Tafakuri Mwalimu Kmaro, amchambua Mr Clean kinagaubaga

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
IMG-20231209-WA0084.jpg

TAFAKURI YANGU KATIKA SIKU HII YA KUADHIMISHA MIAKA 62 YA UHURU

Anaandika Mwalimu Zuberi Kimaro wa Kyeer, Machame

Kwanza Hongera sana kwako Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, kwako nimeridhika 100%, utendaji wako hauna mashaka kabisa, ni fact ambayo wanasheria huiita undisputed one!

Leo nataka niseme upande wa Mawaziri ambao technically ndo wasaidizi wako wa karibu zaidi ya Rais na ambao hutoa tafsiri ya vision ya Rais aliyepo kwa mujibu wa Ibara ya 54(3) ya Katiba ya Tanzania.

Katika kutafsiri vision yako Mh Rais ambayo iko centred katika dhana ya kimageuzi kwenye zile 4Rs zako wapo Mawaziri kadhaa wanaofanya vema kutafsiri hii vision ya MAMA ambao wanafit kukaa kwenye hii tafakuri ila mie ninae mmoja tu Waziri wa Fedha MR CLEAN.

Kwanza Waziri wa Fedha kitaalamu ndio Mchumi No. 1, huyu Waziri ndio Architect wa mifumo ya kiuchumi ya Nchi, ndiye mwenye mandates ya kuset shilingi iweje, GDP iweje, inflation rate iweje etc. Ni huyu ndiye anaetafsiri vision ya Mh Rais katika mawanda ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa Tafakuri yangu leo inaniambia, Waziri wa sasa wa Fedha amefanikiwa sana kutafsiri maono yako katika angle ya kiuchumi na honestly kwa upande wa mawaziri wote kwangu mimi huyu, Waziri wa Fedha Dr. Mwigulu Nchemba a.k.a “Mr. Clean” ndio waziri namba moja (1) anayetekeleza kikamilifu maono yako na hapa nitaenda kwa data kwa maeneo Kadhaa ya mfano!

1. Maono ya Rais ni watoto wote masikini wapate elimu bila ada, na wapate mikopo. Hili hata halikuwa gumu, Mr. Clean ametoa fedha za elimu bure shule zote msingi na sekondari, na mikopo vyuo vyote vya kati, elimu na vikuu. Tumeona shule mpya zikijengwa kamilifu kabisa bila michango.

2). Maono ya Mama Samia ilikuwa kufungua barabara vijijini, Mr. Clean akaanzisha tozo na matusi tukampa. Sasa TARURA wanafedha kutoka 200B nasikia sasahivi zimefika 1.4 trillion. Mr Clean alikuwa mbele ya muda sana. Tozo zimekuwa muarobaini wa tatizo la barabara nchini.

3. Rais maono yako ni kuwa na uchumi imara na unaohakisi katika mifuko ya wananchi, Chini yako maelekezo yako, huyu Mr Clean amebadilisha uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa, huku Pato la Taifa likiongezeka kutoka USD $69.7 bilioni mwaka 2021 hadi USD $85.42 bilioni mwaka 2023. Ukuaji wa uchumi wa nchi umekuwa wa kuvutia, unaakisi maisha ya watu, na uko katika muelekeo sahihi.

4. Rais Samia maono yako ya kufanyika kwa reforms/ mageuzi kadhaa kukuza uchumi wa Tanzania yamesimamiwa na Mr Clean, Mfano; uliamua kuimarisha sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na ufanisi, na mengi yamepatikana kwa kuanzisha ruzuku na mikopo mbalimbali ya serikali. Aidha, sera za uliberali wa biashara kwa njia ya ushuru wa bidhaa zinazoingizwa na ushuru wa huduma za fedha zilizotumwa nje zimewezesha fursa kubwa zaidi za biashara na uwekezaji.

5). Rais maono yako yamekuwa ni kuboresha afya, Kijana wako Mr. Clean amekeleza hilo, tumesikia MRI hospitali zote kanda, CT scan mikoa yote, tayari bajeti ya Wizara ya Afya imeongezeka sana.

6. Maono ya Mheshimiwa Rais ilikuwa ni kumaliza tatizo la maji, wote tunashuhudia Mr Clean amemimina Fedha za kununua Mitambo ya Maji, na hivi sasa inapikana kila mkoa, Visima kila kona ya nchi, Fedha zimeenda kukwamua miradi iliyokufa na kuanzisha mipya ya kutosha. Hongera sana Mama Samia.

7. Maono ya Mama ni umeme ufike kila kitongoji cha Taifa hili, Mr Clean amemwaga mapesa kila kitongoji sasa kina umeme na kazi inaendelea kila pembe ya nchi kuhakikisha upatikanaji wa umeme sio kilio tena.

8. Maono ya Mama Samia ni kuona, miradi ya kimkakati ikamilike na kuanzisha miradi mingine mipya, Mr Clean kasimamia hilo Fedha zinatiririka kwenye Miradi yote, hakuna kilichosimama, kazi zinasonga, hongera Mama Samia.

9. Maono ya Mama Samia ni kuona udhibiti ubadhirifu wa fedha za umma, Mr Clean amemwongeza bajeti Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG na kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi wa ndani. Hongera Dr Samia.

10.Maono ya Mama Samia ni kuona watu wote wanalipa kodi kwa amani, Mr Clean amesimamia hilo tumeona TRA wakiacha kutumia mabavu kwenye ukusanyaji wa kodi na hii imeongeza mara dufu makusanyo hayo kwa mwaka. Hongera sana Dkt Samia.

11. Maono ya Mama Samia ni kuona watumishi wa Umma wanapata stahiki nzuri na kwa muda mwafaka, Mr Clean amesimamia hilo tayari mishahara imepanda mara kadhaa kila mwaka wa kibajeti, hakuna kilichosimamishwa, marypurupu yakutosha kwa kila mtumishi. Hongera Mama Samia.

Haya mambo yanahitaji big minds za kiuchumi na Wizara Vibrants za Fedha ili kuweka uelekeo huu wa kisera sahihi.

Zaidi ya yote Miaka 62 ya Uhuru inatupa nafasi nzuri sana ya shukrani kwa MUNGU kwa ajili yako, lakini zaidi inatupa nafasi kufanya tafakuri ya harakati zetu za mapigano kuelekea uhuru wa Kiuchumi ambapo askari mithiri wa Dr. Mwigulu Nchemba MR CLEAN ni watu muhimu sana kutufikisha huko. We need cleat fiscal policies to navigate through your 4Rs, tunahitaji watafsiri sahihi wa maono yako kama ambavyo Mr. Clean anaonesha njia na kwa mujibu wa tafakuri yangu ni huyu ni Waziri Bora.
 
Haya

Kila nikikumbuka MoU ya Kanisa na Lowassa alivyokatwa 2015 Bila sababu maalumu huku Kamilius akiachwa huwa nacheka sana!
 
View attachment 2837973

Piga makofi!
 
Kiufupi wewe ni msomi ila umeamua kujitoa akili na kuandika vitu virahisi ambavyo mtanzania Mjinga akiona anaelewa ni kweli wakati mambo ya Msingi yameachwa.
 
Back
Top Bottom