Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,018
- 144,377
Tukubali tu sisi waafrika ni tuna tatizo kuanzia akili zetu,n.k ukilinganisha na wenzetu wenye rangi nyeupe wanaotumia vizuri maliasili zao na akili zao kupitia teknolijia walizonazo kujiletea maendeleo tofauti kabisa na sisi waafrika.
Moja ya sababu kwanini sisi ni masikini ni kwasababu hatuzalishi katika nchi zetu(bidhaa za viwandani,kilimo,n.k) na badala yake tunaaagiza zaidi bidhaa kutoka nje tena bidhaa ambazo zinauzwa kwa bei ghali na bado tunaona ni ufahari. Hakika Inasikitisha sana!
Yaani badala ya sisi kujisifu kuongeza exportation ya bidhaa zinazozalisha katika nchi zetu na zilizoongezewa thamani(hasa bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo na mifugo pamoja na madini), sisi tunaona ufahari ku-import bidhaa za thamani kubwa kutoka nje ya nchi hasa ulaya na Marekani!
Kiongozi makini na mwenye vision wa nchi ya kiafrika ni yule ambae atajivuna kwa kuwa na rekodi ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na madini na ambazo zinauzwa nje ya nchi zikiwa processed(zimeongezewa thamani) tangu aingie ofisini.
Badala yake,kiongozi wa kiafrika anakuwa busy na anatumia nguvu kubwa kuitangaza bidhaa alioinunua kutoka Ulaya(anakuwa-bila kujijua- manager masoko wa bidhaa za makampuni ya kibeberu) na wakati huo huo, analaumu hao wanaoitwa mabeberu kwa mambo mengi tu.
Mabeberu hawa wanaposhiriki kutangaza kuwa nchi fulani kutoka Afrika imekuwa ya kwanza kununua bidhaa fulani kutoka kwao sio kama wanawasifu, bali wanatumia fursa hiyo kujitangaza kibiashara na kuwafanye mshindane kuagiza bidhaa zao.
Kwa lugha nyingine,tunaona ufahari kutumia kodi zetu kuagiza bidhaa ghali kutoka nje na hivyo kuwatengeneza ajira watu wa mataifa mengine kuliko kutumia fedha zetu kuongeza uzalisha wa bidhaa humu ndani ya nchi na kuzi-process ili kuziongezea thamani kabla ya kuziuza na tukawa tumetengeneza ajira kwa watu wetu na pia tukaingiza fedha za kigeni na kuimarisha currency zetu.
Kwangu mimi, kiongozi bora wa nchi zetu za kiafrika ni yule ambae angejivuna kwa kuwa na rekodi ya kuongeza uzalishaji katika nchi yake na pia exportation ya bidhaa ambazo ni processed na kisha fedha zinazopatikana kutokana na kuongeza uzalishaji na exportation kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi yake zikiwemo ndege,n.k na si kukopa mpaka kupitiliza na kukamua wananchi wake kodi kubwa zisizoendana na vipato vya watu wake huku akiathiri vipato na mitaji yao.
Vile vile tutambue watu wetu wakiwa na ajira kupitia kilimo processing industries, uchimbaji wa madini,n.k, uchumi ukaaimarika na vipato vya watu vikaongezeka, mbali na kuongeza mapato ya nchi kupitia shughuli hizo za uzalishaji na exportation,pia wataongeza mapato ya nchi kupita PAYE,na hata hizi ndege nazo pia ziapata abira kwani watu wengi zaidi wata-afford kusafiri na nazo na hata SGR itapata mizigo zaidi ya kubeba na kutengeneza faida.
No wonder Wachina wanatamani ziwa Victoria,sisi tunatamani ku-import ndege za kisasa kutoka Ulaya na Marekani.Tumelogwa!
Waafrika tumekosa viongozi wenye vision na wanaolewa kwanini nchi zetu ni masikini na wanaotakiwa wajue wafanye nini kututoa hapa tulipo.