Tunajisifu Kukusanya Trilioni 1.4 na Kujisahau Kukuza Uzalishaji

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,334
72,799
Tokea Kaimu Kamishna wa TRA atangaze kuwa makusanyo ya December yamepanda na kufikia Trilion 1.4 sasa kila kiongozi wa kisiasa huo umekuwa wimbo wa kusifia serikali na kujisahau. Hakuna anayejiuliza jee kuna mikakati gani kuhakikisha makusanyo hayo yanatokana zaidi na uzalishaji wa ndani ambao ndio unaokuza uchumi kuliko sasa hivi kutegemea kodi inayotokana na uchuuzi wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje kama redio,toothpics, vitambaa, sabuni nk nk?
Kuna kila dalili za kuridhika na ukusanyaji wa kodi katika uchuuzi huu wa bidhaa za nje tuu
 
Subiri wamalize kwanza kazi ya kuwasimamisha kazi. Huu ni msimu wa Matamko kwanza.
Subiri wamalize kwanza kazi ya kuwasimamisha kazi. Huu ni msimu wa Matamko kwanza.
So tumesema Hapakazitu? Sasa ndio iwe kukusanyaji wa kodi za vibiriti, toilet paper nna sabuni toka China na matamko tuu bila mikakati ya kuzalisha wenyewe?
 
Tokea Kaimu Kamishna wa TRA atangaze kuwa makusanyo ya December yamepanda na kufikia Trilion 1.4 sasa kila kiongozi wa kisiasa huo umekuwa wimbo wa kusifia serikali na kujisahau. Hakuna anayejiuliza jee kuna mikakati gani kuhakikisha makusanyo hayo yanatokana zaidi na uzalishaji wa ndani ambao ndio unaokuza uchumi kuliko sasa hivi kutegemea kodi inayotokana na uchuuzi wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje kama redio,toothpics, vitambaa, sabuni nk nk?
Kuna kila dalili za kuridhika na ukusanyaji wa kodi katika uchuuzi huu wa bidhaa za nje tuu

Hivyo basi ulitaka viwanda vijengwe vya kutengeneza radio , toothpicks n.k yaani TanZania iwe industrialised ndani ya miezi miwili ya Uraisi wa Magufuli? Hata kama Serikali ya Magufuli ingeanza kujenga kiwanda cha kwanza cha kutengeneza tooth picks siku ilipoapishwa mpaka leo hii Kiwanda kingekuwa bado hakijakamilka kujengwa achilia mbali kuanza uzalishaji, sasa kama ktk hali kama hiyo mtu bado analaumu basi nafikiri wewe ndiyo una matatizo na siyo Serikali ya Raisi Magufuli na ningekushauri utatue matatizo yako kwanza wewe kama wewe!
 
Wewe ndio hujielewi.Hujasikia uzalishaji wa ndani wa gesi? Gesi itaanza kuingiza mabilioni ya kodi .Hizo kodi zilizokusanywa umeambiwa break down yake inatokana na kodi za bidhaa za kutoka nje peke yake? Shusha break down ya hizo trilioni zilizokusanywa uthibitishe hiyo hoja yako.

Naona kichwa chako kimejaa siasa za chuki kwa Magufuli ZAIDI kuliko kuzingatia utaalamu
 
Hivyo basi ulitaka viwanda vijengwe vya kutengeneza radio , toothpicks n.k yaani TanZania iwe industrialised ndani ya miezi miwili ya Uraisi wa Magufuli? Hata kama Serikali ya Magufuli ingeanza kujenga kiwanda cha kwanza cha kutengeneza tooth picks siku ilipoapishwa mpaka leo hii Kiwanda kingekuwa bado hakijakamilka kujengwa achilia mbali kuanza uzalishaji, sasa kama ktk hali kama hiyo mtu bado analaumu basi nafikiri wewe ndiyo una matatizo na siyo Serikali ya Raisi Magufuli na ningekushauri utatue matatizo yako kwanza wewe kama wewe!
Tunazungumzia mikakati na mipango kazi ya kueleweka. Miezi miwili bado tuko kwenye kushtukiza na hata hao mawaziri lini umewasikia wanasema wamepanga kufanya nini kupambana na matatizo ya msingi au mbinu za kuanzisha viwanda zaidi ya kufukuzana tuu?
 
Kazi ndio imeanza usianze kulaumu hi serikali ina siku 60 ,ulitaka viwanda vishushwe toka mbinguni? sasa wanatengeneza mfumo wa utawala ,baada ya hapo mambo ya viwanda yatakuja
 
Hata sijui akili yako kama iko sawa!!
Kwahiyo kwa kusema serikali imevuka lengo la makusanyo ya kodi ndio imejisahau????
Acha kulalamika kama mtoto mdogo, sifia pale jambo jema linapofanywa!!!
 
Tunazungumzia mikakati na mipango kazi ya kueleweka. Miezi miwili bado tuko kwenye kushtukiza na hata hao mawaziri lini umewasikia wanasema wamepanga kufanya nini kupambana na matatizo ya msingi au mbinu za kuanzisha viwanda zaidi ya kufukuzana tuu?

