya siku saba, basi CAG mwenyewe anaiwasilisha kwa Spika au Naibu Spika endapo Spika hayupo.

Kwa mujibu wa Katiba yetu Rais wa JMT ni executive president, ni head of state and the Commander in Chief of Defense Forces and Security, hapangiwi, haamrishwi na yoyote, anaweza kutokea ushauri wa yoyote, lakini katika kufikia maamuzi, rais hufikia maamuzi yeye mwenyewe at his own accord. Sasa hili Bunge linalomuamrisha rais wetu, limepata wapi uwezo huo na mamlaka hiyo?!

Rais Dr John Pombe Magufuli alishaweka wazi kwa kusema 'hapangiwi' na mtu, sasa sijui kama inahusisha na taasisi.
 
Kaka umenena vyema.. natamani Raisi aende kama mgeni akae nani mule ripoti isomwe.. ikikataliwa.. guess iweje

Mimi binafsi hii drama inanishangaza sana.. Spika amechaguliwa na wananchi na anagomea wananchi kupata habari za ukaguzi.. kisa neno "dhaifu".

Nikisikiaga maneno mengine anayotamka na wenzake wakia pale kwenye kiti.. huwa nashangaa hawatambui kuwa wananchi wanayasikia pia.

Viongozi wengi wanapambana awamu hii isichafuliwe.. ila kama Bungeni kupo hivi.. at times mtu unatamani kipengele cha katiba kitumike kiwafutilie mbali.. wote waache kutupa drama zinazo poteza muda wa wao kutuwakilisha ili tusikie mema yapi wanayatenda huko..

Tupate habari za mendeleo tukisoma magaeti au kusikiliza habari na sio kufundishana adabu( hii haihusu Wabunge wanaovunja sheria bungeni)

Haya yanaboa na kuharibu kiaina kuzidi kuvutia watukupenda kuendelea kushangilia lori linaloendeshwa vizuri na Raisi wetu.

Hakuna ubishi neno "dhaifu" linatuonesha wengi limeshupaliwa kuficha maovu.. na kuna maovu yapi huko?
Sahihisho Spika haķuchaguliwa na wananchi balī na wabunge
 
Wanabodi,

Naomba kuanza na angalizo, hii ni thread ya swali na sio statement.

Baada ya CAG kuitwa Kuhojiwa Bungeni licha ya kuwa na kinga ya kikatiba, nilisema humu, tunakokwenda, kuna siku Rais wa JMT ataitwa Kuhojiwa Bungeni.

Dalili za awali zimeanza.
Leo Rais wa JMT ameamrishwa na Bunge, asipeleke Bungeni Ripoti ya CAG iliyosainiwa na CAG Prof. Mussa Assad kwa hoja kuwa Bunge halifanyi kazi na Prof. Assad, hivyo rais ameamriwa asipeleke ripoti hiyo yenye saini ya Prof. Assad na badala yake rais ameamriwa na kupangiwa kazi na Bunge, amsimamishe kazi CAG kwa uchunguzi, ateue Kaimu CAG, zichapwe ripoti mpya, zisainiwe upya ndipo Bunge litapokea.

Amri yenyewe ya kumuamuru rais wetu ni hii

Japo haijatolewa expressly but impliedly lakini amri ni amri, Rais wa JMT hawezi Kuamrishwa na yoyote.
,
Ripoti ya CAG ni lazima isainiwe na CAG na ndio mwenye mandate. Ripoti ikiisha kabidhiwa kwa rais wa JMT, ni lazima iwasilishwe Bungeni ndani ya siku 7. Isipo wasilishwa ni ukiukwaji wa katiba.

Ofisi ya CAG iko kwa mujibu wa katiba, Bunge kufanya kazi na CAG ni takwa la kikatiba, Bunge letu limepata wapi uwezo wa kuchagua litafanya kazi na Nani?!

Sasa limefikia hatua ya kumuamuru rais asiwasilishe ripoti yenye saini ya Prof.Assad na badala yake itapokelewa only if sahihi itabadilishwa!, Huku sio kumpangia kazi rais?. Huku sio kumuamrisha rais wa JMT?.

Kwa mujibu wa Katiba yetu Rais wa JMT ni executive president, ni head of state and the Commander in Chief of Defense Forces and Security, hapangiwi, haamrishwi na yoyote, anaweza kutokea ushauri wa yoyote, lakini katika kufikia maamuzi, rais hufikia maamuzi yeye mwenyewe at his own accord. Sasa hili Bunge linalomuamrisha rais wetu, limepata wapi uwezo huo na mamlaka hiyo?!

Kama mimi ndio Rais Magufuli, ningeiwasilisha hiyo Ripoti hivyo hivyo ilivyo na sahihi ya CAG, Prof. Assad halafu nilione hilo Bunge kidume liikatae.
Kitakacho fuata ni kwa rais kulivunja Bunge. CAG yupo hadi mwaka 2023.

Amri yoyote ya kumuamuru rais wa JMT ni amri batili, na ikitokea Rais Magufuli akaamrishwa na akaamrishika, then nitaamini lao moja na hii ita set a very bad precedence ya undermining mamlaka ya Rais wa JMT.

Alihamisi Njema.

Paskali
Ripoti ikishapokelewa Ikulu biashara imekwisha hayo mambo Assad au alhaj au Prof ama sahihi ni mbwembwe tu za hapo Dodoma!

Pierre..... Juuuuuuu!
 
Leo Rais wa JMT ameamrishwa na Bunge, asipeleke Bungeni Ripoti ya CAG iliyosainiwa na CAG Prof. Mussa Assad kwa hoja kuwa Bunge halifanyi kazi na Prof. Assad, hivyo rais ameamriwa asipeleke ripoti hiyo yenye saini ya Prof. Assad na badala yake rais ameamriwa na kupangiwa kazi na Bunge, amsimamishe kazi CAG kwa uchunguzi, ateue Kaimu CAG, zichapwe ripoti mpya, zisainiwe upya ndipo Bunge litapokea. Paskali

Mkuu Pascal naona tumetoa thread zinazofanana karibu muda sawa!

Kimsingi, Ndugai anamwambia Magufuli Prof Assad unayemtambua kama CAG akikuletea ripoti iishie huko huko Ikulu usituletee huku Bungeni

Inabdi siku moja tukae pamoja kubadilisha mawazo - we seem to think alike sometimes.
 
Back
Top Bottom