Mbona mikakati ya Serikali yake Raisi Magufuli aliielezea pale alipokutana na Wafanyabiashara Ikulu, alisema kila kitu na nini angependa kifanyike na mikakati ipi ataichukuwa yeye kama Mkuu wa Serikali kuwawezesha wawekezaji wa ndani, sasa ulitegemea nini zaidi ya hapo kutoka raisi aliye madarakani kwa miezi miwili tu na hata Mawaziri na Makatibu wakuu hawajamaliza hata mwezi mmoja? Kwanza wengine mpaka leo hawajakadhiwa ofisi bado rasmi?
 
Tunazungumzia mikakati na mipango kazi ya kueleweka. Miezi miwili bado tuko kwenye kushtukiza na hata hao mawaziri lini umewasikia wanasema wamepanga kufanya nini kupambana na matatizo ya msingi au mbinu za kuanzisha viwanda zaidi ya kufukuzana tuu?
Mipango kazi ipo mfano mpango kazi wa bandari na TRA ni kuhakikisha mapato yote yanakusanywa na hakuna kontainer linaondoka bila kulipiwa malipo stahiki.Tatizo ni hao wasimamia hiyo mipango kazi ndio maana wanatumbuliwa mijipu bandari na TRA na sehemu zingine ili mipango kazi iliyopo ifanye kazi na wabakie wale tu wanaoweza kuisimamia.

Kuingia Magufuli si kwamba anaanza kuandika mipango kazi upya.Ipo.Wanachofanya ni kupambana na matatizo ya msingi ambayo ni pamoja na uongozi mbovu na uwepo wa wafanyakazi wabovu bandari ,Tra,mahospitalini nk nk

Huu sio wakati wa viongozi kusimama kuhutubia watafanya nini kutatua matatizo ya msingi .Hotuba zilikuwa wakati wa kampeni saa hii NI KAZI TU.Ukitaka kusikia watafanya nini kutatua matatizo ya msingi rejea kwenye hotuba zao wakati wa kampeni.
 
Tokea Kaimu Kamishna wa TRA atangaze kuwa makusanyo ya December yamepanda na kufikia Trilion 1.4 sasa kila kiongozi wa kisiasa huo umekuwa wimbo wa kusifia serikali na kujisahau. Hakuna anayejiuliza jee kuna mikakati gani kuhakikisha makusanyo hayo yanatokana zaidi na uzalishaji wa ndani ambao ndio unaokuza uchumi kuliko sasa hivi kutegemea kodi inayotokana na uchuuzi wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje kama redio,toothpics, vitambaa, sabuni nk nk?
Kuna kila dalili za kuridhika na ukusanyaji wa kodi katika uchuuzi huu wa bidhaa za nje tuu
Acha chuki mkuu! Rais hana hata siku 90 unaanza kulaumu!! watanzania tuna tabia ya ajabu sana ya kulalamikia kila kitu hata jambo jema linapofanyika! ulitakatiwa kuipongeza Serikali angalau kwa kufikia kukusanya kiasi hicho, japo kuna baadhi ya changamoto za kutatuliwa. pia kumbuka kulikuwa na madudu mengi sana ya serikali iliyopita ambayo bado yanarekebishwa sasa unataka Rais na serikali yake wafanye miujiza ipi ndani ya siku 60?? pia tambua kupanga serikali na mfumo mzuri sio jambo la dk. 1 hasa kama ulikuta mapungufu makubwa ya mtangulizi wako. tujifunze tabia ya ku-appreciate kwanza hasa kitu kizuri kinapofanyikana sio kurusha lawama hovyo!! kwenye mazuri tupongeze kwenye mapungufu tukosoe.
 
Last edited:
Kwani kuna ukusanyaji mpya hapo wa kujisifia? Ongezeko linatokana na watu kulipa deni walilokwepa, wakimaliza deni ndio tuletewe kiwango kipya kinachokusanywa, sio kelele hizi za kupumbaza watanzania. Eti na mtu akapewa uwaziri kwa kukusanya hela ambayo walengwa walipewa wampelekee, jamani hili nalo linahitaji pongezi kweli? kazi ipo.
 
Tokea Kaimu Kamishna wa TRA atangaze kuwa makusanyo ya December yamepanda na kufikia Trilion 1.4 sasa kila kiongozi wa kisiasa huo umekuwa wimbo wa kusifia serikali na kujisahau. Hakuna anayejiuliza jee kuna mikakati gani kuhakikisha makusanyo hayo yanatokana zaidi na uzalishaji wa ndani ambao ndio unaokuza uchumi kuliko sasa hivi kutegemea kodi inayotokana na uchuuzi wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje kama redio,toothpics, vitambaa, sabuni nk nk?
Kuna kila dalili za kuridhika na ukusanyaji wa kodi katika uchuuzi huu wa bidhaa za nje tuu

Ni kweli ndugu yangu pamoja na ukusanyaji kodi tunahitaji uzalishaji. Lakini kila jambo zuri linahitaji mahali pa kuanzia. Sielewi serikali hii ya Magufuli ingeanzaje kutilia maanani uzalishaji bila kuboresha huduma (public services). Na ili kuboresha huduma (public services) kunahitaji funding ambayo chanzo chake kikubwa ni kodi. Hivyo basi hatua anazochukua Magufuli ni miuhimu kwa kukuza uzalishaji. Labda cha muhimu sasa Rais wetu aende hatua ya pili na aanze kuangalia matatizo ya kodi zetu ili wazalishaji wasikwepe kodi, na pia kodi isiwe tuu chanzo cha mapato lakini iwe catalyst ya investment kwa private sector (watu binafsi na makampuni).

Katika mkutano wake na wafanya biashara Raisi alikiri kuna kodi lukuki sizizo na Tija, Je Rais wangu Magufuli lini utaanza reform ya hizi kdoi? Je Dr Mpango amepewa go ahead ya kuanza kubadilisha mifumo hii ya kodi? Katika mfumo huu wa kodi za tanzania viwanda vipya na vilivyoko haviwezi kuzalisha kwa ushindani hivyo biidhaazetu hazitaweza kushindana. Ukwepaji wa kodi ulikuwa unaifanya serikali itegemee kodi chache wafanyakazi (Paye) na makampuni machache hivyo mengi yalibuni mifumo ya ukwepaji. Asilimia kubwa ya kodi inatokana na uingizaji vitu vinavyotokana na viwanda vya wenzetu - hii ni sawa kwasasa lakini tujaribu baada ya miaka 10 tusiendelee kuwa uchumi wa wachuuzi.
 
Sasà hivi ni matamko na kufukuza tu, kiwanda cha toothpick tutaanza kujenga 2019 ili tuingie nayo kwenye kampeni
 
.Nchi ili iwe inakua vizuri kiuchumi ni lazima ikusanye walau asilimia 25 ya GDP.Sasa kwahiyo trilion 1.4 hata asilimia 15 hatujafika
Hii hesabu rudi ukafanye upya.Hizo trilioni 1.4 ni makusanyo kwa mwezi december hiyo 15% ya GDP umeipigaje umechukua GDP ya mwezi December?
 
Acha chuki mkuu! Rais hana hata siku 90 unaanza kulaumu!! watanzania tuna tabia ya ajabu sana ya kulalamikia kila kitu hata jambo jema linapofanyika! ulitakatiwa kuipongeza Serikali angalau kwa kufikia kukusanya kiasi hicho, japo kuna baadhi ya changamoto za kutatuliwa. pia kumbuka kulikuwa na madudu mengi sana ya serikali iliyopita ambayo bado yanarekebishwa sasa unataka Rais na serikali yake wafanye miujiza ipi ndani ya siku 60?? pia tambua kupanga serikali na mfumo mzuri sio jambo la dk. 1 hasa kama ulikuta mapungufu makubwa ya mtangulizi wako. tujifunze tabia ya ku-appreciate kwanza hasa kitu kizuri kinapofanyikana sio kurusha lawama hovyo!! kwenye mazuri tupongeze kwenye mapungufu tupongeze.
Mkuu kuna jambo halijaeleweka hapa, mie sijalaumu ila nimezungumzia wale wanasiasa ambao wamejisahau na kufurahishwa na ukusanyaji wa Trilion 1.4 kama vile kwa mtindo huo wa kukusanya Kodi kubwa kutoka katika uchuuzi wa bidhaa za nje ndio utalitoa taifa hili kwenye Lindi la umasikini.
Mpaka sasa hawa mawaziri wangeonyesha mbinu mpya hata katika kukuza viwanda vidogo vidogo, kilimo na uvuvi ili wakati tukielekea kwenye uchumi wa viwanda vikubwa maisha ya wananchi yaonekane kubadilika na tujikute tunakusanya kodi zaidi kutoka katika uzalishaji wetu badala ya kutulundikia bidhaa za nje ambazo leo tunakusanya Tshs na kesho tunatoa USD kuwapa wakanunue products hizo huko nje.
Lengo la thread sio kulaumu juhudi ila kulaumu kujisahau
 
Tuipe serikali muda. kukuza uchumi sio suala la kutamka tu linahitaji mikakati mizuri.
 
Niko supermarket kuna aina kama 6 za juice lakini za humu ndani ni aina moja tu ya azam... kuna maziwa aina 5 tofauti na viwanda tofauti lakini aina moja kutoka ndani ni ya azam tu.. na wateja wangu wanasema bayana wanapenda kuchangia kwa bidhaa za ndani ila tatizo hazina ubora...wotee wananiuliza bidhaa za kenya.
Serikali lazima ifanye jambo si kila siku kuvizia watumishi inabidi iwape uhuru wawe creative...huu uoga kwa serikali sioni mabadiliko kama tra watakuwa busy kukusanya kodi huku wakisahau wajibu wao mwingine wa kuwaelimisha wafanya biashara.. kuongeza wigo wa soko la ndani...naiona tz ikizidi kuwa dampo la bidhaa na bidhaa zitapanda mara dufu kwa sababu hakuna uzalishaji wa ndani... na bidhaa za ndani hazina ubora kabisa..
 
Back
Top Bottom